Mama wa mtoto wangu anataka nimsomeshe

Mama wa mtoto wangu anataka nimsomeshe

Yaaan we acha tu, kila siku namwambia mama angu usijal atabadili lakin wap! mama ni miongini mwa viongoz kanisani kwa hiyo anaumia sana anavyoona hivi kwa mwanae.
Wasije kua washakushika ufahamu ndo maana unashindwa kufanya maamuzi!hawachelewi! Kuwa makini huku ukimuomba Mungu!

Yaani ningemjua mama ako ningemwambia awaambie hao wazee wenzie wafunge waombe kuwa achanisha na kuwatenganisha kabisa mi sipendi ujinga kabisa ht kwa kaka zangu na ndugu zangu!

Aisee hebu ona yaani mama ako anaumia sbb ya mtu mwingine?! Kweli ? Hebu achana na huyo binti!
Na uanze kumuomba Mungu ss!
 
Wasije kua washakushika ufahamu ndo maana unashindwa kufanya maamuzi!hawachelewi! Kuwa makini huku ukimuomba Mungu!

Yaani ningemjua mama ako ningemwambia awaambie hao wazee wenzie wafunge waombe kuwa achanisha na kuwatenganisha kabisa mi sipendi ujinga kabisa ht kwa kaka zangu na ndugu zangu!
Ubarikiwe sana! roho ya kutokusikia sauti ya mungu nahisi inanitafuna mpendwa! yaan hata ibadani mchungaji anafundisha kuhusu zinaa..halafu narudi nyumbani nalala na mwanamke asie mke wangu, naumia sana! mpaka siku hizi sina amani kabisa moyoni, nakosa furaha.
 
Mkuu kama unatoa msaada wa kusomesha mke wa MTU sawa Fanya ivo maana hapo akimaliza chuo anaolewa na mwanaume mwingine
 
Lipa ada tu.. si umezaa naye huyo demu?? Atamsaidia hata mwanao
 
Mimi muislamu mwenzie nipo tayar kumlipia ada na michango mingine, tafadhar nitumie mawasiliano yake.
 
Kama amekuzalia msomeshe halafu akipata ajira kama akikuacha usiwaze maana yeye ndio atatunza mwanao kila kitu we utakuwa unapeleka zawadi tu kwa mtoto
 
Kaka hapo tumia hekima ya MUNGU ili wewe usilipe hiyo ada ya chuo au gharama za chuo, kwa sababu kama angekuwa ni wa kwako au mke wako , au mwanamke anayekupenda kweli na muaminifu katika penzi lenu au uhusiano wenu kwa dhati kabisa angefanya jambo juu ya kuweka sawa imani zenu na kuwa na imani moja.
Nikiwa ninamaana angeonyesha nia , au hata kuchukua hatua ya kutafuta wazee ili waongee na kumuelewesha mzazi wake juu ya kufuata imani yako. Kwahiyo kilichopo hapo ni mpango wa kupata faida zaidi baada ya kujenga nyumba ya pamoja sasa anataka umlipie gharama za chuo kwa kivuli cha mke , lakini kweli hapo kitakacho fuata ni kilio. Nina maana bado moyoni mwake hayupo na wewe kama mume mtakayezeeka na kutunzana pamoja, bali unatumiwa tu na baada ya malengo yake kukamilika utaona vumbi tu.
Hebu tusome kwa pamoja Zaburi 45:10-11, imeandikwa, " Sikia, binti, utazame, utege sikio lako, Uwasahau watu wako na nyumba ya baba yako.
Naye mfalme(mume)atautamani uzuri wako, Maana ndiye bwana wako, nawe umsujudie".
Sasa , kama kweli angekua anakupenda na kukubali kuwa wewe ni mume wake angekusikiliza na kukubali kubadilisha imani yake na kukufuata.
Nafikiri mpaka hapo utakuwa umepata jibu fulani juu ya future yako na mtoto wenu.
suala la kubadiri dini si dogo kama udhaniavyo, mtu anaweza kuwa na mapenzi nawe ila kubadiri dini ikawa ngumu.

ndoa ngapi wameishi watu wa dini tofauti na wamefariki wakiwa ivo na hakuna cha faida wala nini?

hata akimsomesha na akiondoka tayari ni mama mtoto na mtoto atafaidi matunda ya elimu ya mama. ni nani aijuaye kesho yake hadi useme wanataka pata faida kutoka kwa jamaa.

wacha amsomeshe mkewe maana amejitoa kiwango cha kutosha (kuwa na mtu ambaye wazazi hawamkubali)

braza msomeshe mama watoto hujui kesho imebeba nini? unaweza yumba kiuchumi akawa mkombozi, unaweza fariki ukamuacha na msingi wa kumlea mwanao. yakitokea tofauti (japo sina wazo ilo) unalipokea pia una anza upya.
 
My brother Mentor kama kawaida yako kuibua hoja fikirishi. Kwa ulichokieleza hapo juu umemaliza kila kitu.

Kwa ufupi, nilipanga maishani nisiwe na mahusiano yeyote zaidi ya mke wangu. Ulipofika wakati nilipata binti mkristo akaishia kunichanganya nikavundua nilikua bado chekechea kwenye tasnia ya mahusiano. Kosa kubwa nililolifanya, nikahamishia kusudi langu la kumuoa binti wa kiislam niliyekua namfaham kitambo lakini hatukuwa na chochote kati yetu, zaidi ya heshima kubwa ya kaka na dada.

Nilimuuliza uko tayari kubadili dini? Akasema hana tatizo ila itabidi awaulize wazazi wake. Aliwasilisha wazo kwao mzee wake alilikubali kwa shingo upande kuogopa kumuumiza mtoto wake mpendwa.

Kosa lingine, tukaanzisha mahusiano na kukubaliana kupata mtoto kabla ya kufikia muafaka suala la dini na ndoa. Nilikua nimeweka malengo nikiwa na umri flan niwe na mtoto.

Baada ya mtoto, binti akagomz kubadili dini na toka alipojifungua tulikua tunaishi wote. Kwa ufupi tumesumbuana na hilo nikaenda kwao msimamo wa mzee ukabaki palepale, wananipenda sana ila nibadili dini. Miaka minne ilitosha kufikia tamati nikaacha kila kitu na kuanza upya.

Mke wangu wa sasa analiewewa hilo toka mwanzo na alisema hatopenda kuona mtoto anapata shida. Nalipa kodi yao ya nyumba, nikamshauri asome, akasoma certificake kwa sababu alitaka kubadili fani nyingine, nikamsomesha diploma, amefanya vizuri na sasa akitaka kuendelea ntamsomesha.

Ntafanya hivyo hadi atakapopata mtu wa kumuoa kwa sababu ya mtoto.

Namshukuru Mungu tumejaliwa watoto na huyu mke wangu maizha yanaendelea.

Ndio maana nikamshauri jamaa, kama anauwezo, amsomeshe kwa manufaa ya mwanawe kwamba huyo ni mama wa mtoto wake.

Kwenye kujifunza, laiti tungeweza kukaa mbali na mahusiano kabla ya kuoa kama imani zinavyorushauri, dunia ingekea sehem salama na bora kwa kiasi kikubwa mno.


Hii inafaa kuwa sticky note; Moderator PainKiller !

mafoleni husika hapa!
 
Back
Top Bottom