Na huyu huyu ndio anatakiwa awatibu wagonjwa Ocean Road Hospital; kuna conflict of interests kati ya huduma za Dr. Ngoma kama mkurugenzi wa Ocean Road na pia kama mkurugenzi wa Dr. Ngoma hospital kitu ambacho nashindwa kufafanua ni kwanini wizara ya Afya inalifumbia macho suala la huyu daktari!! His conduct at Ocean road hospital of referring patients to his hospital and charging them exorbitantly is very unethical!!
Hujui ni hospitali ya private?yes tena nakumbuka kuna silku nlilazwa pale sasa the nezt day nikaletewa bili then nikapiga simu nyumbani ili waje walipe bili, cha ajabu dokta alivyoingia wodini cah kwanza alichoniuliza ni malipo,nikamwambi kuwa my mom yupo njiani anakuja kulipa,akaniambia mpigie simu muulize amefika wapi maana mimi siwezi kukupa huduma yoyote mpaka waje walipe
duuh niliishiwa nguvu
Na huyu huyu ndio anatakiwa awatibu wagonjwa Ocean Road Hospital; kuna conflict of interests kati ya huduma za Dr. Ngoma kama mkurugenzi wa Ocean Road na pia kama mkurugenzi wa Dr. Ngoma hospital kitu ambacho nashindwa kufafanua ni kwanini wizara ya Afya inalifumbia macho suala la huyu daktari!! His conduct at Ocean road hospital of referring patients to his hospital and charging them exorbitantly is very unethical!!
Kwa mtu asiyefahamu anaweza kudhani kuwa huyu dr ngoma anasingiziwa, ni bora ukatembelee pale ocean road utaona jinsi huduma zinavyo zorota kila kukicha, wagonjwa wanalala chini, watumishi hawako motivated at all na wengi wanafanya kazi wanavyojisikia, hauwezikuamini hii hospitali iko umbali wa mita 50 tu kutoka ikulu na mita 1000 kutoka wizara ya afya,huyu bwana ni mshirika mkubwa sana wa Blandina Nyoni na chochote anachosema Nyoni ambaye ni katibu mkuu wizara ya Afya hawezi kupinga. Lakini pia ana urafiki na mkuu wa nchi. Huwezi kuamini hii hospitali ina function kama pango la wanyang'anyi.
Kuna kipindi huwachukua wagonjwa wenye uwezo kifedha na kuwahamishia hospitalini kwake na kuwaleta kwenye huduma ya mionzi kwa kulipia na dawa za chemotherapy huchukuliwa kutoka Ocean road na pesa anazopata huenda Mama ngoma. Na hii imefanya madaktari wenzake nao kufungua hospitali zao na kutoa hizo tiba za Kansa kwa gharama za juu kupitia mgongo wa ocean road mfano ni dr Msemo wa ocean road kufungua hospitali yake tabata, na hapa kinachotokea ni kugombania wagonjwa wenye uwezo. Wale maskini siku zote wanaambiwa foleni ni kubwa kwenye mionzi na madawa ya Chemotherapy yamekwisha wakati wale wanaotoka kwenye hospitali za maboss hawa wanaendelea kutibiwa na maskini wanajifia.
Serikali isipo ingilia kati hapa kila siku watu wakipewa rufaa kwenda ocean road ndo inakuwa kama umepewa death sentence, tunajua wenzetu mnaweza kwenda kutibiwa India na ulaya, lakini tuboresheeni na sisi hizi za kwetu. Kwani Ngoma ndo peke yake mwenye uwezo wa kuongoza hii taasisi nyeti ya serikali, He has been there for more than ten years na sasa anafanya kazi kwa mazoea na wizi tu, na ndo maana taasisi haiendelei kwa kipindi chote hiki.
Poleni sana wakuu.
Uzuri wake JamiiForums inatupa uhuru wa kutoa malalamiko yetu na inapitiwa na viongozi labda wanaweza kushughulikia hili tatizo.
Wabunge mtakaosoma hii taarifa tunawaomba mfanye uchunguzi hili swala.
wadau
mimi nimewahi kwenda kutibiwa pale kwa mama ngoma hospital, yani dokta ngoma he is money oriented yeye ndio specialist wa magonjwa yote katika hospitali yake na yeye ndio bosi,kama hayupo basi huduma inayopatikana pale ni first aid,
sasa one day nilienda nilikua na matatizo ilikua usiku,na nilitakiwa kufanyiwa ultra sound wale madokta wa zamu akaniambia imefungiwa ofisini kwa bosi (dokta ngoma) so wakashauri wanipe dawa za kutuliza maumivu na dripu mpaka kesho yake asubuhi atakapokuja bosi wao,nikakubali maana hali ilikua tete
asubuhi bosi wao alikuja na alichojibu akaniambia nilipie tena kitanda atakuja kunifanyia matibabu jioni,nililipia elfu arobaini nikasuri dokta ngoma alipokuja jioni nikalipia ultra sound laki moja na ishirini the nikapata matibau sasa nikaandikiwa dawa za kuchukua nilioenda kaunta kulipia nikaambiwa dawa ni shiling laki moja na themanini,mmh nikaondoka nikaenda nakiete nikapata zile dawa kwa shilingi elfu thelathini na tano tu
'
sasa najiuliza hivi dokta ngoma anatibu wagonjwa au anafanya biashara?