Mama mkwe kajichimbia naona shida kumtoa

Nasema tena, tumezaliwa katika familia tofauti, tunakutana na watu wenye hulka tofauti. Huenda labda hujaingia kwenye ndoa na hujapata experience ya upande wa pili. Ndoa ni "takatifu" lakini ina changamoto nyingi, na moja ya hizo ni kuweza kuishi na watu wa upande wa pili kama ndugu zako wa damu.
Niko kwenye ndoa mkuu na ndugu wapo naishi nao, ila mama mkwe kuhamia tu kwangu bila sababu............
 
Habari za hapa watu wa jukwaa hili

Nimeona nifike hapa niandike duku duku langu

Mama mkwe amekuja home kwa ajili ya kumsaidia mwane ambae mimi ndio barafu ya moyo wangu (my wife) ulezi mtoto ambe tumepata hivi karibuni, lengo kwa mujib wa wife ni kutusaidia ulezi hadi pale mtoto atakapojiweza au kwa sharti la kama tungepata mlezi basi pia angeodoka.

Lakini wadau hivi naandika muda umeenda sana na hana mpango wa kuchomoka tuko naye pika pakua na sasa mpaka anadai room yake.

nataka nijarib kuongea na wife mkwe ataondoka lini lakini naogopa kuja kusema namfukuza mamake au simpend mkwe wangu. kwaio hili jambo laninyima raha na uhuru pale ndani na ukweli naumia sn ata ku-enjoy na wife.

Nilikuwa na tabia nikishaingia ndani nakuwa navaaga vingua vifupi vifupi kama pensi na wakati mwengine tumbo wazi kwa ajili ya upepo upepo lakin sasa nikijarb tu mkwe huyo uso kwa uso sina amani najisikia aibu sana inabidi muda wote nikiwa ndani niwe full-aquip.

Tumepanga tulete mlezi wa mtoto na wife lakini wife na yeye anasema ata mlezi akija na mama yake ataendelea kuwepo.

Huyu mama tayari ni age kidogo na hana mume kama vile maisha yake anataka yawe pale kwangu.

Wadau naomba ushauri kwa kweli
Kama una uwezo kaa nae nakama mama mkwe hana maneno maneno mwache akae na mwanao wafanyakazi wa ndani siku hizi kumwachia mtoto ni sawa na kuweka roho hewani
 
Ni baraka kuwa na wazazi na ni jambo jema kama mume wake hayupo ,ukaweza kumlea wewe.Tuwapende na kuwasaidia wazazi wetu tutapata baraka na mafanikio
 
Habari za hapa watu wa jukwaa hili

Nimeona nifike hapa niandike duku duku langu

Mama mkwe amekuja home kwa ajili ya kumsaidia mwane ambae mimi ndio barafu ya moyo wangu (my wife) ulezi mtoto ambe tumepata hivi karibuni, lengo kwa mujib wa wife ni kutusaidia ulezi hadi pale mtoto atakapojiweza au kwa sharti la kama tungepata mlezi basi pia angeodoka.

Lakini wadau hivi naandika muda umeenda sana na hana mpango wa kuchomoka tuko naye pika pakua na sasa mpaka anadai room yake.

nataka nijarib kuongea na wife mkwe ataondoka lini lakini naogopa kuja kusema namfukuza mamake au simpend mkwe wangu. kwaio hili jambo laninyima raha na uhuru pale ndani na ukweli naumia sn ata ku-enjoy na wife.

Nilikuwa na tabia nikishaingia ndani nakuwa navaaga vingua vifupi vifupi kama pensi na wakati mwengine tumbo wazi kwa ajili ya upepo upepo lakin sasa nikijarb tu mkwe huyo uso kwa uso sina amani najisikia aibu sana inabidi muda wote nikiwa ndani niwe full-aquip.

Tumepanga tulete mlezi wa mtoto na wife lakini wife na yeye anasema ata mlezi akija na mama yake ataendelea kuwepo.

Huyu mama tayari ni age kidogo na hana mume kama vile maisha yake anataka yawe pale kwangu.

Wadau naomba ushauri kwa kweli
STAREHE ZIPO NA SHIDA ZIPO,LAKINI MAMA MKWE KUENDELEA KUWEPO HAPO KWAKO NI ISHARA YA KWAMBA HUDUMA UNAZOZITOA NI NZURI NA BORA HATA HUKU AISHIPO HAZIPATI ,HONGERA KWA HILO...KILA LENYE KHERI NAWE LITAKUUDHI SANA HAPA DUNIANI,MREJEE MOLA WAKO KISHA KUWA MTU WA IBADA MUOMBE ALLAH AKUJAALIE SUBRA ILI USIWE MWENYE KUCHUKIA UMUONAPO MAMA MKWE WAKO..JITAHIDI KUONESHA HUNA TATIZO JUU YA UWEPO WAKE HAPO KWAKO HILO LITAMFANYA AWE HURU SANA AWAPO HAPO ..KWA HALI YEYOTE ILE ULOKUWA NAYO JITAHIDI MPATIE MARADHI KWA KADRI YA UWEZO WAKO..MAMA MKWE NI MAMA YAKO JITAHIDI KUCHEKA NA KUFURAHI HATA KAMA UNAUMIA KIASI GANI ,HUENDA RIZIKI UNAYOIPATA HUKU KATIKA PIRIKA ZAKO NI MATOKEO PIA YA UWEPO WA HUYO MAMA HAPO...MKIRIMU MGENI KUNA FADHILA KUBWA SANA MBELE ZA ALLAH....
 
Mimi mkewangu alijifungua mtoto akiwa na ugonjwa wa njano, ikabidi mtoto alazwe wiki mbili bugando hosptl, hela nikaishiwa nikabaki kukopa tu,baada ya kutoka hospitali mkewangu akanambia mama yake anatoka mkoani kuja kutusalimia,nikamzuia amwambie hasije kwasababu hatujakaa sawa bado tuna madeni pia yeye akija inamaana kuna ghalama kama za kumrudisha na mengineyo, wanawake majasiri sana nilishangaa baada ya siku tatu niko kazini, wife ananipigia kuwa mkwe ndo ashaingia ndani lol! nilisikia hasira si za nchi hii, baada ya kurudi home nakusalimia nilichukua baadhi ya nguo zangu muhimu nikaaga nina safari kikazi maana nimepanga chumba na sebuli,swali alfajiri muda wa job ningepishana vipi na mamakwe sebleni? baada ya kusepa nikabana kwa rafiki yangu siku ya nne wife akanipigia eti mamamkwe anaomba nauli elfu hamsini arudi bush nikakopa nikamtumia akaondoka, sasa wakubwa ambao tayari mna familia naomba mnisaidie je nilikosea kwa maamuzi haya? maana naona aibu sitokuja kwenda kwao mke wangu sababu ya upuuzi aliosababisha yeye.
 
Mi mwenyewe siezi afiki mama angu kukaa naye ndani miaka nenda rudi bila sababu na akati ana kwake, akiwa na shida ntamchukua ata miaka yote, lakin mzima ivi ahamie kwangu wanagusana matako na mkwe koridoni kisa nini
Haha adui wa mwanamke na mwanamke mwenzie duh
 
Iko poa kusepa. Acha wewe kuna jamaa alipo funga harusi tu mamkwe alitinga akawa haondoki na nyumba ya kupanga chumba kimoja. Jamaa akawa anachungulia tu kwenye blanketi. Akaona isiwe shida akasubiri bafuni wanapooga wote asubui. Dem kagoma kutoa mzigo ikawa vurugu wapangaji wakastuka kulikoni.
Wakubwa walipofatilia mamkwe alishauriwa asepe.
 
Ulipokuwa na shida hukuona kama unabanwa, shida imeisha ndio unamuona mzigo!! Angekuwa mama yako ungefanyaje?
Jibu hilo swali then majibu yake ndio hatua za kuchukua ktk hali kama hiyo.
 
Nikuambie kitu mkuu, huyo mama amekuja kusaidia uzazi, unatakiwa kwanza ushukuru kwa msaada aliofanya. Najua wakati mwingine hizi nyumba zetu inakuwa ngumu kuwa na idadi kubwa ya watu coz space yaweza kuwa ndogo na uhuru wako pia.

Lakini likija swala la wazazi (iwe wa upande wako au wa mkeo), jaribu sana kuishi nao kama wa kwako, ukiweka matabaka namna hiyo hata siku akija mama mzazi mkeo anaweza kusema siwezi kuishi na mama yako.

Hawa ni wazazi wetu, baadhi hawapendi kabisa kukaa kwa watoto mda mrefu(wanajua madhara yake), wale ambao hawaelewi basi twende nao hivyo tu.
Kwa ninavyofahamu wamama wa upande wa mke huwa hawapendi kukaa kwa wakwe zao kabisa. Yawezekana mama anaona kuwa msaada aloitiwa autoe bado anahitajika autoe. Hawajaonyesha kutokuhitaji msaada wake tena. Na kama ni uzao wa kwanza ndio kabisaaaa!!!!
 
Huu sasa mtego. Usipokaa vizuri laana ushaipata. Jichunguze, ni nini haswa kinakukera. Uhuru wa kukaa tumbo wazi au uso wa mama mkwe ndo unakukera?? Ninavyojua, kwangu sioni shida yake kukaa hapo kama ukiweza kumdhibiti mapema. Kama ulikuwa unakaa kifua wazi na mkeo hata kwa mamako ungeweza kukaa hivyo. Iweje uone soni kwa mkwe??
Swali, Je, mkeo ndo mtoto pekee kwao? Ka jibu ni hapana, kwa nini ang'anganie kwao?
 
Hiii kitu inahitaji busara sana kuifanyia maamuzi. Kitendo cha kuishi bila mume inafanya mtu awe mpweke sana, just fanya kama kumsitili asije pata mashughuliko ya moyon kuishi peke yake sana.

Hapo kubwa ni kutafuta namna ya kuwa huru na kupata time ya kujiachia.

Nakumbuka wamama wa zamani, mkwe akiingia tu, utakuta yeye anajiongeza anaendelea na shughuli zake, anakuachia uhuru.

Kama imekufika moyon kabisa humtaki, tafuta rafiki yake mwenye busara, atengeze mazingira ataondoka tu.
 
Tafuta shoga ake unayejua kidogo ako smart na mambo yake, na kwake hayajitokezi kama ayo aongee naye, kama mama hana shida na ana kwake, na ule usaidizi umetosha aondoke arudi awaache huru
Ushauri mzuri. namshauri asikilize sauti hii
 
Hiii kitu inahitaji busara sana kuifanyia maamuzi. Kitendo cha kuishi bila mume inafanya mtu awe mpweke sana, just fanya kama kumsitili asije pata mashughuliko ya moyon kuishi peke yake sana.

Hapo kubwa ni kutafuta namna ya kuwa huru na kupata time ya kujiachia.

Nakumbuka wamama wa zamani, mkwe akiingia tu, utakuta yeye anajiongeza anaendelea na shughuli zake, anakuachia uhuru.

Kama imekufika moyon kabisa humtaki, tafuta rafiki yake mwenye busara, atengeze mazingira ataondoka tu.
Naonaga mama angu akija kunisalimia analala mara mbili siku ya tatu anondoka zake, kwanza mkwe akija ye anakaa chumbani hukooo na wajukuu zake,
 
Yaani hapa comenti zote nilizosoma nazidi kusukwa sukwa tu akili kama chombo kilichopoteza uelekeo majini.
 
familia zetu hizi shida tupu
ndo mana hata unakuta romantic moments ndani ya ndoa zinapungua
mara mama mkwe mara shemeji sa ngapi mtu utampiga busu mpenzi sebleni?
watu macho juujuu na masikio yamewasimama kama andazi la nazi
ndoa inapaswa kuwa mke mume na watoto
Hao wengine waje then wasepe asa watu wanahamia kabisa jamani
Inakera
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom