Hii ni kauli mbiu tu ya kumfanya mwanamke kuwa wa thamani machoni pa watu na si kama wewe unavyofikiria,ila ni ukweli mtupu mwanamke amepewa uwezo mkubwa sana wa kufanya mambo mengi kwa wakati mmoja na bado akasema am okey,uvumilivu wake,upendo wake,huruma yake,heshima yake,busara yake ujasiri wake ingawaje anaonekana ni dhaifu,busara na hekima yake,maarifa yake japokuwa yaonekana ni madogo hakika hakuna kama mama,mama ni mama tu.
Hii kauli mbiu ilikuja kutokana na mama kutotambulika katika jamii,alikuwa anaonekana ni chombo dhaifu kisichofaa,hakuthaminiwa,alikuwa hana kauli yoyote katika jamii,alihesabika kama mtoto tu,Baba alikuwa anakula kwanza kisha mama ndiyo ale na wanawe,kulima ilikuwa ni kazi ya mama na wanae,kuangalia mazingira ya nyumbani na malezi ya watoto ni kazi ya mama,mama ahakikishe mumewe afurahi,watoto wafurahi,nyumbani kuna chakula cha kutosha,kwa haya yote haya kwanini wasiseme Nani kama mama,!!! Mama ni mama.