Ukija mjini lazima ukutane na haya:
1. Watu kujilundika kwa meza za muuza magazeti, halafu wakitoka hapo ni wengi wa habariii kama wamesoma habari nzima....
2. Karibia kila raia anamiliki Nokia Tochi ili kujiepusha kuibiwa BB, Samsung, iPhone nyakati za usiku au purukushani....
3. Daladala huwa haijai kwani sio ndoo ya maji, na wakati wowote inaweza kubadili ruti....
4. Hakuna muda maalumu wa kufungua au kufunga baa....
5. Karibia kila mwanamke anavaa suruali, haya mambo kijijini hakuna kabisaaaa...
6. Mjini huwezi kushuhudia nywele za mwanamke ng'oo maana huwa wanavaa nywele za MAITI wa KIHINDI na KIARABU...
7. Ndio sehemu pekee wanawake wanamili VIRIBA TUMBO...
Niendeleeeee???