Mama Rwakatare, Meya Kimbisa, Sofia Simba...

n00b

JF-Expert Member
Apr 10, 2008
1,006
2,667
Meya Kimbisa na Sofia Simba sasa wameamua kuokoka na wanasali kanisa la Mama Rwakatare, hivi hii ni serious issue au kuna issue nyuma ya pazia?
 
Meya Kimbisa na Sofia Simba sasa wameamua kuokoka na wanasali kanisa la Mama Rwakatare, hivi hii ni serious issue au kuna issue nyuma ya pazia?

Tell us Pimbi, what do you think and who can think on their behalf?
 


Tupe chanzo cha habari yako hii?
Malila, as quoted above, issue ya Mama Sofia haikuwa ngeni, lakini jana nilimwona hata Kimbisa kanisani akitoa ushuhuda. Sina tatizo na kuwa muumini wa kanisa hilo na wengine wengi (wanasiasa) niliowaona ambao walikuwa wakitoa shuhuda zao na kupewa fursa za kunena mbele za madhabahu, wasiwasi wangu ni kama wamedhamiria kweli toka kwenye mioyo yao, kama ni kutoka moyoni basi watenda vema, kama wanacheza deal wajue wanacheza mchezo wa hatari ambao kinyume chake wanaweza kukabiliana na balaa kubwa hapo mbeleni na sishauri wala sitamani kuona wengine wakifanya usanii kupitia njia ya imani/dini.

Mkuu Ibra, kama nimekosea basi samahani mkuu wangu. Naomba kama topic inakugusa kwa namna moja ama nyingine au imekukera wafahamishe mods wafute kabisa. Nimeianzisha kwa wema kabisa mkuu wangu
 
Meya Kimbisa.....eamua kuokoka na wanasali kanisa la Mama Rwakatare, hivi hii ni serious issue au kuna issue nyuma ya pazia?

hivi unawajua vizuri wanasiasa wewe? makamba hujawahi kumuona makanisani?

kwa taarifa yako, inawezekana hakuna aliyeokoka hapo, hata rwakatare mwenyewe. we subiri tu utaona
 
Wanasiasa ni viumbe wa ajabu sana, wanaweza kufanya vituko ilimradi vinawapatia kura!! Juzi juzi nimensikia Lyatonga Mrema akiwa anahojiwa pale TBC wakiwa na Lipumba ananukuu aya za Q'oran tukufu kwa kiarabu; Lipumba alishindwa kujizuia ikabidi acheke !!

Thi is the extent politicians can go in search of votes.
 

dr. wewe umeokoka? kwa maelezo yako hapo juu ni kwamba nawe ulikuwemo kwenye kadamnasi hiyo. kama ni hivyo basi wape moyo wahusika utakuwa umefanya jambo la maana sana utashiriki katika kuwasaidia wahusika katika hilo.
 
Politicians like to manipulate the true sons of God! Just be aware! It could be the strategy to use that church as the platform to excel in their political agendas
 
Sasa hivi imekuwa ni kasumba kubwa ya watu kuweza kujipatia utajiri ama kuendesha maisha yao kwa nji za imani za kidini.

Kwa mfano, imekuwa ni kawaida kwa wahubiri wengi sasa hivi kutumia matatizo aliyo nayo mwanadamu kumvuta aende akajisalimishe mahali hapo na mataizo mengi ni yale ya kiuchumi. Matangazo yo husheheni mambo kama huna gari njoo Mikocheni B, unaishi kwenye nyumba ya kupanga njoo kwa Nguruo upate upako, una madeni sugu njoo kwa Mzee wa Upako n.k na wengine hujiita serikali za mbinguni. Ili uyapate haya yote ni lazima uingie mfukoni ndipo ubaikiwe na baraka wanazozitoa zinafuatana na kiwango cha pesa unachotoa. Kwa mwenye laki moja hawezi kupewa upako sawasawa na mwenye elfu kumi.

Kwa hiyo Sophia simba yamkini amefuta kupata upako na si kumuungamia BWANA awe mwokozi wa maisha yake.
 
hivi unawajua vizuri wanasiasa wewe? makamba hujawahi kumuona makanisani?

kwa taarifa yako, inawezekana hakuna aliyeokoka hapo, hata rwakatare mwenyewe. we subiri tu utaona
Hivi mnamkumbuka yule kijana aliyekamatwa na kichwa cha mtu pale Muhimbili?

Kabla ya hapo Rwakatare alikuwa amedai kuwa alimtungua akiwa anaruka kwa ungo na kumdondosha kwenye paa la kanisa lake. Sasa baada ya kumuombea na kumuokoa ilitokeaje mpaka akaenda kuua mtu? Au alifanya hivyo kwa msaada wa Rwakatare?

Hawa manabii, maaskofu wa kujisimika wenyewe, nk. ni watu hatari sana. Wote ni wafanyabiashara, hakuna dini wala imani. Wachunguze wote, Rwakatare, Kakobe, Mwingira,etc. They have one thing in common. UTAJIRI. At the expense of their poor congregations.
 

Kumbuka methali isemayo"UKITAKA CHA UVUNGUNI NI SHARTI UINAME"
 
huyu mama ananikera sana (mh ma' Dk Rwakatare aka mtumishi wa bwana) nilitegemea kuteuliwa kushika kiti cha ubunge kupitia viti maalumu angestaarabika ,kwa kuweka sound proof kwenye kanisa lake ilikuondoa kero ya kalele inayotoka kanisani kwake na kusababisha kero kwa majirani wanao mzunguka.

fikiria kuna watoto wadogo wa shule wanatoka mashuleni jioni wanaitaji mapumziko wanakutana na sebene zito toka kanisani humo, wanafanyeje home works zao na pia wanasomaje katika mazingira yenye kelele kama zile, ? na hua kuna mkesha kanisani hapo, ni balaaa....!!!!!!!
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…