Herbalist Dr MziziMkavu
JF-Expert Member
- Feb 3, 2009
- 42,318
- 33,125
Mtoto Alexander Draper mwenye kilo 251
Mama mmoja wa nchini Marekani amepandikishwa kizimbani kwa kufanya uzembe na kupuuzia afya ya mtoto wake na kupelekea mtoto huyo kuwa mnene kuliko kawaida, kwani pamoja na kuwa na umri mdogo wa miaka 14 mtoto huyo ana uzito wa kilo 251 . Katika kesi hiyo ambayo imekuwa gumzo nchini Marekani mama huyo mkazi wa South Carolina, Jerri Gray mwenye umri wa miaka 49 anatuhumiwa kufanya uzembe na kupuuzia afya ya mtoto wake wa kiume na kupelekea mtoto huyo awe na kilo 251 akiwa na umri wa miaka 14.
Jerri Gray ameachiwa kutoka jela kwa dhamana ya dola 61,000 lakini bado yupo kwenye kupigania kujumuika na mwanae Alexander Draper ambaye alichukuliwa na maafisa wa ustawi wa jamii.
Mahakama iliambiwa kwamba mama huyo alikimbia na mtoto wake pindi baada ya maafisa wa ustawi wa jamii kumfikisha mahakamani wakitishia kumnyang'anya mtoto wake.
Polisi walifanikiwa kugundua sehemu aliyokuwa amejificha baada ya kufuatilia simu zake alizokuwa akiwapigia marafiki zake.
Mama huyo alikamatwa na kupandishwa kizimbani huku mtoto wake akichukuliwa na maafisa wa ustawi wa jamii.
Mama huyo alijitetea kwamba kama asingelazimika kufanya kazi mbili basi hali ya mtoto wake ingekuwa tofauti.
Mama huyo alidai kuwa alikuwa hana uwezo wa kugharamikia matibabu ya mtoto wake huyo 'Kibonge' mwenye uzito wa kilo 251 hivi sasa.
Kesi ya mama huyo imewavutia watu wengi sana nchini Marekani huku baadhi ya wapiga picha wakichukua video za mama akitoka jela kwa nia ya kutengeneza documentary itakayohusu maisha ya mtoto wake.
Mtoto huyo bado yupo kwenye uangalizi wa maafisa wa ustawi wa jamii.
Source: nifahamishe.com