Mama yake Zitto avamiwa

Dah hata kama ni competation fanyeni fair competation ila kama ndo hivi hii ni unfair competation na si vizuri kumdhuru mtu kwa ajili ya maslahi yako au ya wengine
 
Huku tunakoipeleka nchi sasa siko, hebu watanzania tuwe na utu, haya madaraka yatatupeleka wapi??? madaraka ni bora kuliko roho na utu wa mtu???
 
Sijui Mh. Zitto amewakosea nini viongozi wenzake wa CHADEMA.
Zitto ametupa wosia mapema tuwe makini na 'Provocation agents'

wewe ni mmoja kati ya agents ambao tumeshapewa taarifa zao, na hatushangai kwasababu ccm imeshikwa pabaya mmekuwa chama cha propaganda.
 
Last edited by a moderator:
Tayari Zito amesha eleza hivyo mjadala huu umefungwa. Kila mtu akafanye nazi vinginevyo mtakuwa mnapiga majungu.
 
Mama yake Zitto ni kibogoyo nini? Hata kucha hana? Igondhu umekuwaje

mkuu umesoma mada umeielewa au umekurupuka tu, mama yake zitto amevamiwa na kutaka kuuawa na makada wa chadema na walikuwa na appointment naye wakitaka awasaidie cement kwa ajili ya ujenzi wa ofisi yao tabata relini..
 
Tayari Zito amesha eleza hivyo mjadala huu umefungwa. Kila mtu akafanye nazi vinginevyo mtakuwa mnapiga majungu.
aliyevamiwa ni mama yake zitto sio zitto. hata hivyo zitto amesema yy sio msemaji wa familia
 
Yuko slaa, mbowe na wengineo katika viongozi wa chadema? Hata pole ya kinafiki hamtoi?
 
GAzeti la Mtanzania linaripoti Mama mzazi wa zitto kabwe amevamiwa na majambazi.
Walikuwa wanataka computer na kiwekea kumbukumbu flash.
Kada wa chadema atajwa kutambuliwa na mama huyo.Alikuwa miongoni wa majambazi waliomvamia.

Hivi jina la Tanzania likitumiwa kwa manufaa ya wachache si tunaweza kupinga maana mtanzania limekuwa gazeti la CCM na propaganda mbaya juu ya CDM. I hate this, mwenye mama kasema wao wanasema mama kamtambua kada wa CHADEMA?
 
ni nani??? wamemtaja?? na je walifanikisha lengo lao???

amesema anamfahamu mmojawapo, ni kada wa chadema alimuomba cement kwa ajili ya ujenzi wa ofisi, akawakubalia kuwapa, walipofika kuchukua fedha ndipo wakataka kumlipua kwa risasi, ameokolewa na dereva wake
 
Wanachadema wanafiki na wasio na roho ya utu hawachelewagi sema zitto kaitengeneza hii move.
 
Mtanzania na propaganda wamesema mama yake Zitto alimwona kada wa chadema na anamfahamu yale yale ya baba yake Mtela Mwampamba, mtu amuonye tu Shida binti Salum ana heshima kwenye jamii asijiingize kwenye propaganda za kusaidia usaliti wa mwanane wa masalia, mama tulia kula vya mwanao pole pole dhambi ya uongo ni mauti , sasa hili dili litakufa kama lilivyokufa la video, pole mama habari ya leo ni liwale
Wakati mwingine tusifanye haraka kukanusha. Kuna watu ambao ni mamburula kwelikweli. Usishangae kwamba kuna lijitu la CHADEMA limelipwa milioni kadhaa ili liende likafanye huo uvamizi kwa wazi ili mama Zitto amuone na waongeze ya kusema katika propaganda zao dhidi ya CHADEMA. Haitashangaza kwamba jamaa kaahidiwa tu kwamba wewe nenda, halafu ukienda mahakamani utashinda kesi. Wala sitashangaa. Kama usalama wa taifa walikuwa tayari kuwanunua watu ili watoe ushahidi wa uongo dhidi ya Lwakatare, watashindwa nini kununua mtu ili afanye uvamizi fake kwa mama Zitto halafu Mwigulu aje na hoja ya kwamba anaweza kutoa ushahidi hata mbinguni?
Mimi nafikiri tusifanye haraka kukataa kwamba hakuwemo kada wa CCM bali tutafute kumjua ni nani na kwanini alifanya hivyo?
 
Mama yake Zitto ni kibogoyo nini? Hata kucha hana? Igondhu umekuwaje

una akili sawa sawa wewe???mbona unataka kupotosha mada na ukweli??? mama yake zitto amemtambua kada wa chadema. hata hivyo tuwe tunasoma na kuelewa kabla ya kuchangia.
 
Sijui Mh. Zitto amewakosea nini viongozi wenzake wa CHADEMA.

Just think about it isn't it obvious? There is no way Slaa na mbowe wakamtuma huyo "kada wa chadema" wakati hiki ni kipindi kigumu kutokana na kesi ya Lwakatare. Hili kwa mtu aliye na akili yake hawezi kuamini lakini kwa wengine wasiofikiri au wanaotaka negative kwa upande mwengine watataka kusisitiza kuwa Viongozi wa juu wanajua na walikuwa nyuma ya mpango huu.

Mama Zitto anweza kuwa amevamiwa lakini majambazi gani watake laptop na simu pasipo kuchora ramani inayoeleweka, hao ni vibaka na kama huyo Kada inwezekana anatumiwa. Lakini huyu mama itakuwa vizuri Amseme huyo kada ni nani ili sheria ifuate mkondo wake. Awe na uhakika ili kisije kikawa ni kikwazo cha Zitto kwa chama.

Naamini hadi sasa Polisi wanajua ukweli halisi wa nini kilichowatokea Ulimboka, kibanda, na Lwakatare lakini wanatafuta jinsi ya kusolve issue hii kwa kuwaundanisha CHADEMA ili kesi hizo ziishe.

Angalizo kama watashindwa kusolve hivi vitu Mwaka huu wewe utakuwa shahidi 2015 endapo hali itakuwa ngumu kwa CCM basi wataliibua ili
1. Propaganda ya kuchafua chadema kupitia matukio maana nao chadema watakuwa wakihubiri kuwa CCM ndio wahusika wakuu
2. Mambo yakliwa magumu zaidi basi watafuta connections ili Slaa na Mbowe na Viongozi wengine wafunguliwe mashitaka ili wasisimame kugombea au wafungwe

Sasa ole wao wamiscalculate.

One hour in Politics it is a lifetime.
 
nanukuu tu ''Ushauri- tuwe makini na "Agente provocatuers" au in English "provocation agents" nyakati kama hizi. Calmness is the best protection against provocations. Nadhani mmenipata"
Watanzania wengi tunatabia ya kufuatilia upepo unakoelekea na si unapotokea, nimekuwa mfuatiliaji mzuri sana wa ''Detective movies'' nukuu hiyo hapo juu kwangu mie ni Bonge la ''Clue'' sintoufuata upepo uendako nafuatilia utokako!! Siasa zetu kwa sasa zinahitaji umakini sana, haya matukio ya kutekwa waandishi wa habari, wanasiasa kuhusishwa na ugaidi ni mambo ambayo naamini yanafanyika kwa kiwango cha hali ya juu sana iwe yanafanywa kweli au ya kupandikiza! kwa mara ya kwanza nilistuka sana baada ya kuiona video ''Rwakatale' simhukumu kwani ukweli utajulikana mahakamani, kwajinsi maelezo yalivyokuwa mle ilkuwa kama naagalia FBI movies vile na kwa sasa huenda mbinu hii ya ''kutia mtu wasiwasi'' kutisha kwa maneno au vitendo vya kuteka vikaendelea kwani huenda inawafaidisha wanaosingiziwa au kusingizia!! what makes it more interesting na movie hii ni kuwa wahusika ni CCM/SERIKALI na CHADEMA ( mhukika mkuu hajajulikana bado), kwa undani zaidi kuna wahusika wengine wadogo wadogo toka pande zote mbili ambao wamegawanyika na kuishia kutoa siri za wanaodaiwa kuwa wahusika wakuu.... hawana umoja hawa!! hawana siri hawa!! kitu kinacholeta utamu wa movie hii... naamini kutakuwa na mwisho wake ambao ni kuelekea 2015. Kibaya zaidi ni kuwa huenda wahusika wakuu hawatambui kuwa mwisho wa movie hii ni kuwa STELINGI ATAKUFA!!!! napita......
 
Hivi familia ya zitto wameikosea nini chadema. Kila siku misukosuko ya kutishiwa kutolewa roho

Na wewe unahangaika kama unataka kutaga,
ID kibao unauulizaa unajijibu, kazi unayo hadi 2015 utakuwa na ID 200! Kila la Heri....!
 
Vyovyote iwavyo, tunampa pole sana Mama huyu, Zito na wanafamilia wengine.

Hii nchi haitakuja kuwa na baraka. Kama tunaanza kuwateka mpaka wazee hawa, akina Mama, tena mlemavu, hizo baraka tutazipataje? Hawa ni wazazi wetu wanastahili kulindwa lakini sasa, kinyume chake wenye nguvu wanawaandama wanyonge.

Wamewang'oa meno na kucha vijana akina Ulimboka na akina Kibanda, wameona haitoshi, sasa wanawaendea na akina Mama wazee!
 
Back
Top Bottom