Mambo mabaya kuwahi kunipata katika mahusiano

Mambo mabaya kuwahi kunipata katika mahusiano

julius mahinya

JF-Expert Member
Joined
May 11, 2013
Posts
1,152
Reaction score
384
Katika mahusiano hasa ya gf na bf! kuna mambo mabaya huwapata watu mengine ya aibu mengine ya kutisha ila ndio tena hivyo siri hubaki kwa wahusika! Na mahusiano huwa ni kucheza bahati nasibu, waweza ingia chaka au ukalamba joka wakati mwafaka!
Sasa ni bora kuelimishana hapa ili wanaoanza mahusiano kuchukua tahadhari! mwaka 2009 mwezi wa sita nilingia na binti mmoja katika mahusiano ile kimjini mjini! yeye alikuwa anaishi Sinza na mimi mitaa fulani hivi hapa Dar! aliniambia anaishi na mama yake mdogo, na akasisitiza kuwa alimshirikisha wakati namtongoza na yeye ni mchango katika kukubaliwa kwangu na maneno mengine ya kulidhisha nafsi yangu!
Siku moja kaja kwangu nilimtaka alale, akaanza, oh sikuaga nikamwambia nani kwako muhimu kujua ulipo, akajibu mama mdogo! ok mpigie simu mwambie uko kwangu na unalala! kama saa mbili hivi usiku basi akalala na akadai kamtumia sms amekubali!
Alikaa kwangu siku nne, siku ya tano jioni tukakubaliana tunaenda kwa mama yake mdogo arejeshe simu ya mjomba wake kama alivyodai kuwa simu anayotumia ni ya mjomba wake na ni ya mambo ya kibiashara! ili sisi turudi twendelee na maisha yetu! Tuliamua kwenda nilichukua bajaji wakati huo toka nyumbani hadi Bamaga 2000/=, tukapanda dala dala tukashuka Sinza katangulia mimi nyuma kaingia kwenye duka la nguo namimi naingia mara anatoka nduki kulikua na dala dala kapanda huyo!
Ndani ya duka hilo la nguo nilibaki mimi, dada mmoja (nilikuwa namfahamu kama rafiki yake baada ya kutubamba siku moja kati ya siku hizo nne Rose garden) na kaka mmoja amepanda hewani amevimba ana hasira anagomba (nilikuwa simfahamu)
Kwa kuwa yule kaka alikuwa anagomba na ananiangalia mimi, huku maneno yote kama ananiambia mimi, unamchukua mke wangu, mnakaa na simu yangu mipango yangu ya biashara inakufa............. na matusi unayo yajua!
mara kanikaba, nikamuuliza unanifahamu, mimi huyo dada simjui! akasema nimekuona unashukanaye kwenye dala dala unaongozana naye kuja humu! nikajibu mimi nimeshuka nakuja kununua shati yeye simujui na kwenye dala dala tumeshuka wengi! jamaa linanibana nimekuona unaongea naye, nikajibu jamani mimi nimemuulizia duka la nguo ndio kasema lile pale nami naenda humo!
Akamgeukia huyo dada nayemfahamu kama shemeji yangu akamuuliza huyu unamfahamu akatikisa kichwa kwa uoga kuashilia hanifahamu! jamaa kaniachia oh samahani huyo demu nimemtoa kwenye dhiki leo ananidharau,hata kama sijamtolea mahari miaka miwili si ni sawa na kuoa, kaondoka na simu yangu .......unajua lawama kibao! nikaonyesha kusikitika duh! Jamaa anasisitiza nikimjua huyo bwana aliye naye namuua! nafika nyumbani namkuta yule demu duh! Eti oh mimi nilitaka nimuachie simu yake kwenye duka la rafiki yangu pale ili akifika aikute pale! nilitaka kupasuka, si angeniambia ukweli? nilimtimua kama simjui!
Kila nikikumbuka demu nisiyemfahamu hapa mjini duh noma!!!!!!!!!!!
 
dahhhh pole mkuu ulinusurikaje pale ushukuru ulipata maneno ya kujitetea ghafla na uakeleweka na yule shemejio alikuwa na roho ya huruma,vinginevyo labda sa hivi ungekuwa unatupa stori nyingine kaaabisaaaaaaaaaa.
 
una bahati wewe..siku hizi kiboga ndugu yangu watu si wema tena

Bora ufanyiwe ufilauni kama ulikuwa unafahamu, lakini kimjini mjini ndugu yangu mtu hujui kwao ila yeye kwako anapafahamu bila shaka! nilisha jifunza sana japo stasahau! sijui yule dada angesema ananifahamu hiyo ligi inge chezekaje! kiboga labda ninge uwawa kwanza wale maiti!
 
Ila mkuu unawezaje kumwamin mtu ukampeleka kwako day one na kuanza kuishi nae? Ulishindwa kuanza na voda faster?

Haikuwa siku moja process za kutongoza ni za kawaida tumekutana naye siku ya kwanza Mwenge kwenye dala dala mimi na rafiki yangu tukabadilishana namba kimjini mjini, siku anakuja kwangu alinitafuta yeye! ndio maana alisema mama yake alihusika yeye kunikubalia!
 
Alikuja kwako na plan ya kutolala,ukamconvince badala ya kutupia usiku mmoja akavuta 4 na we hata hujajiuliza swali lolote hapo...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom