Mme Mwenza
JF-Expert Member
- Feb 6, 2025
- 2,697
- 3,858
Umewahi kujiuliza kwanini kuna watu kila wakigusa jambo linafanikiwa, na kuna wengine kila wakijaribu wanagonga ukuta? Siri kubwa haipo kwenye bahati, bali ipo kwenye sumaku iliyojificha ndani ya akili na nafsi yako.
*Ukweli ni huu: Huvuti unachokitaka, unavuta kile ulicho nacho ndani.
1. Acha Kujiashiria Mabaya
Kama ndani yako kumejaa hofu, mashaka, na picha za kushindwa, usishangae kuona maisha yako yakizungukwa na watu waongo, fursa zinazokufa, na milango inayofungwa. Unapojiambia "Mimi sina bahati" au "Hili jambo haliwezekani kwangu," unatoa agizo kwa ulimwengu kukuletea mazingira yatakayothibitisha unachokiwaza.
Badili muonekano wako wa ndani, anza kujiona mshindi kabla hata filimbi ya ushindi haijalia.
2. Acha Kujiona Maskini
Umaskini si ukosefu wa fedha kwenye pochi,, umaskini ni hali ya akili (Mindset). Ukijiona maskini, hata ukipewa mamilioni leo, yataondoka kesho kwa sababu ndani yako hakuna chombo cha kubeba utajiri huo.
Acha kusema Sina uwezo
Acha kusema Sisi ni watu wa hali ya chini
Acha kusema Maisha ni magumu sana
Anza kujiona tajiri wa mawazo, tajiri wa afya, na tajiri wa fursa Unapojiona una thamani, ulimwengu unaanza kukulipa kwa thamani hiyo hiyo unayojipa
* Maisha yako ya sasa ni matokeo ya vibration yako ya ndani. Kama unataka kuvuta baraka, lazima uwe na baraka ndani yako kwanza kupitia Shukrani.
Yule aliye na shukrani, ataongezewa,, lakini yule asiye na shukrani, hata kile kidogo alichonacho atanyang'anywa.
* Chukua Hatua Hizi Leo:
- Linda Lango la Akili: Usiruhusu mawazo ya hovyo yakae ndani yako zaidi ya sekunde 60. Yafukuze kama mwizi!
- Badili Lugha Yako: Acha kusema "Sijui kama nitatoboa," sema "Natafuta njia na nitaipata."
- Jione Tayari: Anza kujiandaa kwa ajili ya maisha unayoyatamani. Vaa vizuri, tabasamu, na fanya kazi kwa bidii kana kwamba tayari umeshafanikiwa.
Kumbuka: Ulimwengu hausikilizi maneno yako ya mdomoni, unasikiliza imani iliyopo moyoni mwako. Kama unajiona ni wa thamani, basi thamani itakufuata popote uendapo.
Wewe ni mshindi, na ndani yako kuna hazina ya ajabu. Iamshe leo! 💪