Mambo kumi kuhusu kuzama kwa meli ya Titanic na filamu yake

Zurie

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
2,002
5,535
titanic-P.jpeg

1.Wanamuziki waliokuwa wakipiga muziki kwenye meli ya titanic, waliendelea kupiga muziki kwa saa moja Toka meli ilipoanza kuzama.

2.Gharama za kutengeneza Movie ya Titanic Ni Kubwa kuliko gharama za Kutengeneza Meli halisi ya Titanic iliyokuwa na uwezo wa kubeba watu zaidi ya elfu tatu! Movie ya Titanic ilitengenezwa kwa gharama ya dola Milioni miambili ($ 200Mil) wakati Meli ya Titanic ilikuwa na thamani ya $170 Mil.

3. Baada ya Kuona Meli inazama Maeneo yenye baridi kali, Mpishi Mkuu wa meli hiyo, alikunywa pombe Kupita Kiasi ili aweze Kuhimili baridi Kali! Aliweza Kukaa masaa Mawili kwenye Barafu na Hatimae Kuokolewa.

4.Sekunde 30 zingetosha Kuokoa Meli ya Titanic Kama si Kuchelewa Kutoa Taarifa za Kuwepo kwa Mwamba wa Barafu. Watoa taarifa walichelewa kwa Sekunde 30 tu!

5.Baada ya Kugongana na Mwamba, Ilipita masaa mawili mpaka Meli yote ya Titanic Kuzama.

6.Hakuna Meli Yoyote nyingine Iliyowahi Kuzama kwa kugonga Barafu!

7.Mjapani Aliyepona kwa kuokolewa Kwenye Ajali ya Titanic, aliitwa Mpumbavu nchini kwake eti tu, Kwanini hakufa kishujaa pamoja na wengine?

8. Vyumba vya Hadhi ya juu zaidi kwenye Meli ya Titanic vililipiwa Dola 200.

9. Zaidi ya Maharusi 20 walikuwa wakisherekea “HoneyMoon” kwenye meli hiyo iliyozama.

10. Msanii Madonna ni moja kati ya watu waliotakiwa kuigiza uhusika wa “Rose” lakini baadae Kate Winslet aliigiza uhusika huo
 
gharama za utengenezaji wa filam na meli si sawa mkuu wenzi hizo dola mil 200 na enzi za utengenezaji wa filamu haziendani
 
gharama za utengenezaji wa filam na meli si sawa mkuu wenzi hizo dola mil 200 na enzi za utengenezaji wa filamu haziendani
Hiyo hela imebadilishwa kulingana na wakati....."At $200 million, the movie cost more than the Titanic itself. The cost to construct the ship in 1910-1912 was £1.5 million, equivalent to $7.5 million at the time and about $120 to $150 million in 1997 dollars. "
 
gharama za utengenezaji wa filam na meli si sawa mkuu wenzi hizo dola mil 200 na enzi za utengenezaji wa filamu haziendani
Hapo ndipo linapoingia somo la usimamizi wa fedha (Financial Management). Fedha ya miaka kadhaa nyuma au ijayo inafanyiwa mahesabu na kupata thamani yake halisi kwa wakati uliopo au wakati uliokusudiwa (Net Present or Future Value).
 
oky
 
Lakini dola milioni 200 ni za 1997....thamani yake ya sasa itakuwa zaidi,...maybe hata twice that amount
 
Mapenzi ya kweli sana yale,hasa Rose alivyoenda kumuokoa jamaa deka za chini alikokuwa amefungwa pingu!
 
4.Sekunde 30 zingetosha Kuokoa Meli ya Titanic Kama si Kuchelewa Kutoa Taarifa za Kuwepo kwa Mwamba wa Barafu. Watoa taarifa walichelewa kwa Sekunde 30 tu!

Hii ndo sjaiamini ebu elezea kidogo mkuu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Copy and paste kwa wapenda historia:

Titanic—“Meli Maarufu Zaidi katika Historia”

APRILI 10, 1912: Meli ya Titanic inaondoka Southampton, Uingereza, ikielekea New York, Marekani.

APRILI 11: Baada ya kuwachukua abiria huko Cherbourg, Ufaransa, na huko Queenstown (ambayo sasa inaitwa Cobh), Ireland, Titanic inaelekea kwenye Bahari ya Atlantiki.

APRILI 14: Saa 5:40 hivi usiku, Titanic inagonga mwamba wa barafu.

APRILI 15: Saa 8:20 usiku, Titanic inazama, watu 1,500 hivi wanakufa.

MELI ya Titanic ilikuwa ya aina gani? Ni nini kilichoifanya izame? Tunapata majibu tunapotembelea Jumba la Makumbusho la Ulster Folk and Transport, karibu na Belfast huko Ireland Kaskazini.

Titanic—Kwa Nini Ilikuwa Meli ya Pekee?

Kulingana na Michael McCaughan, aliyekuwa msimamizi wa Jumba la Makumbusho la Ulster Folk and Transport, Titanic ilikuwa ndiyo “meli maarufu zaidi katika historia.” Lakini meli ya Titanic haikuwa ya kipekee. Kati ya meli tatu kubwa zilizojengwa katika viwanda vya kutengenezea meli vya Harland and Wolff huko Belfast, Titanic ilikuwa ya pili kwa ukubwa.* Titanic ilikuwa moja ya meli kubwa zaidi za wakati huo, ikiwa na urefu wa mita 269 na upana wa mita 28.

Kampuni ya meli ya White Star iliagiza meli hizo kubwa zitengenezwe ili iweze kutawala biashara ya usafiri kwenye Bahari ya Atlantiki Kaskazini. Kampuni hiyo ya White Star Line haingeweza kuishinda kampuni ya Cunard Line katika usafiri wa kasi. Kwa hiyo, ilikazia fikira hasa kujenga meli kubwa na zenye starehe ili kuwavutia watu maarufu na matajiri.

Lakini meli ya Titanic ilikuwa na uwezo wa kutimiza jambo lingine vilevile. “Wahamiaji 900,000 hivi waliingia Marekani kila mwaka kati ya 1900 na 1914,” anasema William Blair, msimamizi wa Majumba ya Makumbusho ya Ireland Kaskazini. Kampuni za kuwasafirisha watu kwenye Bahari ya Atlantiki zilipata pesa nyingi zaidi kwa kuwasafirisha wahamiaji hao kutoka Ulaya hadi Marekani, na Titanic ilitumiwa kwa kusudi hilo.

Msiba

Kapteni wa Titanic, E. J. Smith, alijua hatari zilizotokezwa na barafu kwenye Bahari ya Atlantiki Kaskazini. Alikuwa amesafiri kupitia njia hiyo mara nyingi akitumia meli ya Olympic. Meli nyingine zilitoa maonyo mara kadhaa kwamba kuna miamba ya barafu, lakini huenda kapteni alipuuza au hakupokea maonyo hayo.

Ghafula, wenye kushika doria kwenye Titanic walitoa onyo kwamba kuna mwamba wa barafu mbele—lakini ilikuwa kuchelewa mno! Ofisa aliyekuwa akisimamia alifaulu kuepuka kuugonga mwamba huo moja kwa moja lakini hangeweza kuzuia ubavu mmoja wa Titanic usikwaruze mwamba huo. Hilo liliharibu ubavu wa meli hiyo na maji yakaanza kujaa ndani ya vyumba kadhaa vya mbele. Punde si punde, Kapteni Smith akaelezwa kuwa meli hiyo ilikuwa hatarini. Akatuma ujumbe wa dharura na akaagiza kwamba mashua za kuokoa uhai zishushwe.

Meli ya Titanic ilikuwa na mashua 16 za kuokoa uhai na mashua nyingine nne za kujazwa upepo. Mashua hizo zikiwa zimejaa kabisa zingeweza kutoshea watu 1,170 hivi. Lakini meli yote ilikuwa na watu 2,200! Zaidi ya hayo, mashua nyingi ziliondoka kabla ya kujaa kabisa. Na nyingi hazikuwatafuta waokokaji waliokuwa wameruka ndani ya maji. Mwishowe, ni watu 705 tu waliookolewa!

Baada ya Msiba

Baada ya msiba wa Titanic, wenye mamlaka wanaosimamia usafiri wa baharini waliweka sheria zilizoboresha usalama baharini. Sheria moja ilihakikisha kwamba kuna mashua za kutosha za kuokoa uhai ndani ya meli.

Kwa miaka mingi watu waliamini kwamba Titanic ilizama haraka sana kwa sababu ilikuwa na shimo kubwa sana kwenye upande ambao uligonga mwamba. Lakini katika mwaka wa 1985, baada ya Titanic kupatikana chini ya bahari, wachunguzi walifikia mkataa tofauti—kwamba maji yenye barafu yaliharibu vyuma vya meli hiyo na kufanya vyuma hivyo vivunjike kwa urahisi. Katika muda usiozidi saa tatu baada ya meli hiyo kugonga mwamba, ilivunjika na kuwa vipande viwili kisha ikazama, na kwa sababu hiyo, huo ukawa mojawapo ya misiba mikubwa zaidi katika usafiri wa baharini.*
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom