Hashpower7113
JF-Expert Member
- Sep 26, 2011
- 1,353
- 2,137
Wengi wanamfahamu kutokana na umahiri wake mkubwa katika medani ya muziki, utambulisho
wake mkubwa ukiwa ni sauti yake nzito na ya kipekee. Yafuatayo ni mambo kumi kuhusu msanii huyu.
1. Alizaliwa Septemba 22, 1952 katika eneo la mashambani la Highfield, Salisbury, Zimbabwe na kukulia huko. Anafahamika kwa jina la utani la Tuku.
2. Mbali na muziki, Mutukudzi pia ni mfanyabiashara, mwanaharakati wa haki za binadamu na balozi wa UNICEF Kusini mwa Bara la Afrika.
3. Alianza kutambulika zaidi kimuziki baada ya kuingia katika Kundi la Wagon Wheels mwaka 1977, akiwa na wenzake kadhaa, akiwemo Thomas Mapfumo.
4. Anaimba muziki wake katika lugha tatu, Kishona, Kindebele na Kiingereza na huchanganya ala za muziki wa kiasili kwenye nyimbo zake, jambo lililompa umaarufu mkubwa dunia nzima.
5. Tofauti na wenzake katika Kundi la Wagon Wheels waliokuwa wakimuimba vibaya Rais Robert Mugabe, Mutukudzi amekuwa akimsifia sana na kusababisha anufaike kwa misaada mbalimbali kutoka serikalini.
6. Mutukudzi ni baba wa watoto watano na mpaka sasa ana wajukuu wawili. Watoto wawili kati ya hao, ni wanamuziki.
7. Mwaka 2010, mwanaye kipenzi, Sam Mutukudzi ambaye naye alikuwa mwanamuziki, alifariki dunia kutokana na ajali mbaya ya gari.
8. Mutukudzi amekuwa akidaiwa mara kwa mara kwamba ni muathirika wa ugonjwa wa Ukimwi ingawa mwenyewe amekuwa akikanusha vikali madai hayo.
9. Kati ya wasanii wenzake waliokuwa wakiunda kundi la Wagon Wheels, ni yeye pekee aliyebakia hai hadi leo. Wenzake wote wamekufa kwa Ukimwi.
10. Hivi karibuni, mashabiki wake nchini humo walipatwa na mshangao mkubwa baada ya kitabu kiitwacho Tuku Backstage kuvuja kikiwa na kashfa nyingi za ngono zinazomhusu gwiji huyo, mwandishi akiwa ni Shepherd Mutamba.