GE2025 Mamalishe, babalishe na bodaboda waungana kumdhamini mgombea urais wa CCM Samia Suluhu Hassan

GE2025 Mamalishe, babalishe na bodaboda waungana kumdhamini mgombea urais wa CCM Samia Suluhu Hassan

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Mkalukungone Mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
2,437
Reaction score
5,235
Wajasiriamali wadogo wakiwemo mamalishe, babalishe na vijana wa bodaboda mkoani Arusha leo Jumanne Agosti 12, 2025 wamejitokeza kwa wingi kumuunga mkono na kumdhamini mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan.

Wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi, wajasiriamali hao walifika katika Ofisi za CCM Wilaya ya Arusha na kusaini fomu za udhamini, wakisema wameona mabadiliko makubwa katika maisha yao kutokana na sera na miradi iliyotekelezwa katika miaka minne ya uongozi wa Samia.

“Mama Samia ametupatia mazingira bora ya kufanyia biashara, mikopo yenye masharti nafuu na masoko ya bidhaa zetu. Ndiyo maana tupo tayari kumdhamini na kumpa kura zetu,” amesema Asha Mohamed, mama lishe kutoka Soko Kuu la Arusha.

Wajasiriamali wadogo wakiwemo mamalishe, babalishe na vijana wa bodaboda mkoani Arusha leo Jumanne Agosti 12, 2025 wamejitokeza kwa wingi kumuunga mkono na kumdhamini mgombea urais wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Samia Suluhu Hassan.

Wakiongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Kenani Kihongosi, wajasiriamali hao walifika katika Ofisi za CCM Wilaya ya Arusha na kusaini fomu za udhamini, wakisema wameona mabadiliko makubwa katika maisha yao kutokana na sera na miradi iliyotekelezwa katika miaka minne ya wa Samia.

“Mama Samia ametupatia mazingira bora ya kufanyia biashara, mikopo yenye masharti nafuu na masoko ya bidhaa zetu. Ndiyo maana tupo tayari kumdhamini na kumpa kura zetu,” amesema Asha Mohamed, mama lishe kutoka Soko Kuu la Arusha.

Bill ngapi nazo zimekusanywamoo?
 
IMG-20250812-WA0004.jpg
 
Back
Top Bottom