Mambo 6 Duniani yaliyotokea kwa namna ya kuacha Mdomo wazi

LOSEJMASAI

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
332
856
1. Ozil na Ferrari
Enzo Ferrari mwanzilishi wa ferrari ambaye Kisura anafanana na Mchezaji wa mpira Mesut Ozil alifariki Mwaka ambao Ozil alizaliwa.

5040f2c2-cc99-4587-b437-dbf8c28dc6f6.jpg


2. Lincoln na Kennedy.
Maraisi wawili wa Marekani waliowahi kupendwa sana Lincoln na Kennedy wote walikuwa na urefu sawa wa futi sita. Wote waliwahi kwenda vitani kabla ya kuwa Marais. Wote walikufa siku ya ijumaa. Wote kwa kupigwa risasi kichwani. wote wakiwa wamekaa pembeni ya wake zao.

854bd75f-829a-463f-95c9-4858ed986291.gif


3. Kutabiriwa kwa Titanic.
Miaka 14 kabla ya kutengenezwa titanic, mwandishi wa vitabu Morgan Robertson alitabiri Kuzama kwa Titanic. Kwenye kitabu chake cha Futility, or the Wreck of the Titan alitumia jina la titan kusimulia meli isiyoweza kuzama. Meli ya kwenye kitabu ilikuwa urefu sawa na meli ya ukweli ya Titanic. Meli ya kwenye kitabu cha Robertson ilizama kwa kugonga mwamba wa barafu kwenye Bahari ya Atlantic ya kaskazini, kitu ambacho kilitokea pia kwenye titanic ya ukweli.
013bd087-2f7c-4b85-86fb-6ddde6e48965.jpg


4. Mfalme Umberto I wa Italy
Mfalme Umberto I wa Italy alifahamiana na mumiliki wa mgahawa baada ya kugundua kuwa wote wamezaliwa siku moja, mji mmoja na wote wameoa wanawake wenye majina yanayofanana. Siku chache baadaye wote wakauliwa siku moja sehemu tofauti kwa kupigwa risasi.


442b575c-9d18-4adf-800a-9d6819e902bb.jpg


5. Napoleon na Hitler (129).
Adolf Hitler alizaliwa miaka 129 baada Napoleon Bonaparte. alitawala miaka 129 baada ya utawala wa Napoleon. aliivamia Urusi miaka 129 baada ya Napoleon kuivamia Urusi pia. Na aliondolewa madarakani miaka 129 baada ya Napoleon naye kuondolewa madarakani.

ca79d43d-c905-4542-ac0e-e5b2b104aee3.jpg


6. Gari la Archiduke Ferdinand.

Kuuliwa kwa Archduke Franz Ferdinand kulifungua rasmi vita ya kwanza ya dunia. Gari alilokuwa amepanda wakati anauliwa lilikuwa na plate number A11-11-18. Vita vya kwanza vikaisha rasimi November 11, 1918 - 11-11-18.
9f162de7-d2f3-4289-b287-f17fdfabd6f1.jpg



Three Updates


7. Ujenzi wa Bwawa la Hoover
Ujenzi wa bwawa hili liligharimu maisha ya watu wengi, lakini mtu wa kwanza kufa ni bwana J.G. Tierny, ambaye alifariki December 20, 1922. Mfanyakazi wa Mwisho kufa kwenye huu ujenzi alikuwa Mtoto wa Tierny alikufa siku sawa na siku aliyokufa baba ake miaka 13 baadaye, December 20, 1935.
5903df49-d792-4a1f-b4f7-be183d72a5c7.jpg



8. Video game Iliyotabiri semptember eleven (Twin tower iliyopigwa na Osama)
Video game ya Deus Ex ambayo ilikuwa officially released June 2000. Game hili lilitengenezwa kuakisi maisha ya New york city, lakini katika hatua za mwisho kabisa wakagundua kwamba wamesahau kuyaweka majengo pacha ya biashara (Twin Towers). Ili kukwepa gharama na muda wa kuanza kutengeneza upya ikabidi waandike tu mwanzo wa game kwamba yale majengo yamelipuliwa na magaidi.
c08e89b2-e0ef-4624-946e-a9b84b6492aa.jpg


9. Ndugu wawili wa Hamilton
Dereva wa baiskeli yenye injini (Moped) mji wa Hamilton, Bermuda alifariki mwaka 1974 kwa kugongwa na taxi. mwaka ulifuta 1975 eneo lile lile, mdogo wake naye aligongwa akiwa anaendesha baiskeli ya injini, gari iliyomgonga ni ile ile iliyomgonga kaka ake, na cha ajabu kabisa dereva yule yule, na pia alikuwa amebeba abiria yule yule aliyekuwa amemubeba siku anamugonga kaka mtu.
d73d7446-4194-4ae4-a8a5-716959e833e5.jpg
 
Namba 5 sijaelewa

Pattern ya kufanya mambo kati ya hao jamaa wawili inafanana, in other words, napolean alizaliwa miaka 129 kabla hitler hajazaliwa, and aliingia madarakani miaka 129 kabla hitler hajaingia madarakani, Napoleon aliivamia Urusi Miaka 129 kabla ya Hitler kuivamia pia Urusi. Wote hawa jamaa wawili walikuwa na vision ya Kuitawala Dunia.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom