Mambo 6 ya kudumisha mapenzi katika ndoa

Rodwell mTZ

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
818
1,000
MAMBO 6 YA KUDUMISHA MAPENZI KATIKA NDOA

Habari za Jumapili wana JF,

Wengi watu tukiwa tumetulia majumbani mwetu siku ya leo Jumapili nimeona ni vyema ku'share' nanyi mambo machache kama 6 hivi yanayoweza kuimarisha mahusiano ya mapenzi katika ndoa naomba mchangie kama kuna mengine mengi si vibaya tuweze kuielimishana, kama vile mjuavyo ndoa ni darasa pana sana.

(1) Jitahidi ujue vitu gani ambavyo mwenza wako anavipenda zaidi, mfano wewe ni mume na mkeo anapenda sana movie za kiswahili wewe moyo wako haupo huko basi Jitahidi hata kuwajua wasanii maarufu wa movie za kiswahili ili angalau mara moja moja muweze kuangalia pamoja movie hizo naifike mahali uwe na uwezo wa kujadili kinachoendelea katika movie. Kwa mke vilevile mmeo anaweza kuwa anapenda kuangalia mechi za mipira basi waweza kujifunza kujua vitu muhimu katika soka kama vile offside, direct kick, Injury time n. k

(2) Usipende kuongelea habari za mpenzi wako wa zamani mbele ya mkeo(mmeo). kama usemi wa kiswahili unavyosema yaliyopita sindelwe tulonge yajayo ndoa ni kama mmea uliopandwa unahitaji matunzo nakulindwa dhidi yawadudu waharibifu na jua kali unavyosema yaliyopita sindelwe tulonge yajayo ndoa ni kama mmea uliopandwa unahitaji matunzo nakulindwa dhidi yawadudu waharibifu na jua kali.

(3) Tahadhali na maneno ya watu yanayoongelewa kuhusu mpenzi wako kuna mengine si ya kweli ni uzushi wa kuwatenganisha.

((4) Jitahidini kutembea pamoja. Katika zama hizi watu wako bize kuliko maelezo katika kutafuta vipato ili kukidhi mahitaji mbalimbali si vibaya kama utapata mda wewe na mwenzi wako mkatoka pamoja hata mara moja kwa wiki itasaidia, mnaweza kutembelea ndugu, au mkaenda sehemu tulivu mkapata kitu cha kuwaburudisha.

(5) Hii namba 5 itawahusu wanaume zaidi, msaidie mwenza wako kazi za ndani mara moja moja anapoelemewa hii itamjengea mkeo kujiamini kwamba ana mume anayeweza kumsaidia.

(6) Naomba unisamehe" sentensi hii yenye maneno mawili ina nguvu kulishinda bomu la nyumba, unapoona umemkosea mwenzi wako tumia sentensi hii" naomba unisamehe " badala ya kujenga ukuta wa kujitetea na kutoa visingizio kibao.

Nawakaribisha tena wadau wa wa JF
 

Smart911

JF-Expert Member
Jan 3, 2014
70,632
2,000
Mambo ya kuzingatia yamekuwa mengi sana... mpaka unashindwa jua nini cha kufuata...
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom