Mambo 30 usiyoyajua kuhusu msitu wa Amazon

hiyo ya mchanga kupeperuka kutoka sahara na kusafiri juu ya bahari kilomita zaidi ya milioni moja ni ulongo na uchawi.

Huyo Jaguar nasikia ndiyo mnyama hatari kuliko wote
anapanda mti
anaogelea
ana spidi

Yani huna pa kumchenga
Kaka; kipenyo cha dunia ni 12,742km tu; na mzingo wake ni 40,075km sasa sijui huo umbali kutoka Sahara Desert to Amazon just crossing over the Atlantic kwamba ni zaidi ya 1,000,000km sijui umeutoa wapi! Imezidi sana, the longest distance from the most westerly point on the Coast of Africa, Dakar - Senegal say, to the most easterly point on Eastern Cost of Southern America, Rio De Janeiro, Brazil say, over the Atlantic is not more than 6,500km!

Pili, huo mchanga haupeperuki kwa mwezi mmoja, mwaka, au karne; ni millions of years since the existence of the universe! Hata ukipeperuka tani 10 kwa mwaka (very possible; very minimal estimation; vumbi linalotimka Sahara sio la kitoto) kwa hiyo miaka 55milioni unaweza kuona ni tani ngapi hizo! Umeambiwa Msitu wa Amazon una zaidi ya miaka 55 milioni kumbuka hilo.
 
mzee kama unajua tools of language hiyo figure ya 1M ilikuwa exaggeration.kutilia mkazo
pili,mchanga unapeperukaje kuvuka bahari mzee?
ata punje moja haiwezi kusafiri umbali wa km1 juu ya maji sembuse matani?? Halafu eti kazi ya mchanga ni kuirutubisha amazon...ulisikia wapi??Amazon hakuna mchanga au? Plus kati ya michanga isiyo na rutuba ni hiyo ya jangwani.hizo ni stori za vijiwen
 
Aerosol.
 
Sorry chief; nikaelewa vinazungumzwa vitu serious kwenye huu uzi kumbe wengine mnaleta mizaha "tools of language"! Anyway, kuhusu mchanga wa Sahara kuvuka Atlantic soma hizo links za kitaalamu badala ya "stori za vijiwen" ambazo kimsingi wewe ndio unataka kuzileta kwenye huu uzi.
  1. Massive Saharan dust cloud shrouds the Caribbean
  2. The Sahara dust storm has reached the US mainland. Here's what it looks like.
  3. Forecast: Dust and sand from the Sahara | EarthSky.org
  4. https://www.washingtonpost.com/weather/2020/06/29/saharan-dust-exits/
  5. https://www.washingtonpost.com/weather/2020/06/24/sahara-dust-plume-gulf-coast/
Cc: Santos06
 
Umesahau kimoja kuna watafti waligungua chini ya msitu (chini ya aridhi ya msitu) kuna mto mkubwa zaid ya mto Amazon tena
 
Sorry chief; nikaelewa vinazungumzwa vitu serious kwenye huu uzi kumbe wengine mnaleta mizaha "tools of language"! Anyway, kuhusu mchanga wa Sahara kuvuka Atlantic soma hizo links za kitaalamu badala ya "stori za vijiwen" ambazo kimsingi wewe ndio unataka kuzileta kwenye huu uzi.
  1. Massive Saharan dust cloud shrouds the Caribbean
  2. The Sahara dust storm has reached the US mainland. Here's what it looks like.
  3. Forecast: Dust and sand from the Sahara | EarthSky.org
  4. https://www.washingtonpost.com/weather/2020/06/29/saharan-dust-exits/
  5. https://www.washingtonpost.com/weather/2020/06/24/sahara-dust-plume-gulf-coast/
Cc: Santos06
story za vijiweni ndizo zinatrend kuliko reality
 
Habari wana JF,

Nimependa kuandika machache ninayoyafaham juu ya msitu wa Amazon. Utaongeza chochote unachokifaham juu ya msitu huu.

1: Msitu wa Amazon ndio msitu mkubwa zaidi duniani unaopatikana huko America kusini.

2: Kama ulifikiri msitu huu unapatikana Brazil pekee jibu ni hapana msitu huu umegawanyika katika nchi tisa nchi hizo ni Blazil 60% peru 13% colombia 10% na mataifa mengine kama Venezuela, Ecuador, Bolvia, Guyana, Suriname na France Guiana.

3: Msitu huu una eneo lenye ukubwa wa kilomita za mraba 5,500,000 (Milioni 5) yani kwa ukubwa huu nchi ya TANZANIA iingie mara 6 kwenye msitu huo.

4: Kwa mujibu wa wanasayansi wa mimea msitu wa Amazon una umri wa miaka zaidi ya million 55

5: Msitu wa Amazon unakadiriwa kuwa na miti billion 400 na aina mbalimbali za miti zaidi ya 160,000 pia kuna miti ya matunda tofauti tofauti elfu tatu katika msitu huo.

6: Mchanga wa jangwa la sahara hupeperushwa na upepo hupita juu ya bahari Atlantic hadi katika msitu wa amazon ambako hurutubisha katika msitu huo.

7: Katika msitu wa amazon kuna mto umekatisha mto huo unaitwa mto amazon huu ndio mtu mkubwa zaidi duniani na unaingiza maji baharini mara 5 ya mito mingine maajabu ya mto huu kuna muda haueleweki kuna kipindi unapeleka maji kinyume badala ya maji kwenda mashariki yana kuwa yana toka mashariki kwenda magharibi.

8: Asilimia 20% ya oxygen iliyopo dunia inatengenezwa katika msitu wa amazon acha hili pia zaidi ya asilimia 70% ya madawa ya kisasa yana tengenezwa kwa kutumia miti inayo patikana ndani ya msitu wa amazon. Ndio maana unaitwa mapafu ya dunia.

9: Katika msitu wa amazon kuna makabila zaidi ya 50 yana ishi hapo watu wameishi kwa maelfu ya miaka iliyo pita lakini watu hao wamekuja kuonekana miaka ya hivi karibuni.

10: Green anaconda
Hawa ndio nyoka wakubwa zaidi duniani kwa sasa ni aina ya nyoka wanao patikana msitu wa amazon pekee wana rangi ya kijani na madoa meusi.

11: Poison dork frog
Ni aina ya vyura wanaopatikana msitu wa amazon pekee wana sumu kali katika migongo yao mfano uchukue mwiba uchome ugongo wa chura hao kisha ujichome mwiba huo uvuki dakika kumi tunakua tusha kukosa

12: American jaguar
Huyu anapatikana msitu wa amazon pekee Ni mnyama jamii ya paka huyu kafanana na duma ila yeye ni mweusi mwili mzima kama kiwi anapendelea sana kujificha juu ya miti mirefu ana uwezo mkubwa kuogelea ni mnyama mwenye speed kali sana ukimtoa duma .

13: Harpy Eagle
Ni aina ya tai wanaopatikana msitu wa amazon hawa ni wakubwa zaidi hawa ni wapole wanaweza ishi na binadamu bila tatizo .

14: Black caiman
Ni aina ya mamba wenye rangi nyeusi Hawa ni baadhi tu pia inasemekana nyoka mkubwa zaidi kuishi duniani aina ya titanoboa aliishi hapo Kizazi chake hakipo tena masalia ya nyoka huyo yanapatikana nchini colombia .

15: Mimea huitaji mwanga wa jua ili kustawi, ila msitu huu wa Amazon unastaajabisha., mwanga wa jua unaopenya katika msitu ule ni mdogo sana lakini bado mimea inastawi kwa kasi.

16: Asilimia kubwa ya madawa ya kisasa yanayotumika hospitalini yanatokea katika mimea ya msitu wa Amazon. Na hadi sasa ni mimea asilimia moja tu! Ambayo imetumika kutengeneza madawa.Bado kuna asilimia 99 haijatumika.

17: Vyakula vingi ambavyo tunakula vinatokana na mimea kutoka Amazon! Mfano Ndizi, Pilipili nyeusi, Chocolate, kahawa, mahindi, mchele na nyanya.

18: Takribani makabila hamsini ya watu wanaoishi katika msitu wa Amazon hayajawahi kamwe kukutana na watu wanaoishi duniani!

19: Kuna matunda takribani elfu tatu katika msitu wa Amazon. Ajabu sasa hadi sasa matunda ambayo dunia imeyatumia ni matunda mia mbili tu. Wewe umekula mangapi kati ya hayo mia mbili???

20: Ikiwa msitu huo utaamuliwa kukatwa, basi utatoweka baada ya miaka arobaini. Yaani itachukua miaka 40 kuisha.

21: Msitu wa Amazon unasaidia kupunguza kasi ya ongezeko la joto. takribani asilimia 20 yahewa safi duniani huzalishwa kutoka kwenye msitu huo.

22: Kwamujibu washirika la kimazingira (WWF) Msitu wa AMAZONI unazalisha asilimia 20 ya majisafi duniani AMAZONI.

23: inakaliwa na viumbe zaidi ya milioni 3 wanyama na mimea pamoja nawakazi wa eneohilo ni milion1
asilimia 60 ya nchi ya PERU imefunikwa na mstu wa Amazon.

24: Kwa mujibu wa Mamlaka za Brazil, inadaiwa mpaka sasa mioto 75,000 zimeteketeza msitu huo na jitihada za kuuzima zinaendelea, moto mkubwa zaidi umewahi kutokea ndani ya Amazon mwaka 2013, lakini pia mwaka jana mioto 33,000 ziliteketeza msitu huo lakini huu wa sasa unaonekana kutekeleza eneo kubwa zaidi!

25: Watu wanaoishi kwenye mstu huu Amazon ni asili yao huko hawawezi toka hata wakijengewa ma gorofa, pia ni kivutio kwa watalii kma wa, hadzabe huku Tanzania na wamaasai ni culture.

26: Msitu wa Amazon upo mbioni kupotea baada shughuri za kibinadamu kushamiri Sana msituni apo. Katika ukataji miti , mashamba na n.k kwa mwaka hufikia sawa na wiwanja 1200 vya mpira vinavyopotea.

27: Wakazi wa msitu wa Amazoni huamini kwamba msitu huo umejaa nafsi zinazozurura usiku, roho zinazosababisha magonjwa, na miungu inayojificha ndani ya mito ikisubiri kuwanasa watu. Fikiria kuhusu Aguaruna, moja kati ya makabila makubwa zaidi nchini Peru. Wanaabudu miungu mitano tofauti: “Baba Shujaa wa Vita,” “Baba wa Maji,” “Mama wa Dunia,” “Baba wa Jua,” na “Baba wa uganga.” Wengi wanaamini kwamba wanadamu wanabadilishwa kuwa mimea na wanyama. Kwa kuwa wanaogopa kuwakasirisha viumbe wa roho, wenyeji huepuka kuwaua wanyama fulani nao huwawinda wengine inapohitajika tu.

Waganga ndio husimamia maisha ya kidini na ya kijamii. Wao hutumia mimea kujipumbaza akili. Watu fulani katika maeneo hayo huwatazamia waganga hao watibu magonjwa, watabiri jinsi uwindaji na mavuno yatakavyokuwa, na kutabiri matukio ya wakati ujao.

28: Wakati Msitu wa Amazon ukiongoza kwa ukubwa duniani unafuatiwa na msitu Congo Zaire wa pili kwa ukubwa.

29: Ndani ya Msitu wa Amazon Kuna mto mkubwa Sana unaoitwa Mto Amazon. Ambao ni wa pili kwa Urefu duniani ukiacha Mto Nile unaoongoza duniani kwa Urefu.

30: Msitu wa Amazon mapafu ya dunia kwani una faida nyingi Sana duniani. Kiafya, kiuchumi, kijamii hata kimazingira.

Asante interesting
 
Back
Top Bottom