Mama Salma, Ally Kessy wapinga wanafunzi waliopata mimba kurudishwa shuleni, wasema dini haziruhusu

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,059
Mama Salma amesema ili kudhibiti ubora wa elimu serikali iboreshe maslahi ya walimu, kutilia mkazo elimu ya awali, kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa walimu, na pia haungi mkono suala la kuwarudisha wanafunzi waliopata mimba shuleni kwa kuwa itakua ni kuendekeza hilo swala wakati linakatazwa na dini zote na mila na desturi zinakataza kupata mimba kabla ya wakati

Ally Kessy nae amepinga vikali suala hilo na kusema wasichana wanaofanya mapenzi na shule elimu yao inashuka na kusema dini yake ya uislamu inapinga vikali na waislamu wanaounga mkono hilo hao sio waisilamu na kuunga mkono hilo ni kuongeza watoto wa mtaani

Mh! Kaazi kwei kweli,haoni ya kwamba wanawake wataendelea kuwa nyuma kielimu? Mwanafunzi kupata ujauzito ni kama ajali katika maisha yake,kupata ajali siyo mwisho wa kutimiza malengo. Yaani anawabagua binti zake. Kweli mwenye shibe hamjui mwenye njaa. Hapo cha maana alichokiongea ni maslahi ya waalimu ila anasahau mazingira na hali ya maisha ndiyo chanzo cha hizo mimba.hapo anaongelea watoto wa maskini ila kwa matajiri hutawasikia maana wanauwezo wakuflash bila mzazi kujua kupitia pocket money wanazopewa na wazazi.
 
Wanaopata mimba ni viherehere vyao-JK

wanaopata mimba mashuleni wasiruhusiwe kuendelea na masomo-Mama Salima

Connect dots hapa ni nani alimshauri mwenzake.

Leo nimegundua siri ya urembo na inawezekana hata katika teuzi hawa ndio wana-play part kubwa nani akae pale na nani atoke na nani aingie.
 
Huku ni kutokuwatakia mema vijana ambao wanaajiriwa wakiwa wabichi kabisa kutoka chuo!
Si ndio tutategeka nao hao mwanafunzi wazazi mpaka tukome!
Naungana na mama salma
 
Mama Salma amesema ili kudhibiti ubora wa elimu serikali iboreshe maslahi ya walimu, kutilia mkazo elimu ya awali, kufanya ukaguzi wa mara kwa mara kwa walimu, na pia haungi mkono suala la kuwarudisha wanafunzi waliopata mimba shuleni kwa kuwa itakua ni kuendekeza hilo swala wakati linakatazwa na dini zote na mila na desturi zinakataza kupata mimba kabla ya wakati

Yaonekana ana mtazamo mmoja na mme wake, mme wake alisema wanafunzi kupata mimba ni viherehere vyao!
 
Back
Top Bottom