Mambo 20 yanayouponza upinzani Tanzania

Mambo 20 yanayouponza upinzani Tanzania

CalvinKimaro

JF-Expert Member
Joined
Sep 11, 2017
Posts
245
Reaction score
314
yafuatayo ni mambo 20 yanayouponza upinzani Tanzania:

1. Mitandaoni haswa Twitter Instagram na Jamii forum. Utadhani wapiga kura woote wanasoma Twitter! Utadhani tabu zao zitapatiwa ufumbuzi Twitter! Lakini kwa wenzao CCM wanawatumia mitandao hii kwa akaunti zao kama MTAGA kuelezea zaidi yanayofanywa na yaliyotekelezwa kwa umakini wa hali ya juu sanaaa bila kupepesa macho kabisaaaaa.

2. Press conferences: wanashindana kuita press conference. Adui yao anachapa kazi vijijini kutatua kero. Wao wanatatua kero kwenye press conference!

3. BBC Swahili service: ni TZ pekee wapinzani hawakatiki BBC. Utadhani Ikulu iko London!

4. DW: kama BBC hapo juu

5. Jumuia zao za vijana: hazijitambui. Hawana uwezo wa kubuni miradi au mikakati mipya zaidi ya nao kuitisha press conferences na kutoa vitisho hewa.

7. Ukabila: kauli na matendo yao yamejaa harufu ya ukabila. Mfano ni juzi wanatuambia wa kaskazini wanaonewa! Hili nalinukuu toka kwenye msiba wa Mzee Ndesamburo uwanja wa MASHUJAA mjini moshi ambao Mbowe aliongea kauli hiyo.

8. Kukosa nidhamu hasa ya utoaji taarifa na matumizi.

9. Kushabikia maadili yasiyokubalika na jamii. Ukijinasabisha na LGBTQIs kwa jamii kama ya Tanzania umekwisha!

10. Kupinga kila kitu: reli, ndege, bandari, makanikia, n.k. ni kupinga tu!

11. Vituko misibani: wakati jamii inaheshimu mno misiba hata uwe wa mwizi, mchawi, fisadi, mzinzi wao ni jukwaa la comedy. Mara wazike mbwa kwa misa, mara wagombane na polisi wakizuiwa kumzungusha maiti sokoni, mara wagombee u mc msibani, mara wanawake wabebe jeneza, mara watake kuombwa radhi ndani ya sala ya wafu, mara waje msibani wamevaa sare ya chama!

12. Kutokuishi majimboni. Mtu ni mbunge Hai au Ujiji au Arusha au Tarime lakini muda wote Yuko Bongo Dalisalama?

13. Kushindwa kuendesha harakati za kisiasa bila maandamano na mikutano ya hadhara. Hata hapa jirani Kenya wapinzani hawategemei maandamano au mikutano ya hadhara lakini wanasikika. Hapa wameshindwa.

14. Kukosa vigezo makini vya uongozi. Yeyote anaweza kupewa uongozi.

15. Kushindwa kuwa taasisi na kutegemea mtu kama kwamba ni private company

16. Kuzoa viongozi toka Chama tawala na kuwatukuza mno. Watarudia kosa hili tena 2020.

17. Kujichanganya na wanaharakati uchwara mpaka tofauti kati ya Chama na wanaharakati unatoweka. Wanaharakati uchwara wakisema au kutenda hovyo vyama vyao vinahusishwa.

18. Kuongoza katika ukosefu wa demokrasia na utawala wa Sheria ndani ya vyama vyao. CCM inabadili viongozi toka 1995. Wao wanafia ofisini na wanakataa waziwazi kung'atuka eti wanapendwa! Wanasahau hata Yaya Jammeh na Mugabe ambao waliwasema vibaya nao walidai wanapendwa!

19. Kujidhihirisha hawaitakii mema nchi na watu wake. Chuki ya kupita kiasi dhidi ya nchi wanayotaka kuiongoza

20. Kushindwa kubaini adui yao ni CCM na kudhani ni Serikali. Matokeo yake adui yao mkuu hana bughudha hata kidogo. Wanagombana na dola. CCM hana upinzani. Ambaye angempinga yuko bize kugombana na dola!
 
Back
Top Bottom