Elections 2010 Mama Sitta aeleza alivyokamatwa na TAKUKURU

Mzito Kabwela

JF-Expert Member
Nov 28, 2009
18,857
7,617
SIKU moja baada ya Takukuru mkoani Tabora kumnasa Waziri wa Maendeleo ya Jamiii Jinsia na Watoto Margaret Simwanza Sitta, jana aliibuka na kusema taasisi hiyo inawabambikia wananchi makosa ili waonekane wanafanya kazi.

Alisema kutokana na tukio lililompata juzi, sasa anawasiliana na wanasheria wake kuona achukue hatua gani dhidi ya maafisa wa Takukuru waliodai kumkamata kwa rushwa.


Waziri Sitta alisema kwamba juzi saa 7:30 usiku aliamshwa kwa mlio wa simu ya Catheri Sepetu iliyomwomba afike gesti ya Camise kuona mtoto mgonjwa. "Niliomba anielekeze gesti hiyo iko wapi ili niende kumwona huyo mgonjwa," alisema Mama Sitta.


Hata hivyo Magreti alidai kwamba kutokana kutoyafahamu maeneo hayo alimwomba katibu mwenenzi CCM manispaa Tabora wafuatane katika maeneo hayo aliyoambiwa na Sepetu.


Alisema alipofika karibu na njia ya kwenda katika gesti hiyo, wakatokea vijana zaidi ya sita na kusimamisha gari alipowahoji nyie ni nani ndipo walipotoa vitambulisho na kujitambulisha kwamba wao ni Takukuru na kwamba sasa yuko chini ya ulinzi.


Alisema walimchukua hadi ofisini kwao na kuanza kumpekua huku wakimwambia alikuwa akigawa rushwa kwa wajumbe.


"Nikahoji huyo ndiyo mgonjwa mliokuwa mnaniitia? Hawakumjibu badala yake waliendelea kunipekua mkoba wangu na mkoba wa mdogo wangu na kumwamrsisha katibu mwenezi Rashid Ramadhan akubali kwamba alikuwa akigawa fedha,"alisema Sitta.


"Katibu huyo alibaki anaduwaa kwani alichokuwa anajuwa ni kumsindikiza waziri kwa mgonjwa. Alishangaa kulazimishwa aandike maelezo kueleza kina nanni alikuwa anawagawia fedha. Akajibu siwezi kuandika uwongo,"


Waziri Sitta aliendelea kueleza kuwa akiwa ofisini hapo, alimuuliza Sepetu kulikoni, naye alimjibu alilazimishwa kumpigia simu na baada ya kuwakatalia, walimpiga na kuchukua simu yake na kuanza kumpigia (Sitta) na ilipoita walimlazimisha aongee na waziri kwa maelekezo watakayompa.


"Niliwahoji iwapo mnafanya haya kwangu ambaye alau najua sheria kwa wale ambao hawajui inakuaje kama siyo kuwaonea wananchi na kupoteza fedha za serikali kuendesha kesi za kubambikiza."alieleza.


Waziri Sitta alisema iwapo viongozi wa Takukuru wataachwa kukemewa kuendelea na tabia hiyo, itakuwa vigumu kuelewa nani kabambikiwa kesi na nanni ana kesi halali. Habari ya Victor Kinambile.


SOURCE: MWANANCHI
 
Labda mchezo wa mafisadi mama, shombo upakwe wewe anuke mumeo..teh...teh...teh...!!!
 
vumilia mama...ukiwa mchokozi usiogope ngumi za usoni..na wewe sasa saa 7 usiku unaenda kumuona mgonjwa wapi?aaah mi napata mashaka bana ,kwa nini usingoje asubuhi ndo uende kwani kulikuwa na ulazima gani wewe kwenda usiku?????mmmhhh mama hii haijakaa vizuri
 
Takukuru wanatakiwa kuwa na vinasa sauti kama ushahidi vinginevyo ushahidi gani utathibitisha hayo ,me no know! wanajisemea wajamaica
 
Mama Sitta wewe ni daktari? Au ndio unatibu watoto na bahasha, simu na shillingi milioni moja!
 
He! mgonjwa Guest!! na sio Hospitali...
We mama wee! msalie mtume....
kwahiyo yule bwana anajidai mpambanaji mkubwa wa ufisadi! kumbe....................
Tutaona/tutasikia mengi miezi mitatu hii
 
huamini nini, maelezo ya takukuru au utetezi wa mama 6 ?

utetezi wa mama sita hauna mshiko, mama alikuwa anatoa rushwa huyo, wewe unaambiwa mtoto mgonjwa guest, sasa na huyo kiongozi wa ccm alikuwa nae ama alimpigia simu, na hivyo vitu alivyokutwa navyo vilkuwa ni vya nin usiku wa manane?
 
of course amebambikiwa.. hivi hamjiuliza pamoja na kelele zote za watu kukutwa wakitaka kutoa rushwa hakuna hata mmoja ambaye amefikishwa mahakamani? Na wote watashiriki Uchaguzi J'pili. Lengo ni kutengeneza majalada ambayo yatatumiwa na Kamati Kuu kuwaengua baadhi ya wagombea ambao wanaweza kushinda kabisa uchaguzi.
 
aache uhuni huyu mama kwa tunaomjua huwa anatoa rushwa siku zoote!
Thanks Mkuu... ni vigumu sana kupata ukweli kwa sasa hasa tukielewa kwamba hizi primaries zote ziko run na corrupt campaigners.. si tabora, si kondoa, si kilolo

Naomba kuongezea tu kwamba inaniwia vigumu sana kutoamini kwamba huyu mama hakuwa akihonga... she is capable of doing it na hata kale kabinti kake kaliko pale TFDA kanaongoza kwa kuhongwa na wahindi wa maduka ya madawa... APPLE DONT FALL TOO FAR FROM THE TREE
 
of course amebambikiwa.. Hivi hamjiuliza pamoja na kelele zote za watu kukutwa wakitaka kutoa rushwa hakuna hata mmoja ambaye amefikishwa mahakamani? Na wote watashiriki uchaguzi j'pili. lengo ni kutengeneza majalada ambayo yatatumiwa na kamati kuu kuwaengua baadhi ya wagombea ambao wanaweza kushinda kabisa uchaguzi.
thanks mkuu... Hapo kwenye kuenguana ndio patachimbika

time will tell
 
Ingekuwa busara angemwambia mtoa taarifa ampeleke mtoto hospitali na wao wakutanie huko.....sasa yeye kwenda gesti saa 7 usiku na milioni moja?.....
 
Lengo ni kutengeneza majalada ambayo yatatumiwa na Kamati Kuu kuwaengua baadhi ya wagombea ambao wanaweza kushinda kabisa uchaguzi.

MM hivi wagombea huwa wanapewa feedback na kamati kuu baada ya kunominate majina?? Na whtf mgombea ni mjumbe pia wa kamati kuu?????

My point is........ Kamati kuu ikiamua kufyeka jina lako si wanafyeka tu?
 
MM hivi wagombea huwa wanapewa feedback na kamati kuu baada ya kunominate majina??

Hakuna Feed Back.. mahali pekee ambapo mtu angeweza kukata rufaa ni Mkutano Mkuu wa CCM ambao ndio wanaweza kutengua uamuzi wa chombo kingine chochote... Umeshafanyika kwa mwaka huu..!

Na whtf mgombea ni mjumbe pia wa kamati kuu?????

Wakati mjadala unapofikia zamu yake huondolewa, hashiriki.


My point is........ Kamati kuu ikiamua kufyeka jina lako si wanafyeka tu?

yep! hawadaiwi maelezo na mtu yeyote.
 
Back
Top Bottom