Mama Ngoma hospital wanatibu wagonjwa au wanafanya biashara? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Ngoma hospital wanatibu wagonjwa au wanafanya biashara?

Discussion in 'JF Doctor' started by Mtende, Jan 13, 2012.

 1. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #1
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,071
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  Wadau,

  Mimi nimewahi kwenda kutibiwa pale kwa mama ngoma hospital, yani dokta ngoma he is money oriented yeye ndio specialist wa magonjwa yote katika hospitali yake na yeye ndio bosi,kama hayupo basi huduma inayopatikana pale ni first aid.

  Sasa one day nilienda nilikua na matatizo ilikua usiku,na nilitakiwa kufanyiwa ultra sound wale madokta wa zamu akaniambia imefungiwa ofisini kwa bosi (dokta ngoma) so wakashauri wanipe dawa za kutuliza maumivu na dripu mpaka kesho yake asubuhi atakapokuja bosi wao,nikakubali maana hali ilikua tete.

  Asubuhi bosi wao alikuja na alichojibu akaniambia nilipie tena kitanda atakuja kunifanyia matibabu jioni,nililipia elfu arobaini nikasuri dokta ngoma alipokuja jioni nikalipia ultra sound laki moja na ishirini the nikapata matibau sasa nikaandikiwa dawa za kuchukua nilioenda kaunta kulipia nikaambiwa dawa ni shiling laki moja na themanini, mmh nikaondoka nikaenda nakiete nikapata zile dawa kwa shilingi elfu thelathini na tano tu.

  Sasa najiuliza, hivi dokta Ngoma anatibu wagonjwa au anafanya biashara?
   
 2. JS

  JS JF-Expert Member

  #2
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 2,065
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 135
  Mfanyabiashara yule hana lolote wako ghali sana. Inabidi atengeneze faida eti
   
 3. B

  Bulesi JF-Expert Member

  #3
  Jan 13, 2012
  Joined: May 14, 2008
  Messages: 6,447
  Likes Received: 414
  Trophy Points: 180
  Na huyu huyu ndio anatakiwa awatibu wagonjwa Ocean Road Hospital; kuna conflict of interests kati ya huduma za Dr. Ngoma kama mkurugenzi wa Ocean Road na pia kama mkurugenzi wa Dr. Ngoma hospital kitu ambacho nashindwa kufafanua ni kwanini wizara ya Afya inalifumbia macho suala la huyu daktari!! His conduct at Ocean road hospital of referring patients to his hospital and charging them exorbitantly is very unethical!!
   
 4. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #4
  Jan 13, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,071
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  yes tena nakumbuka kuna silku nlilazwa pale sasa the nezt day nikaletewa bili then nikapiga simu nyumbani ili waje walipe bili, cha ajabu dokta alivyoingia wodini cah kwanza alichoniuliza ni malipo,nikamwambi kuwa my mom yupo njiani anakuja kulipa,akaniambia mpigie simu muulize amefika wapi maana mimi siwezi kukupa huduma yoyote mpaka waje walipe

  duuh niliishiwa nguvu
   
 5. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #5
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Hujui ni hospitali ya private?
  Umeenda kutibiwa kwa malipo,
  kudaiwa imekuwa nongwa?
  Mwananyamala mnaponda!
  Amana mnaponda!
  Mhimbili mnaponda
  MOI mnaponda.
  Bora huko kwa Ngoma mnakopondwa.
   
 6. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #6
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Binafsi simfagilii Ngoma na Hospitali yake.
  Huduma pale Mama Ngoma Hosp. ni below standard kwa sana.
  Lakini pia Watanzania mjue afya ni gharama.
  Nchi zinazotambua hilo kila mwananchi ana insuarance.
  Ni vizuri kama Ngoma anawaamsha
   
 7. Sigma

  Sigma JF-Expert Member

  #7
  Jan 13, 2012
  Joined: Feb 26, 2011
  Messages: 5,014
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
  Ukienda kwa mwanasheria kuongea naye tu kwa dk 15 unapewa bili- laki moja.
  Lakini daktari kukuona na kukuandikiwa dawa unataka bure.
  Tena tunawapigia simu watuSMS dawa twende tukachukue pharmacy tunaona sawa.
   
 8. Mganga wa Jadi

  Mganga wa Jadi JF-Expert Member

  #8
  Jan 14, 2012
  Joined: Mar 12, 2008
  Messages: 278
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa mtu asiyefahamu anaweza kudhani kuwa huyu dr ngoma anasingiziwa, ni bora ukatembelee pale ocean road utaona jinsi huduma zinavyo zorota kila kukicha, wagonjwa wanalala chini, watumishi hawako motivated at all na wengi wanafanya kazi wanavyojisikia, hauwezikuamini hii hospitali iko umbali wa mita 50 tu kutoka ikulu na mita 1000 kutoka wizara ya afya,huyu bwana ni mshirika mkubwa sana wa Blandina Nyoni na chochote anachosema Nyoni ambaye ni katibu mkuu wizara ya Afya hawezi kupinga. Lakini pia ana urafiki na mkuu wa nchi. Huwezi kuamini hii hospitali ina function kama pango la wanyang'anyi.

  Kuna kipindi huwachukua wagonjwa wenye uwezo kifedha na kuwahamishia hospitalini kwake na kuwaleta kwenye huduma ya mionzi kwa kulipia na dawa za chemotherapy huchukuliwa kutoka Ocean road na pesa anazopata huenda Mama ngoma. Na hii imefanya madaktari wenzake nao kufungua hospitali zao na kutoa hizo tiba za Kansa kwa gharama za juu kupitia mgongo wa ocean road mfano ni dr Msemo wa ocean road kufungua hospitali yake tabata, na hapa kinachotokea ni kugombania wagonjwa wenye uwezo. Wale maskini siku zote wanaambiwa foleni ni kubwa kwenye mionzi na madawa ya Chemotherapy yamekwisha wakati wale wanaotoka kwenye hospitali za maboss hawa wanaendelea kutibiwa na maskini wanajifia.

  Serikali isipo ingilia kati hapa kila siku watu wakipewa rufaa kwenda ocean road ndo inakuwa kama umepewa death sentence, tunajua wenzetu mnaweza kwenda kutibiwa India na ulaya, lakini tuboresheeni na sisi hizi za kwetu. Kwani Ngoma ndo peke yake mwenye uwezo wa kuongoza hii taasisi nyeti ya serikali, He has been there for more than ten years na sasa anafanya kazi kwa mazoea na wizi tu, na ndo maana taasisi haiendelei kwa kipindi chote hiki.
   
 9. k

  kakolo Senior Member

  #9
  Jan 14, 2012
  Joined: Jul 7, 2011
  Messages: 176
  Likes Received: 31
  Trophy Points: 45
  Ni kweli kabisa, nilienda kumuona huyu dr katika hospital yake its a shock. Lakini ndio hatujui hilo jengo kajengaje ukiongeza na unyeti wa huduma za matibabu ndio unyeti wa hizo gharama pia.
  Lakini kutumia facilities za mlala hoi its beyond belief. Kuna kipindi kifaa cha machine ya chemo kilichomolewa kikaibiwa watu wakakosa huduma + na hii unaweza amini hao wenye hospital za private its very convicing huenda walikihamisha tu.
  Kwa hizo bills wachache watamudu.
   
 10. KakaJambazi

  KakaJambazi JF-Expert Member

  #10
  Jan 14, 2012
  Joined: Jun 5, 2009
  Messages: 15,030
  Likes Received: 3,231
  Trophy Points: 280
  Mi nilijuaga ni hospitali ya kupima "ngoma", kunasiku nilikua na tripu ya kwenda Mwenge, basi nikajikuta naingia humo kwa minajili ya kupima ngoma. Nilivutiwa na lile bango aliloliweka pale la yeye,mkewe na watoto wake wote takribani 5 ni madokta.
   
 11. jonal rashidi

  jonal rashidi Senior Member

  #11
  Jan 16, 2012
  Joined: Aug 27, 2011
  Messages: 121
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  dah! aisee
   
 12. K

  Kintiku JF-Expert Member

  #12
  Jan 16, 2012
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 611
  Likes Received: 72
  Trophy Points: 45
  Hii ni mojawapo ya maajabu ya duniani na inapatikana Tz tu. Mkurugenzi ya Taasisi ya Kansa, na yeye ana taasisi yake (ni Active Mkurugenzi), wagonjwa wanatolewa Ocean Rd wanapelekwa Mwenge, na ikionekana wanahitaji huduma ya mionzi wanatolewa tena Mwenge to Ocean Rd. Kuna ka vicious cycle fulani hivi.

  Majengo makubwa uwekezaji wa hali ya juu- lakini upande wa HR hovyo kabisa- kisa ugonjwa ule ule wa Watanzania, ajiri ndugu yako, kabila yako, au dini yako. Hospitali ya Dr. Msemo leo naiweka kiporo maana ni kopo na mfuniko na Mama Ngoma nadhani mshauri wao ni mmoja. Hapa ndipo alipolazwa mwandishi wa BBC aliyefariki hivi karibuni- Kuna mtu amewahi kupitia maabara ya hiyo hospitali?. Naomba wataalamu wa maabara mtueleze muda (standard) wa vipimo kama Malaria(BS), Urinalysis, Typhoid na Sukari (fasting) kisha nitaongea kuhusu vipimo pale kwa Msemo
   
 13. L

  Losemo Senior Member

  #13
  Jan 17, 2012
  Joined: Mar 30, 2010
  Messages: 183
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna gari pale land cruiser mkonga. Ukitaka mgonjwa wako wampeleke ocian road kwa mionzi unalipia nasikia shs 40,000 kwa siku. Hilo gari la serkali, Dereva wa serikali, na hizo hela zinaingia kwake. Hata muda anaotumia kuhudumia wagonjwa pale alipaswa kuwahudumia waganjwa kule alikoajiriwa ( When are u commig back jesus we are tired)
   
 14. Kwisimla

  Kwisimla Senior Member

  #14
  Jan 19, 2012
  Joined: Apr 15, 2011
  Messages: 124
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  I am so sorry for you, that was extremely expensive..........
   
 15. Oxlade-Chamberlain

  Oxlade-Chamberlain JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2012
  Joined: May 26, 2009
  Messages: 7,928
  Likes Received: 103
  Trophy Points: 160
  Poleni sana wakuu.

  Uzuri wake JamiiForums inatupa uhuru wa kutoa malalamiko yetu na inapitiwa na viongozi labda wanaweza kushughulikia hili tatizo.

  Wabunge mtakaosoma hii taarifa tunawaomba mfanye uchunguzi hili swala.
   
 16. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,071
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180
  hapo umesema ikweli mkuu ngoma is too much jamani,money front huduma hovyooooo
   
 17. Mtende

  Mtende JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2012
  Joined: Sep 27, 2010
  Messages: 4,071
  Likes Received: 338
  Trophy Points: 180

  kweli kabisa imefika wakati sasa serikali inabidi iwe strict
   
 18. Pdidy

  Pdidy JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2012
  Joined: Nov 22, 2007
  Messages: 33,606
  Likes Received: 5,781
  Trophy Points: 280
  atakaejibu hili swali wachaga wanamwita """""itooooooooooondoooooooooooooooo"""""""""""""""""

  kwa nini biashara ni nini kwanza??na ungekuwa ujalipa ningekujibu kwa kuwa umelipa then jibu unalo angekuwa anatibu pekeesi ungemwita na mumeo alalae kile kitanda kilichokuwa wazi pembeni yako kwakuwa amlipii lakini kwa kuwa ulilipa jibu unalo
   
 19. kau

  kau Member

  #19
  Jan 21, 2012
  Joined: Dec 21, 2011
  Messages: 80
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Jamani kama madokta wenyewe ndo hawa tutaishi kweliiii??????? sababu hawa ndo watu wanastahili kuwa kipaumbele kwenye kuonyesha UTU lakini hao ndo wauaji wakubwaaaaaaaaaaaaaa................
   
 20. n

  nndondo JF-Expert Member

  #20
  Jan 21, 2012
  Joined: Feb 1, 2010
  Messages: 1,250
  Likes Received: 535
  Trophy Points: 280
  Naliliona ni hilo la kuwa na exact service na ile anayoisimamia, ni kweli kakaa sana ocean road, nafikiri its hight time vijana kama wakina Dr Julie Makani winner wa Pfizer award ya young african scientist 2011 waanze kuchukua madaraka haya makubwa, imefika wakati ngoma aende kusimamia hospitali yake kwa makini zaidi, Lingine ambalo hamalisema ni kwamba haweki wazi kwamba huduma yake ni ya kumfanya mgonjwa afe bila taabu sana yaani ni pallative care jambo ambalo nimejaribu kuangalia kwenye maandiko yote pale hospitali kwake sijaona kitu kama hicho.

  kwa hiyo anaibiwa wagonjwa kwa kuwapa matumaini potofu anapofika kwamba unaweza kupona, huku akijua kabisa ni terminal cases, familia zinaishia kufanya maamuzi ya jazba ya kulipa mamilioni ya pesa by the time wanajua wameliwa ni pale mgonjwa anapokua hoi kabisa ama pale anapofariki. Juu ya garama na kukosa utu kwenye huduma hili ni la kweli, walau watakujali ukiwa bado pale lakini moto utauona siku mgonjwa wako amefariki.

  Binafsi nililazimika kwenda lugalo mara mbili mbili baada ya watendaji wake kwa makusudi kuni mislead kwamba maiti ingepokelewa bila death certificate inayotolewa nao kwa kuwa nilikua nadaiwa shilingi laki mbili hii ni baada ya kuwa nimeshalazwa pale zaidi ya mwezi na tayari nimeshalipia zaidi ya 4m kwa matibabu na huduma laki mbili ziliwatoa roho wakati nilikua nawahisha maiti lugalo ikawekewe dawa nikasema kuna mtu atakuja kulipia hili deni kule lugalo huduma zinaishia sas saba basi nilifika mortuary lugalo naulizwa kitu ambacho nilishawakumbusha pale ngoma wakaniambia we nenda tu wanapokea, nikarudi nikawachamba sana na kuwaambia huo ni ushenzi na unafiki maiti ilibidi niiache nje pale lugalo kwa kuomba tu waombolezaji wengine waniangalialie mimi nimerudi kwa ngoma imagine jamani hata ulaya hawafanyi hivi wanasystem ya kuhakikisha kwamba watakufuatilia
   
Loading...