Ndachuwa
JF-Expert Member
- Mar 8, 2006
- 6,269
- 4,569
Mazingira ya Mama sitta yanatia shaka kidogo hasa muda na mahali.Lakini pia ningependa kujua huyo mtoto ana uhusianano gani na Mama Sitta.Kwanini mtoto mgonjwa asiwe amelazwa hosipital kwaajili ya matibabu na badala yake awe gest house ?.
upo pia uwezekano mkubwa hasa kipindi hiki cha kampeni mgombea kujikuta anakwenda sehemu za ajabu ajabu pengine kujijengea mazingira mazuri kwa wapiga kura.Inawezekana Mama Sitta aliamua kweli kwenda kumwangalia mgonjwa lakini yakaandaliwa mazingira yakumchafua ili aenguliwe kwenye vikao vya mchujo kamati kuu.
Ifahamike wazi Mama Sitta ni miongoni mwa wabunge wa CCM wanaojipambanua kama wapiganaji dhidi ya lile kundi la waathirika wa kashfa za kifasadi ambao sasa wanafanya kila juhudi kuhakikisha wanakuwa na nguvu ndani ya Bunge.Ukifuatilia kwa makini harakati zote za ufisadi katika chaguzi za ndani za CCM utagundua kwamba wanaCCM wanaokumbana na mkono wa TAKUKURU ni wale wanaojiita wapiganaji !.
Na kama umejitenga na wenzio kwamba hutaki kupokea wala kutoa rushwa kwa nini uwashawishi wapiga kura kwa pesa na zawadi ili wakuchague?