Mambo mabaya kwenye simu ambayo ulimwengu wa Tech unalazimisha tuone ni ya kawaida

Yani uhame brand ya simu unayoipenda kisa chaja? Sidhani
Labda kama unazitaka sana Fast charger za Mchina, dakika 9 tu simu imeshajaa
Mchina kwenye fast charge hana mpinzani pia anakupa chaji, headphone, cover na glass protector sasa hapo anaachaje kuuza? Shida ya mchina ni software yake tu ndo kapitwa na wengine
 
Mchina kwenye fast charge hana mpinzani pia anakupa chaji, headphone, cover na glass protector sasa hapo anaachaje kuuza? Shida ya mchina ni software yake tu ndo kapitwa na wengine
Shida ya software za Mchina ni bloatware tu, tena zinafutika. Ukishafuta bloatware umemaliza kazi
Anakupa features kibao mpaka unajiuliza umekosa nini
 
Hiyo haijawa copied wala pasted wala translated. Kuna mtu Twitter alitaja hizo point, yeye alitaja tu point bila maelezo. Hayo maelezo nimeyaandika mwenyewe na point nyingine nimeziongeza mwenyewe.
Pia mifano ya simu nimeitaja mwenyewe

Anyway itabidi nirudi Twitter nikaitafute hiyo Source nakuletea muda si mrefu usijali.
Kwanza huko juu nilishaandika Source ni Twitter kwa hiyo usije ukadhani sijui ni wapi ulikotoa hiyo point ya Copy na Paste

Halafu hiyo point yako inayofuata mbona sijakuelewa. Unasema niwe "nachanganua" Kuchanganua maana yake ni kufafanua, mbona nimeleta mifano na maelezo kabisa hapo juu, au kusoma ni shida? Unamaanisha Kuchanganua nini?
Halafu unasema nisitegemee kuona iOS na Samsung wanaleta USB Type C?????
Kwanza iOS ni operating system na Samsung ni simu, unaongelea mambo mawili tofauti. Pili iPhone na Samsung tayari zinatumia USB Type C kwa hiyo sielewi unachokiongelea hapa.
Hapo juu imeongelewa USB Type C 3.x sasa sielewi nini hujakielewa.

Soma vizuri, ni aidha hujaelewa nini naongelea au ulisoma haraka ili uje kumuattack mleta mada

Source nimeshakuwekea
Msamehe huyo kenge.
 
Hazifutiki mzee mpaka u root simu, pia xiomi zinakula bando kupita kawaida shida nn?
Sasahivi zinafutika.
Umeona MIUI 14 inafuta bloatware zote kasoro apps 8 tu za muhimu. Nyingine zinafutika, maybe MIUI 11 ndio ilikuwa na apps nyingi zisizofutika, hata hivyo Redmi 9 imeshapata MIUI 14

Usipowasha Data saver MB zako lazima ziende. Kutokana na bloatware nyingi ambazo hujazifuta ukiwasha data zile apps zinatumia MB zako in the background
Unaweza kublock pia zisiaccess MB zako
Solution ni kuwasha Data saver
 
Mchina kwenye fast charge hana mpinzani pia anakupa chaji, headphone, cover na glass protector sasa hapo anaachaje kuuza? Shida ya mchina ni software yake tu ndo kapitwa na wengine
Hao wachina fast charger kali wanaotoa ni wachache tu, hizi lowend labda ila hizo fast charging nzuri unanunua separate na bei ndefu hadi laki mpaka laki na nusu.

Nimetest s20 na 15W ya Samsung pamoja na 27W ya Xiaomi zote zimedunda hakuna inayopeleka zaidi ya 10W,

Pia nimeangalia A24 inasuport Pd+pps charger, ina maana hata Quickcharge kwako haikufai (tech ya Qualcomm).

Tafuta Samsung 25W kama utapata, alternative tafuta pd charger yoyote, na Max kujaza simu yako ni kama saa 1 na nusu, sema kutunza battery lako set ijae kwenye asilimia 85 hivi, utapunguza muda wa kuchaji na pia utatunza betri.
 
Ila naona Wachina wanajitahidi ku include charger kwenye box hata kwenye simu zao premium, charger za 120W, 100W, 90W, 165W na 210W unazikuta kwenye box kabisa

Ile Redmi Note 12 Discovery Edition nimeona inakuja na 210W fast charger (9 min charging time). Motorola, Oppo, Vivo, Realme, One Plus na Xiaomi naona wanaweka sana charger kwenye box

Halafu ili kupata original charger za flagship za Samsung unapaswa uagize wapi, maana naona AliExpress zina bei rahisi kuliko bei wanaotaja phone reviewers, maybe ni fake au?
IMG_20230727_134006.jpg
 
Source: Twitter

1. Notch kubwa kwenye iPhone
View attachment 2697810
Flagship za Apple kama iPhone X series, 11 series, 12 series na 13 series zimekuwa zikija na notch kubwa kwa juu kwenye display ambayo imekuwa ikizuia kuona sehemu kubwa wakati wa kuangalia video. Hata hivyo kampuni imekuwa ikifanya hivyo kuanzia mwaka 2017 hadi 2022. Ila at least kwa sasa iPhone 14 Pro Max imekuja kupunguza hiyo notch ambayo ilikuwa kubwa kwenye iPhone 13 series na wenzake

2. Baadhi ya midrange za Samsung kuja na chipset ambazo zipo behind competition
View attachment 2697811
Kwenye picha ni Samsung Galaxy A54, moja ya midrange bora zaidi kwa sasa. Simu hii inakuja na chipset ya Samsung Exynos 1380 ambayo ni weak kuliko wapinzani katika bei hiyo. Exynos 1380 ina matatizo ya overheating pia wakati wa kucheza heavy games. Wapinzani kama Google Pixel 7 na Xiaomi Poco F5 wanakuja na chipset zenye nguvu kushinda ya Samsung Galaxy A54
Kwa mfano Google Pixel 7 inakuja na Google Tensor G2 na Poco F5 inakuja na Qualcomm Snapdragon 7+ Gen 2 ambazo ni strong kuliko Samsung Exynos 1380 ya kwenye Galaxy A54

3. Xiaomi, Oppo, Vivo na One plus kuendelea kulimit selfie camera kwenye flagship zao kurekodi maxum 1080p video tu
View attachment 2697813
View attachment 2697812

Picha ya kwanza ni Xiaomi 13 Ultra(juu) na ya pili ni Oppo Find X6 Pro. Hizi ni miongoni mwa simu zenye kamera bora zaidi mwaka huu lakini cha ajabu ni kwamba kamera zao za mbele bado haziwezi kurekodi video za 4K@30fps, matokeo yake zinaishia 1080p tu.
Hata Samsung Galaxy A54 inarekodi 4K video kwenye kamera ya mbele. Jambo la kushangaza zaidi ni kwamba hata midrange kutoka kwa Xiaomi wenyewe (Xiaomi Civi 3) inaweza kurekodi video za 4K kwenye kamera ya mbele ila flagship yao 13 Ultra haina uwezo huo.
Jambo jema ni kwamba kwa sasa Oppo wameshatoa software update ambayo imeongeza 4K video recording kwenye Oppo Find X6 Pro na pia Xiaomi 14 Pro inatarajiwa kuja na 4K selfie camera mwishoni mwa mwaka huu

4. Xiaomi kuchelewesha security updates kwenye baadhi ya models zake
View attachment 2697814
Kwenye picha ni moja ya models za Poco ambayo hadi sasa imeishia MIUI 14.0.2 update tu wakati simu kama Xiaomi Civi 1S imeshapata MIUI 14.0.9
Tabia hii inafanya baadhi ya watumiaji wa Xiaomi kuchelewa kuhamia kwenye new security update na hivyo kuleta kero. MIUI 14 imekuwa available tangu December mwaka jana lakini cha ajabu simu kama Redmi 9 zimekuja kupata MIUI 14 update kwenye hii miezi ya karibuni, na hii ni kwa sababu MIUI 14 Global ilichelewa kuwa released.
Wale wa Chinese version wanapata updates za haraka.
Jambo jema ni kwamba kuna feature kwenye simu za Xiaomi inayokuwezesha kupata updates za haraka sambamba na Chinese version

5. One UI kuwa nzito kwenye simu za low end
View attachment 2697815
Kwenye picha ni Samsung Galaxy A13, moja ya simu zenye UI nzito zaidi kwa sasa.
Samsung anajitahidi sana linapokuja suala la software quality kwa sababu software zao ni nzuri na zina features nyingi ambazo ni useful kwa matumizi ya kila siku na pia UI ikiwa na matatizo basi wanafix haraka kwa kupitia software update. Lakini kutokana na hii UI kuja na mambo mengi imefanya iwe UI nzito sana kuliko UI nyingine za Android.
Samsung pia amejitahidi kutumia One UI Core kwenye baadhi ya simu zake za low end ambayo imepunguzwa features nyingi ili walau iwe nyepesi.
Lakini bado simu kama Samsung Galaxy A13 zinashindwa kuhimili uzito wa One UI na kufanya iwe very sluggish. Features za muhimu za One UI kama multitasking hazifanyiki effectively kwenye low end kutokana na uzito wa UI na RAM ndogo.
One UI inafanya vizuri sana kwenye midrange na flagship zao. Aidha One UI Core inafaa zaidi kwenye low end

6. Midrange phones kutokuja na stereo speakers
View attachment 2697816
Kwenye picha ni Vivo V27, midrange nzuri kutoka kwa Vivo. Lakini jinsi kampuni hii ilivyo haina aibu wameamua kuweka speaker moja tu, matokeo yake imetoa unimpressive results kwenye gsmarena audio test.
Hata Redmi 10 inakuja na stereo speakers katika bei ya 370,000 tu ila hii simu kutoka kwa Vivo ambayo inakaribia milioni 1 hivi bado inatumia mono speaker.
Kwa sasahivi ni aibu kwa midrange kuja na mono speaker. Hata Samsung anayefahamika kwa bei za juu bado anaweka stereo speakers kwenye midrange zake, sijui Vivo V27 inakwama wapi

7. Simu kutokuja na chaja kwenye box kwa kisingizio cha kutunza mazingira
View attachment 2697817
Sony Xperia 1 V inakuja na simu tu ndani ya box. Hakuna kitu chochote kile zaidi ya simu. Labda kama utahesabia na pin ya kutolea line.
Samsung, Apple na Google nao hawaweki chaja kwenye box, wanataka utafute mwenyewe na bei ya chaja pekee inafikia hadi laki 1. Kisingizio chao kikubwa ni kwamba wanatuza mazingira
Flagship za China zinakuja na accessories za muhimu kama chaja kwenye box mfano Xiaomi 13 Ultra na Vivo X90 Pro Plus
Kitu kilichonishangaza zaidi ni kwamba hadi low end sasahivi zinaanza kuja bila chaja. Hapa ninailenga Xiaomi Redmi 12 moja kwa moja. Inasikitisha sana kuona hadi simu cheap kama Redmi 12 inakuja bila charger

8. Makampuni ku rebrand simu na kutumia SoC zilizopitwa na muda
View attachment 2697818
Kwenye picha ni Redmi 12. Nadhani kama unaijua Redmi 10 basi utanielewa. Simu hizi ni simply rebranded Redmi 10 tena inakuja na downgrade kama mono speaker na poor night photography. Matokeo yake ni kwamba bado inaendelea kutumia chipset ile ile ya MediaTek Helio G88 wakati kuna chipset nyingi tu nzuri kwa sasa.
Plus bei yake inakaribiana na Redmi Note 12 kwenye sehemu nyingi kwa hiyo sioni sababu ya kununua Redmi 12 wakati Redmi Note 12 5G tayari ipo tena ina SoC nzuri ya Snapdragon 4 Gen 1

9. Kupuuzia matatizo yanayotokea kwenye specific models za simu na ku pretend ni matatizo ya kawaida tu
View attachment 2697819
Kwenye picha ni Samsung mojawapo ambayo imekutwa na tatizo la green lines kwenye OLED display. Tatizo hili limekuwa common kwenye baadhi ya models kama Samsung Galaxy Note 9, Samsung Galaxy S20+ na baadhi ya Vivo na One Plus lakini inaonesha watu hata hawajali, wanapretend kama ni normal issue kwa OLED display ku form green lines

10. Flagship za Samsung, Apple, Xiaomi, Oppo, Vivo, One Plus na Google kutokuja na 3.5mm jack
View attachment 2697821
Kwenye picha ni Sony Xperia 1 V. Ndio flagship ya maana inayokuja na 3.5mm jack kwa sasa. Hawa akina Samsung, Apple, Xiaomi na wenzake wameamua kuondoa kabisa 3.5mm jack.
Wanataka utumie wireless earbuds ambazo zinauzwa kwa bei ghali kuliko wired earphones, plus unapaswa kuzichaji kila zinapoisha chaji.

11. Samsung kutumia chipset za Exynos kwenye flagship zake za EU variant
View attachment 2697822
Samsung Galaxy S22 Ultra inakuja na overclocked Snapdragon 8 Gen 1 lakini EU variant zinakuja na Exynos 2200 ambayo haiwezi kuwa nzuri kama overclocked Snapdragon 8 Gen 1 hata siku moja.
Jambo jema ni kwamba sasahivi wameamua kutumia Qualcomm Snapdragon 8 Gen 2 kwenye Samsung Galaxy S23 Ultra zote.

12. Flagship kuja na 128GB base storage
View attachment 2697823
Xiaomi 13 Pro, Samsung Galaxy S23 Ultra na iPhone 14 Pro Max zote hizi zinaanzia storage ya 128GB licha ya kuwa ni simu expensive.
Ingekuwa jambo la busara kama flagship zingeanza kuja na 256GB kama base storage mfano Xiaomi 13 Ultra.

13. Xiaomi imechelewa kuanza USB Type C 3.x, iPhone hadi leo hawajaanza hata kutumia
View attachment 2697824
Mwaka huu kwa mara ya kwanza ndio tunaona Xiaomi anaanza kutumia USB Type C 3.2 kwenye simu zake za Xiaomi 13 Ultra na tablets zake za Xiaomi Pad 6 na Xiaomi Pad 6 Pro. Pia Xiaomi Pad 6 Max iko mbioni kuja. USB Type C 3.x ni muhimu kwa sababu zinawezesha features za muhimu kama video out na faster files transfer.
USB Type C 3.x imewezesha flagship za Samsung kuja na feature ya Samsung DeX, kwa jina lingine inaitwa "Desktop Mode" ambayo imeimprove connection kati ya simu na kompyuta na ni useful kwa matumizi ya ofisini pia
Flagship za Motorola nazo zinakuja na feature kama hii ya Samsung DeX, kwenye Motorola inaitwa "Ready for" ila ndio feature ileile
iPhone hadi leo anatumia USB 2.0 na hatuoni dalili za kuhamia USB 3.2

14. Samsung, Apple na Google hawajahamia kwenye Super fast charging technology hadi leo
View attachment 2697826
Tumeona simu za China zenye uwezo wa kuchaji kutoka asilimia 0 hadi 100 chini ya dakika 30.
Mfano
*Xiaomi 13 Pro inatumia dakika 19 tu kwa kutumia chaja yake ya 120W
*Xiaomi Redmi Note 12 Discovery Edition inachaji kutoka asilimia 0 hadi 100 kwa dakika 9 tu kwa chaja yake ya 210W

Samsung Galaxy S23 Ultra inatumia approximately saa nzima kuchaji kwa chaja yake ya 25W
iPhone 14 Pro Max inatumia charger ya 27W na Google Pixel 7 Pro inatumia 23 W tu (kama nakumbuka vizuri)

Habari njema ni kwamba kuna rumours kwamba Samsung Galaxy S24 Ultra itakuja na 65W fast charger finally. Itakuwa ni improvement kubwa sana kwa simu za Samsung

Huko juu nilisema Source ni Twitter. Kuna mtu ametaka kujua exact source INGIA HAPA CHINI
Hii ndio source

Nitaendelea kutaja mambo mengine pia (kuanzia namba 15 na kuendelea)
Hapo tatizo linalonihusu ni namba 10 la 3.5mm audio jack tu, mengine yote hayanihusu kwenye simu yangu.
 
Hao wachina fast charger kali wanaotoa ni wachache tu, hizi lowend labda ila hizo fast charging nzuri unanunua separate na bei ndefu hadi laki mpaka laki na nusu.

Nimetest s20 na 15W ya Samsung pamoja na 27W ya Xiaomi zote zimedunda hakuna inayopeleka zaidi ya 10W,

Pia nimeangalia A24 inasuport Pd+pps charger, ina maana hata Quickcharge kwako haikufai (tech ya Qualcomm).

Tafuta Samsung 25W kama utapata, alternative tafuta pd charger yoyote, na Max kujaza simu yako ni kama saa 1 na nusu, sema kutunza battery lako set ijae kwenye asilimia 85 hivi, utapunguza muda wa kuchaji na pia utatunza betri.
Nashukuru kiongozi, mtandaoni naona pd charger za 20w kwe bei ya 20k zitafaa kweli? Au ndo yaleyale nilinunua fast charge ya 15k na simu usiku kucha haijai iko slow mnoo
 
Ila naona Wachina wanajitahidi ku include charger kwenye box hata kwenye simu zao premium, charger za 120W, 100W, 90W, 165W na 210W unazikuta kwenye box kabisa

Ile Redmi Note 12 Discovery Edition nimeona inakuja na 210W fast charger (9 min charging time). Motorola, Oppo, Vivo, Realme, One Plus na Xiaomi naona wanaweka sana charger kwenye box

Halafu ili kupata original charger za flagship za Samsung unapaswa uagize wapi, maana naona AliExpress zina bei rahisi kuliko bei wanaotaja phone reviewers, maybe ni fake au?
View attachment 2700487
Hio charger feki, toka lini charger ya 45W ikawa travel adapter.
 
Hio charger feki, toka lini charger ya 45W ikawa travel adapter.
Duh... Kwani kwenye kuchagua charger unapaswa kuangalia nini ili kujua ni original
Mfano umenunua Sony Xperia 1 V au Samsung Galaxy S23 Ultra then charger unatafuta mwenyewe

Hapa sielewi wakati wa kutafuta charger ni kitu gani kitakuongoza ili kupata perfect charger kwa simu yako
 
Nashukuru kiongozi, mtandaoni naona pd charger za 20w kwe bei ya 20k zitafaa kweli? Au ndo yaleyale nilinunua fast charge ya 15k na simu usiku kucha haijai iko slow mnoo
20W kwa hio Samsung probably itachaji 10W ama 15W sababu ili utumie 20W effectively inabidi iwe 5V 4A ambazo mara nyingi simu za BBK ndio zinakua hivyo.

Samsung fast charging yao ni 5V x 3A (15W) na 9Vx2.77A (25W)

To be sure mkuu tafuta tu 25W ya Samung, otherwise soma kwenye charger kama hivyo nilivyoandika vipo.

Pia kuna hiki kitu kinaitwa PD-PPS (power delivery programable power supply) hizi ni charger ambazo zina akili na zinawasiliana na simu kupeleka volt na amps zozote zile, kifupi haziwi fixed, ukipata charger yenye label hio pia itakuwa fresh kwa simu yako
 
Duh... Kwani kwenye kuchagua charger unapaswa kuangalia nini ili kujua ni original
Mfano umenunua Sony Xperia 1 V au Samsung Galaxy S23 Ultra then charger unatafuta mwenyewe

Hapa sielewi wakati wa kutafuta charger ni kitu gani kitakuongoza ili kupata perfect charger kwa simu yako
Njia ya uhakika mkuu ni uwe na usb meter ya kupima amps na voltage, zipo aliexpress 25,000-50,000.

Alternative utumie software kama Ampere ama zifananiazo hizi ni apps zipo playstore, sema naona Ampere kama haisomi vizuri latest charger ila still itasaidia kujua charger si kimeo kabisa. Charger kimeo inachaji simu amp moja kushuka.

Njia hizo mbili zinakusaidia ukienda dukani physically, kama unanunua online inabidi ununue Official kwenye Duka la kampuni husika ama utumie maduka makubwa ya Online ambayo yanauza yenyewe.
 
Back
Top Bottom