Mambo gani ya kuzingatia kijana anayetaka kuanza safari ya usanii bongo?

Singida ndio home

JF-Expert Member
Feb 23, 2012
3,192
3,353
Ni vijana wengi sana wanapenda kuwa wasanii, binafsi kwa huu mtaa wangu wenyevnyumba nane kuna wasanii wanne ila hawajafika popote na umri umeshaenda, labda pengine ni kwasababu hawakupata elimu ya mambo yapi ya kukazania na yapi ya kukwepa kwenye safari ya usanii.

Binafsi kitu cha kwanza kusisitiza ni msanii kwenda na muda maana muda hausimami, kuna msanii hapa mtaani alianza kuimba tangu 2005 na kwa sasa ana miaka 33 anaendelea kuimba na hafiki popote kwasababu anaimba zile hiphop ngumu na kila tukimwambia abadili style hakuelewi matokeo yake hajafika popote,

Kingine nashauri kwa sasa mtu ajiwekee mwonekano wa kisanii, hata awe underground kivipi lazima ajijue ye ni msanii tayari, kwahio inabidi asiwe rafu awe anavaa vizuri na kupendeza hata mtu akimwona anajua huyu msanii,

Kuepukana na unyinyaji hapa naomba mzoefu kidogo aliongelee.

Naombeni muendelee mambo mengine, mchango wenu ni muhimu sana.
 
itabdi uachie ngoma moja afu..umlipe muhuni aku papase makalio kwenye video.BASATA waki iona upite nao juu kwa juu navi online TV kama vyote...




Ukiwa star usini sahau ..uchawi wa keyboard u no need kwenda kwa mganga

Sent using Jamii Forums mobile app
 
namkumbuka Sana marehem #efrahim kibonde aliwahi kusema ni jinsi gani unaweza kuwa star na utayari mpka Leo maneno yake yanaishi kwangu R.i.p brother
 
Ukitaka kutoka kimuziki kuwa na pesa Fanya Kazi promote Kazi honga TVs and radios.....acha mboyoyo hapa za sijui hip hop ngumu imefanya nini.
Hugo Rayvan kabla ya kwenda wasafi alikua nobody tu hapo tptp...
Ukitaka kua star honga kipaji peleka kwenu huko...
 
Msanii anaishi maisha ya sanaa na anasa

Kwani Insta una followers wangapi?

Chopstick from Hong Kong
 
Utaskika mziki bila shobo hautoki, na hizo ngumu sana hazinogi.../

Fanya vitu flani utabamba, wasanii wenu wapo tu mtaani wamesanda.../

Wametoboa ulimi mpaka pua, mameneja wao wamewafundisha kujishaua na kujichubua.../

Msanii awe na rangi, usionekane sana utapoteza brand.../

Brand au brandina?, si wengine tunaonekana kama wavuta bangi kiana.../

Mziki biashara mtaji mi sina, utabebeshwa madawa uende ukadakwe china.../

Umesikiliza wimbo mpaka umeisha, sijakuomba ushauri eti Scars badilika.../

Msanii wako akipanda stage anakatika, sa tutafanyaje naye ndo nguvu kazi ya taifa?.../

Nala mzalendo
 
Kila mtu ana njia zake,
Binafsi napenda msanii ambaye anajimudu kwa vitu vingi, awe ana uwezo wa kuandika, kuproduce muziki na awe na uwezo wa kuchora idea kali za video.
1. Jifunze kuandika mashairi na mistari vizuri
2. Kama unaweza, nunua vifaa kwa studio na utengeneze home studio ambako utajifua kiuhalisia.
3. Ukifikia hatua ya kutaka muziki wako usikike, wekeza sana kwenye ubunifu katika video. Fanya video simple lakini zenye idea kali.
4. Promotion, dunia imefunguka sio kama zamani. Ukiweza kutumia vyema social networks utakuwa na mahala bora pa kuanzia.
Yatakayofuata huko ni wewe na kichwa yako.

Mimi nipo hapo kwenye namba mbili.
 
Jiandae kupakwa vasseline maana maproducer hatutaki ujinga........tunawapa umaarufu harafu baadaye mnareta kiburi........mnajiona kama mpo hollywood tayari
 
Back
Top Bottom