Katika mahusiano hasa ya gf na bf! kuna mambo mabaya huwapata watu mengine ya aibu mengine ya kutisha ila ndio tena hivyo siri hubaki kwa wahusika! Na mahusiano huwa ni kucheza bahati nasibu, waweza ingia chaka au ukalamba joka wakati mwafaka!
Sasa ni bora kuelimishana hapa ili wanaoanza mahusiano kuchukua tahadhari! mwaka 2009 mwezi wa sita nilingia na binti mmoja katika mahusiano ile kimjini mjini! yeye alikuwa anaishi Sinza na mimi mitaa fulani hivi hapa Dar! aliniambia anaishi na mama yake mdogo, na akasisitiza kuwa alimshirikisha wakati namtongoza na yeye ni mchango katika kukubaliwa kwangu na maneno mengine ya kulidhisha nafsi yangu!
Siku moja kaja kwangu nilimtaka alale, akaanza, oh sikuaga nikamwambia nani kwako muhimu kujua ulipo, akajibu mama mdogo! ok mpigie simu mwambie uko kwangu na unalala! kama saa mbili hivi usiku basi akalala na akadai kamtumia sms amekubali!
Alikaa kwangu siku nne, siku ya tano jioni tukakubaliana tunaenda kwa mama yake mdogo arejeshe simu ya mjomba wake kama alivyodai kuwa simu anayotumia ni ya mjomba wake na ni ya mambo ya kibiashara! ili sisi turudi twendelee na maisha yetu! Tuliamua kwenda nilichukua bajaji wakati huo toka nyumbani hadi Bamaga 2000/=, tukapanda dala dala tukashuka Sinza katangulia mimi nyuma kaingia kwenye duka la nguo namimi naingia mara anatoka nduki kulikua na dala dala kapanda huyo!
Ndani ya duka hilo la nguo nilibaki mimi, dada mmoja (nilikuwa namfahamu kama rafiki yake baada ya kutubamba siku moja kati ya siku hizo nne Rose garden) na kaka mmoja amepanda hewani amevimba ana hasira anagomba (nilikuwa simfahamu)
Kwa kuwa yule kaka alikuwa anagomba na ananiangalia mimi, huku maneno yote kama ananiambia mimi, unamchukua mke wangu, mnakaa na simu yangu mipango yangu ya biashara inakufa............. na matusi unayo yajua!
mara kanikaba, nikamuuliza unanifahamu, mimi huyo dada simjui! akasema nimekuona unashukanaye kwenye dala dala unaongozana naye kuja humu! nikajibu mimi nimeshuka nakuja kununua shati yeye simujui na kwenye dala dala tumeshuka wengi! jamaa linanibana nimekuona unaongea naye, nikajibu jamani mimi nimemuulizia duka la nguo ndio kasema lile pale nami naenda humo!
Akamgeukia huyo dada nayemfahamu kama shemeji yangu akamuuliza huyu unamfahamu akatikisa kichwa kwa uoga kuashilia hanifahamu! jamaa kaniachia oh samahani huyo demu nimemtoa kwenye dhiki leo ananidharau,hata kama sijamtolea mahari miaka miwili si ni sawa na kuoa, kaondoka na simu yangu .......unajua lawama kibao! nikaonyesha kusikitika duh! Jamaa anasisitiza nikimjua huyo bwana aliye naye namuua! nafika nyumbani namkuta yule demu duh! Eti oh mimi nilitaka nimuachie simu yake kwenye duka la rafiki yangu pale ili akifika aikute pale! nilitaka kupasuka, si angeniambia ukweli? nilimtimua kama simjui!
Kila nikikumbuka demu nisiyemfahamu hapa mjini duh noma!!!!!!!!!!!