Mama wa mtoto wangu anataka nimsomeshe

Mama wa mtoto wangu anataka nimsomeshe

Habarini wa ndugu,

Mimi ni mwanaume mwenye mke na mtoto mmoja. Tumeishi takribani miaka minne pamoja bila kufunga ndoa kwa sababu ya utofauti wa dini.

Mimi ni mkristo na yeye muislam nimehangaikia sana kuhusu kubadili dini lakini wazazi wake wamekataa katu katu.

Nimeamua tu tuishi hivi hivi japokua sipendi kabisa maana ni kama tunazini na kuendelea kuvunja amri ya sita kwa muda usiojulikana.

Kiukweli nashindwa kumuacha huyu binti kwa sababu tometoka nae mbali sana, tulipanga chumba na sasa tuko kwenye nyumba yetu.

Hoja ya msingi ni hii hapa.
AMENIAMBIA ANATAKA KUSOMA MWAKANI INABIDI NIANDAE ADA""
sasa tatizo linakuja baba yake hapendi kabisa mwanae aishi na mimi, mtoto wake yupo kwangu, akirudi kwao kuja huwa mpaka mizozo yani.

Na chuo anachotaka kusoma kipo huko huko kwao, je si naweza lipa ada halafu akimaliza wakaniachia manyoya! Au nilipe tu jamani. Nahisi naweza somesha mke wa mtu hapa.

USHAURI JAMANI. NILIPE MIZIGO?
Subiri wazazi wake wafe kwanza. Nina uhakika hii haitachukua hata miaka 10, then mbatize huyo hawala yako fungeni ndoa dhen ndo mambo ya shule yaanze.
 
acha woga mlipie ili mwanao pia awe na mama aliyeenda shule na atajua umuhimu wa shule kwa mwanao.
kuhusu kupoteza usijali hivi wewe ungeambiwa ulipe elfu tano kila tendo la ndoa ulilofanya naye je lingefikia ada yako?
achilia mbali kufuliwa nguo na kila starehe uliopata ungeweza kilipa?
we lipa akisepa kivyake wako watoto wadogo wana kazi nzuri wanakutafuta hivyo usiogope akisepa
 
Mmh,mm mwanamke lakini kwa hili jipange unaweza dondokea pua,ukajutaa
Labda umsomeshe kwa manufaa ya kizazi chenu.
 
Huyo baba yake si anakuchukia wewe anampenda mwanae, asomeshwe na baba yake, shenzi kabsa mwambie hicho sio kipaombele chako kwan wewe ni HELSB
 
Hebu funguka zaidi mkuu huenda tukapata cha kujifunza.

Kuna msemo huwa napenda kuutumia: It takes more than love for two people to be together. Hata kama mnapendana lazima muangalie na 'other compatibilities' kama zipo kabla hamjaanza mahusiano.
Changamoto aliyonayo huyu ndugu ni kuwa alishaanza kuogelea baharini sasa inakuwa ngumu kutoka. Hayo ya dini waliyajua tangu mwanzo mwa mahusiano wao. Labda walidhani binti akipata mimba wazazi watakubali. lakini pia, je binti mwenyewe msimamo wake ni upi? Sijasoma mtoa mada ameelezeaje msimamo wa binti. Ndiyo maana wachangiaji wengi - suprisingly, hata wa kike - wamepatwa hofu juu ya hitaji la mama wa mtoto wake.

Thread kama hizi huwa nazipenda kwa ajili ya kufundishia vijana wetu ambao bado hawajafikia huku mbali;

USHAURI KWANZA KWA MTOA MADA: Kama kweli mnapendana na mnataka kuwa pamoja, jua msimamo wa huyo mama wa mwanao kwenye hili kwanza.

FUNZO KWA WENGINE: Msikimbilie kusema mnapendana tu. Angalieni kama na mengine mna-nia moja.
Mkuu huyu bint anasema hawezi amua lolote linaloweza kwenda kinyuma na wazizi wake. Kama wazazi wamekstaa basi yeye hawez badili dini
 
Huyo baba yake si anakuchukia wewe anampenda mwanae, asomeshwe na baba yake, shenzi kabsa mwambie hicho sio kipaombele chako kwan wewe ni HELSB
Hahaha!!!! dah umenifanya nicheke sana.
 
Mpe elimu kwaajili ya mtoto wako mpe elimu huku ukijiwekea garantee ya kuwa mwanao au watoto wako hawatakuja kuishi kwa shida as longer as mama yao atakuwa na elimu nzuri na kazi hilo la kuachana ni mipango ya mungu Kama anakupenda hatokuja kukuacha kamwe na dini atabadilisha iz just a matter of time nashangaa sio wanawake wote wanaowaacha waume zao baada ya kusoma wanao fanya hivyo ni wale wachache wasiokuwa na fadhira
 
Cha msingi atafute chuo ambacho kipo karibu na makazi yenu awe anaenda anarudi nyumbani hapo hakutakuwa na ntafaruku
 
Ww huna msimamo unaona kabisa dini kikwazo unaendelea kuishi nae ili kiwe nn? Na ndugu zako wanakuangalia tu? Hebu fanya maamuzi ,ni mambo 2, either abadirishe dini mfunge ndoa au hataki muachane ,mwache aende fanya yako oa upya,anza upya km hataki kukufuata we si ndo mwanaume bwana
 
My brother Mentor kama kawaida yako kuibua hoja fikirishi. Kwa ulichokieleza hapo juu umemaliza kila kitu.

Kwa ufupi, nilipanga maishani nisiwe na mahusiano yeyote zaidi ya mke wangu. Ulipofika wakati nilipata binti mkristo akaishia kunichanganya nikavundua nilikua bado chekechea kwenye tasnia ya mahusiano. Kosa kubwa nililolifanya, nikahamishia kusudi langu la kumuoa binti wa kiislam niliyekua namfaham kitambo lakini hatukuwa na chochote kati yetu, zaidi ya heshima kubwa ya kaka na dada.

Nilimuuliza uko tayari kubadili dini? Akasema hana tatizo ila itabidi awaulize wazazi wake. Aliwasilisha wazo kwao mzee wake alilikubali kwa shingo upande kuogopa kumuumiza mtoto wake mpendwa.

Kosa lingine, tukaanzisha mahusiano na kukubaliana kupata mtoto kabla ya kufikia muafaka suala la dini na ndoa. Nilikua nimeweka malengo nikiwa na umri flan niwe na mtoto.

Baada ya mtoto, binti akagomz kubadili dini na toka alipojifungua tulikua tunaishi wote. Kwa ufupi tumesumbuana na hilo nikaenda kwao msimamo wa mzee ukabaki palepale, wananipenda sana ila nibadili dini. Miaka minne ilitosha kufikia tamati nikaacha kila kitu na kuanza upya.

Mke wangu wa sasa analiewewa hilo toka mwanzo na alisema hatopenda kuona mtoto anapata shida. Nalipa kodi yao ya nyumba, nikamshauri asome, akasoma certificake kwa sababu alitaka kubadili fani nyingine, nikamsomesha diploma, amefanya vizuri na sasa akitaka kuendelea ntamsomesha.

Ntafanya hivyo hadi atakapopata mtu wa kumuoa kwa sababu ya mtoto.

Namshukuru Mungu tumejaliwa watoto na huyu mke wangu maizha yanaendelea.

Ndio maana nikamshauri jamaa, kama anauwezo, amsomeshe kwa manufaa ya mwanawe kwamba huyo ni mama wa mtoto wake.

Kwenye kujifunza, laiti tungeweza kukaa mbali na mahusiano kabla ya kuoa kama imani zinavyorushauri, dunia ingekea sehem salama na bora kwa kiasi kikubwa mno.
Aisee pongezi kwa huyo mkeo!

Mmh !
 
Akielimika yeye atafaidika mwanao toa pesa mpeleke shule bana
 
Mke anawasikiliza wazazi wake mkuu
Basi hapo hamna mke unapoteza muda!
Km amekupenda kweli angekusikiliza ww!

Wewe ni mwanaume kuwa na msimamo,mwambie huwezi kumlipia ada sbb mahusiamo yenu hayaeleweki!

Mpe option,km hawezi kubadili dini mkafunga ndoa basi mahusiano yaishee sbb huwezi kuishi hivyo ndani ya zinaa
 
Ww huna msimamo unaona kabisa dini kikwazo unaendelea kuishi nae ili kiwe nn? Na ndugu zako wanakuangalia tu? Hebu fanya maamuzi ,mi mambo 2, eithet abadirishe dini mgunge ndoa au hataki muachane ,mwache aende fanya yako oa upya,anza upya km hataki kukufuata we si ndo mwanaume bwana
Yaaan we acha tu, kila siku namwambia mama angu usijal atabadili lakin wap! mama ni miongini mwa viongoz kanisani kwa hiyo anaumia sana anavyoona hivi kwa mwanae.
 
Mkuu huyu bint anasema hawezi amua lolote linaloweza kwenda kinyuma na wazizi wake. Kama wazazi wamekstaa basi yeye hawez badili dini
Yaani kumbe ww majibu unayo ila unajifariji!
Acha kupoteza muda!

Na ww mwambie huwezi somesha mwanamke ambae si mke wako!
Akasomeshwe na wazazi wake anaowasikiliza! Full stop!
Jmn mwanaume ni kichwa!
 
Mkuu huyu bint anasema hawezi amua lolote linaloweza kwenda kinyuma na wazizi wake. Kama wazazi wamekstaa basi yeye hawez badili dini
Yaani kumbe ww majibu unayo ila unajifariji!
Acha kupoteza muda!

Na ww mwambie huwezi somesha mwanamke ambae si mke wako!
Akasomeshwe na wazazi wake anaowasikiliza! Full stop!
Jmn mwanaume ni kichwa!
 
Back
Top Bottom