Mambo matano ya awali niliyoyaona kwa Rais Samia

Joined
Oct 13, 2018
Posts
35
Reaction score
260
Na Thadei Ole Mushi.

1. Mpaka saa Hakuna Mvujo wa Taarifa za Serikali. Hakuna anayeweza kunusa kabisa nini kinaweza kutokea. Zimebaki kuwa confidential kwa asilimia 💯.

2. Viongozi waliopo kwenye Utumishi wa Umma wawe makini Sana. Kwa muda mfupi niliomsoma Mama anataka viongozi wenye Discipline ya kutosha. Kwa kumuangalia Usoni haogopeshi Ila maamuzi yake yanaogopesha Sana.

3. Kuondolewa kwa Gelasius Gasper Byakanwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ni muendelezo wa kuelekea kwenye Political reconciliation. Huyu mkuu wa Mkoa ni yule aliyevunja Green House ya Mbowe kule Hai na kupewa promotion toka kuwa mkuu wa Wilaya hadi Mkuu wa Mkoa. Kuna kitu watu hawajakielewa, Mama anataka kuyaleta makundi yote Pamoja. Kuna watu bado wapo kwenye Enzi za matumizi ya Nguvu badala ya akili. Kwa walioteuliwa Mpaka sasa kumbukeni Hili zama zimebadilika.

4. Jambo Lingine naloliona kwa sasa Mama anasikiliza Sana anaowaongoza. Hapo nyuma Kidogo watu wangeweza kupiga kelele kuhusu uadilifu wa Mtu flan lakini mamlaka ikamuacha tu as long as wanaolalamika ni wapinzani. Kwa sasa viongozi wanaoteuliwa pona yao ipo kwa wananchi... Yaani wananchi wakikuchukia utatolewa. Niwahusie wote walioteuliwa Mpaka sasa kuwa mtaji wao upo kwa wananchi. Kiwango Cha kukubalika na wananchi kitaamua umri wako kwenye nafasi uliyopewa.

5. Vipengele Muhimu katika uongozi vimeshaonekana (Power & Authority). Power uwezo wa Ku influence wengine kufanya au kutokufanya jambo flani. Cha pili ni Authority, huu ni uwezo wa kumshurutisha mtu kuacha au kufanya jambo flan "Mamlaka" ambayo kutokana na kazi yako na nafasi yako kazini unakuwa na mamlaka ya kumwamrisha wa chini yako au unaowaongoza.

Kauli Moja tu ya "Kudemka" ilitosha kunyamazisha wabunge na mijadala yao ya kumfananisha na Hayati Dkt. John Magufuli.

Ole Mushi
0712702602

FB_IMG_1621143308072.jpg
 
Kumbe aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara hakuwa na tofauti na kina Makonda walivyopatikana, nilimuona amekosea alivyoamua kumzika aliekuwa Mkuu wa Wilaya ya Mtwara E. Mmanda huko huko badala ya kumsafirisha kwenda kumzika kwao Kilimanjaro.
 
Kwa sasa viongozi wanaoteuliwa pona yao ipo kwa wananchi... Yaani wananchi wakikuchukia utatolewa. Niwahusie wote walioteuliwa Mpaka sasa kuwa mtaji wao upo kwa wananchi. Kiwango Cha kukubalika na wananchi kitaamua umri wako kwenye nafasi uliyopewa.
Mbona aliwaambia atawatimua kwa mabango ya wananchi
 
Kuondolewa kwa Gelasius Gasper Byakanwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ni muendelezo wa kuelekea kwenye Political reconciliation.
Hivi huwa inakuwaje hapa kama huyo RC alikuwa ziarani somewhere na tangazo linamkuta njiani na bendera, na nyumbani je nako anahama siku hiyohiyo, maana miungu watu huwa wanaona kama hawatakuwa na kikomo
 
Na Thadei Ole Mushi.

1. Mpaka saa Hakuna Mvujo wa Taarifa za Serikali. Hakuna anayeweza kunusa kabisa nini kinaweza kutokea. Zimebaki kuwa confidential kwa asilimia [emoji817].

2. Viongozi waliopo kwenye Utumishi wa Umma wawe makini Sana. Kwa muda mfupi niliomsoma Mama anataka viongozi wenye Discipline ya kutosha. Kwa kumuangalia Usoni haogopeshi Ila maamuzi yake yanaogopesha Sana.

3. Kuondolewa kwa Gelasius Gasper Byakanwa Mkuu wa Mkoa wa Mtwara ni muendelezo wa kuelekea kwenye Political reconciliation. Huyu mkuu wa Mkoa ni yule aliyevunja Green House ya Mbowe kule Hai na kupewa promotion toka kuwa mkuu wa Wilaya hadi Mkuu wa Mkoa. Kuna kitu watu hawajakielewa, Mama anataka kuyaleta makundi yote Pamoja. Kuna watu bado wapo kwenye Enzi za matumizi ya Nguvu badala ya akili. Kwa walioteuliwa Mpaka sasa kumbukeni Hili zama zimebadilika.

4. Jambo Lingine naloliona kwa sasa Mama anasikiliza Sana anaowaongoza. Hapo nyuma Kidogo watu wangeweza kupiga kelele kuhusu uadilifu wa Mtu flan lakini mamlaka ikamuacha tu as long as wanaolalamika ni wapinzani. Kwa sasa viongozi wanaoteuliwa pona yao ipo kwa wananchi... Yaani wananchi wakikuchukia utatolewa. Niwahusie wote walioteuliwa Mpaka sasa kuwa mtaji wao upo kwa wananchi. Kiwango Cha kukubalika na wananchi kitaamua umri wako kwenye nafasi uliyopewa.

5. Vipengele Muhimu katika uongozi vimeshaonekana (Power & Authority). Power uwezo wa Ku influence wengine kufanya au kutokufanya jambo flani. Cha pili ni Authority, huu ni uwezo wa kumshurutisha mtu kuacha au kufanya jambo flan "Mamlaka" ambayo kutokana na kazi yako na nafasi yako kazini unakuwa na mamlaka ya kumwamrisha wa chini yako au unaowaongoza.

Kauli Moja tu ya "Kudemka" ilitosha kunyamazisha wabunge na mijadala yao ya kumfananisha na Hayati Dkt. John Magufuli.

Ole Mushi
0712702602

View attachment 1786654
Ni suala la mda tu uvujaji wa siri za serikali linafanyiwa na watumishi wa juu wa serikali subiri kdgo tu watu wajiakikishie nafasi zao,
 
Kama sijakosea Mwendazake kwa mara ya kwanza kabisa alikwenda na jina la PM bungeni kwenye karatasi aliyoandika kwa mkono tena aliipeleka mwenyewe[emoji23][emoji1787]
Kwa maana hakuwa na ADC?
 
Back
Top Bottom