Mambo 30 usiyoyajua kuhusu msitu wa Amazon

DR SANTOS

JF-Expert Member
Mar 11, 2019
10,519
21,437
Habari wana JF,

Nimependa kuandika machache ninayoyafaham juu ya msitu wa Amazon. Utaongeza chochote unachokifaham juu ya msitu huu.

1: Msitu wa Amazon ndio msitu mkubwa zaidi duniani unaopatikana huko America kusini.

2: Kama ulifikiri msitu huu unapatikana Brazil pekee jibu ni hapana msitu huu umegawanyika katika nchi tisa nchi hizo ni Blazil 60% peru 13% colombia 10% na mataifa mengine kama Venezuela, Ecuador, Bolvia, Guyana, Suriname na France Guiana.

3: Msitu huu una eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 5,500,000 (Milioni 5) yani kwa ukubwa huu nchi ya TANZANIA iingie mara 6 kwenye msitu huo.

4: Kwa mujibu wa wanasayansi wa mimea msitu wa Amazon una umri wa miaka zaidi ya million 55

5: Msitu wa Amazon unakadiriwa kuwa na miti billion 400 na aina mbalimbali za miti zaidi ya 160,000 pia kuna miti ya matunda tofauti tofauti elfu tatu katika msitu huo.

6: Mchanga wa jangwa la sahara hupeperushwa na upepo hupita juu ya bahari Atlantic hadi katika msitu wa amazon ambako hurutubisha katika msitu huo.

7: Katika msitu wa amazon kuna mto umekatisha mto huo unaitwa mto amazon huu ndio mtu mkubwa zaidi duniani na unaingiza maji baharini mara 5 ya mito mingine maajabu ya mto huu kuna muda haueleweki kuna kipindi unapeleka maji kinyume badala ya maji kwenda mashariki yana kuwa yana toka mashariki kwenda magharibi.

8: Asilimia 20% ya oxygen iliyopo dunia inatengenezwa katika msitu wa amazon acha hili pia zaidi ya asilimia 70% ya madawa ya kisasa yana tengenezwa kwa kutumia miti inayo patikana ndani ya msitu wa amazon. Ndio maana unaitwa mapafu ya dunia.

9: Katika msitu wa amazon kuna makabila zaidi ya 50 yana ishi hapo watu wameishi kwa maelfu ya miaka iliyo pita lakini watu hao wamekuja kuonekana miaka ya hivi karibuni.

10: Green anaconda
Hawa ndio nyoka wakubwa zaidi duniani kwa sasa ni aina ya nyoka wanao patikana msitu wa amazon pekee wana rangi ya kijani na madoa meusi.

11: Poison dork frog
Ni aina ya vyura wanaopatikana msitu wa amazon pekee wana sumu kali katika migongo yao mfano uchukue mwiba uchome ugongo wa chura hao kisha ujichome mwiba huo uvuki dakika kumi tunakua tusha kukosa

12: American jaguar
Huyu anapatikana msitu wa amazon pekee Ni mnyama jamii ya paka huyu kafanana na duma ila yeye ni mweusi mwili mzima kama kiwi anapendelea sana kujificha juu ya miti mirefu ana uwezo mkubwa kuogelea ni mnyama mwenye speed kali sana ukimtoa duma .

13: Harpy Eagle
Ni aina ya tai wanaopatikana msitu wa amazon hawa ni wakubwa zaidi hawa ni wapole wanaweza ishi na binadamu bila tatizo .

14: Black caiman
Ni aina ya mamba wenye rangi nyeusi Hawa ni baadhi tu pia inasemekana nyoka mkubwa zaidi kuishi duniani aina ya titanoboa aliishi hapo Kizazi chake hakipo tena masalia ya nyoka huyo yanapatikana nchini colombia .

15: Mimea huitaji mwanga wa jua ili kustawi, ila msitu huu wa Amazon unastaajabisha., mwanga wa jua unaopenya katika msitu ule ni mdogo sana lakini bado mimea inastawi kwa kasi.

16: Asilimia kubwa ya madawa ya kisasa yanayotumika hospitalini yanatokea katika mimea ya msitu wa Amazon. Na hadi sasa ni mimea asilimia moja tu! Ambayo imetumika kutengeneza madawa.Bado kuna asilimia 99 haijatumika.

17: Vyakula vingi ambavyo tunakula vinatokana na mimea kutoka Amazon! Mfano Ndizi, Pilipili nyeusi, Chocolate, kahawa, mahindi, mchele na nyanya.

18: Takribani makabila hamsini ya watu wanaoishi katika msitu wa Amazon hayajawahi kamwe kukutana na watu wanaoishi duniani!

19: Kuna matunda takribani elfu tatu katika msitu wa Amazon. Ajabu sasa hadi sasa matunda ambayo dunia imeyatumia ni matunda mia mbili tu. Wewe umekula mangapi kati ya hayo mia mbili???

20: Ikiwa msitu huo utaamuliwa kukatwa, basi utatoweka baada ya miaka arobaini. Yaani itachukua miaka 40 kuisha.

21: Msitu wa Amazon unasaidia kupunguza kasi ya ongezeko la joto. takribani asilimia 20 yahewa safi duniani huzalishwa kutoka kwenye msitu huo.

22: Kwamujibu washirika la kimazingira (WWF) Msitu wa AMAZONI unazalisha asilimia 20 ya majisafi duniani AMAZONI.

23: inakaliwa na viumbe zaidi ya milioni 3 wanyama na mimea pamoja nawakazi wa eneohilo ni milion1
asilimia 60 ya nchi ya PERU imefunikwa na mstu wa Amazon.

24: Kwa mujibu wa Mamlaka za Brazil, inadaiwa mpaka sasa mioto 75,000 zimeteketeza msitu huo na jitihada za kuuzima zinaendelea, moto mkubwa zaidi umewahi kutokea ndani ya Amazon mwaka 2013, lakini pia mwaka jana mioto 33,000 ziliteketeza msitu huo lakini huu wa sasa unaonekana kutekeleza eneo kubwa zaidi!

25: Watu wanaoishi kwenye mstu huu Amazon ni asili yao huko hawawezi toka hata wakijengewa ma gorofa, pia ni kivutio kwa watalii kma wa, hadzabe huku Tanzania na wamaasai ni culture.

26: Msitu wa Amazon upo mbioni kupotea baada shughuri za kibinadamu kushamiri Sana msituni apo. Katika ukataji miti , mashamba na n.k kwa mwaka hufikia sawa na wiwanja 1200 vya mpira vinavyopotea.

27: Wakazi wa msitu wa Amazoni huamini kwamba msitu huo umejaa nafsi zinazozurura usiku, roho zinazosababisha magonjwa, na miungu inayojificha ndani ya mito ikisubiri kuwanasa watu. Fikiria kuhusu Aguaruna, moja kati ya makabila makubwa zaidi nchini Peru. Wanaabudu miungu mitano tofauti: “Baba Shujaa wa Vita,” “Baba wa Maji,” “Mama wa Dunia,” “Baba wa Jua,” na “Baba wa uganga.” Wengi wanaamini kwamba wanadamu wanabadilishwa kuwa mimea na wanyama. Kwa kuwa wanaogopa kuwakasirisha viumbe wa roho, wenyeji huepuka kuwaua wanyama fulani nao huwawinda wengine inapohitajika tu.

Waganga ndio husimamia maisha ya kidini na ya kijamii. Wao hutumia mimea kujipumbaza akili. Watu fulani katika maeneo hayo huwatazamia waganga hao watibu magonjwa, watabiri jinsi uwindaji na mavuno yatakavyokuwa, na kutabiri matukio ya wakati ujao.

28: Wakati Msitu wa Amazon ukiongoza kwa ukubwa duniani unafuatiwa na msitu Congo Zaire wa pili kwa ukubwa.

29: Ndani ya Msitu wa Amazon Kuna mto mkubwa Sana unaoitwa Mto Amazon. Ambao ni wa pili kwa Urefu duniani ukiacha Mto Nile unaoongoza duniani kwa Urefu.

30: Msitu wa Amazon mapafu ya dunia kwani una faida nyingi Sana duniani. Kiafya, kiuchumi, kijamii hata kimazingira.

View attachment 1600951

images-5.jpg
 
Namba 18, sasa kama hayo makabila hayajawahi kukutana na mtu yoyote duniani,, hao watafiti wamewezaje kujua kwamba kuna makabila 50 pasipo kuonana na wananchi wa hayo makabilla???

Namba 6
ni kulingana na mataifa ambayo msitu huo umepita
 
Namba 18, sasa kama hayo makabila hayajawahi kukutana na mtu yoyote duniani,, hao watafiti wamewezaje kujua kwamba kuna makabila 50 pasipo kuonana na wananchi wa hayo makabilla???

Namba 6
ni kulingana na mataifa ambayo msitu huo umepita
 
Kwa hiyo, ikitokea jangwa Sahara ikabadilishwa na kuwa bahari(man made sea) msitu wa Amazon utapotea/utafutika?
Kuna readers digest nilisoma wanasoma MTO Amazon una kiasi cha maji 80% ya maji yanayotiririka mitoni dunia nzima . Na Amazon inagawanyika matawi mawili inapoingia Atlantic ocean na kufanya delta kubwa. Na delta inayotengenezwa na hayo matawi hulingana na nchi moja ndogo sikumbuki ni Belgium au Switzerland. Amazon INA majabu mengi.

Sent from my TECNO-J5 using JamiiForums mobile app
 
9: Katika msitu wa amazon kuna makabila zaidi ya 50 yana ishi hapo watu wameishi kwa maelfu ya miaka iliyo pita lakini watu hao wamekuja kuonekana miaka ya hivi karibuni.
1)Jamii ya watu wa huko Amazon ni warefu?

Kama jibu ni ndio, kwa Nini ni watu warefu ijapokuwa ile jamii ya wenzao wa Congo ni wafupi? Kwa maana tumeaminishwa na sayansi kwamba ufupi(mbilikimo) wa ndugu zetu waishio misitu ya Congo ni kutokana na kukosa mwanga wa jua kwa muda mrefu, Sasa Kama mwanga wa jua SI wanakosa wote?(Amazon&Congo)

2)Huwa inasemwa kwamba kwa kiasi kikubwa/muda mwingi huwa maeneo hayo Yana mvua kubwa Sana, je ni kweli? Kama jibu ni ndio niambie ili nikuulize swali lingine, samahani lakini kwa maswali ya kitoto, ni mtoto wangu huwa ananiuliza, na mie ndio naona nikuulize ili unisaidie.
 
1)Jamii ya watu wa huko Amazon ni warefu?

Kama jibu ni ndio, kwa Nini ni watu warefu ijapokuwa ile jamii ya wenzao wa Congo ni wafupi? Kwa maana tumeaminishwa na sayansi kwamba ufupi(mbilikimo) wa ndugu zetu waishio misitu ya Congo ni kutokana na kukosa mwanga wa jua kwa muda mrefu, Sasa Kama mwanga wa jua SI wanakosa wote?(Amazon&Congo)

2)Huwa inasemwa kwamba kwa kiasi kikubwa/muda mwingi huwa maeneo hayo Yana mvua kubwa Sana, je ni kweli? Kama jibu ni ndio niambie ili nikuulize swali lingine, samahani lakini kwa maswali ya kitoto, ni mtoto wangu huwa ananiuliza, na mie ndio naona nikuulize ili unisaidie.
sidhani kama mwanga wa jua ni sababu ya mtu kua mfupi, urefu na ufupi ni genes....kuhusu mvua ndio lakini kuna vipindi vya jua pia
 
Back
Top Bottom