Mama mkwe huyu anaweza kuharibu ndoa ya Mwanawe wa kike. Suluhisho ni nini?

ushauri mkuu, hata kidogo tu, baada ya wiki hii nasafiri nakwenda kwake kumshauri hili suala ili kulinda ndoa yake.
Kama uwezo anao,amtafutie sehemu nyingine mama mkwe(Ampangishie sehemu nyingine) ,wajukuu na ampatie mfanyakazi wa ndani ili aokoe ndoa yake.
 
Kama uwezo anao,amtafutie sehemu nyingine mama mkwe(Ampangishie sehemu nyingine) ,wajukuu na ampatie mfanyakazi wa ndani ili aokoe ndoa yake.
mama mkwe ana mji wake kwa taarifa rasmi , nyumba kubwa tu, yani ye kaamua tu kukaa kwa mwanae, ushauri hapo, huko awali kuna mtu kaja dm anasema nimshauri jamaa amle mama mkwe na hao wajukuu, nawaza nisije shauri vibaya.
 
mama mkwe ana mji wake kwa taarifa rasmi , nyumba kubwa tu, yani ye kaamua tu kukaa kwa mwanae, ushauri hapo, huko awali kuna mtu kaja dm anasema nimshauri jamaa amle mama mkwe na hao wajukuu, nawaza nisije shauri vibaya.

Basi wao wahame wamuachie MJI kunusuru ndoa.
 
Cha muhimu na wewe pia mlete mama yako na ndugu wengine kama 3 au 4 wakae kama mwezi hivi,wenyewe wataondoka tu,na mama mkwe akileta za kuleta uwaombe waondoke wote,ndugu wa upande wa mke na wako,ila kabla hujafanya hvyo mweleze azma hiyo mamako
 
Kama kweli tatizo ni kitanda kupiga kelele wakati wa kujamiiana, akitengeneze au nunua kitanda imara.

Afike nyumbani kwa bashasha, aanze rom na mkewe sebuleni, amfate jikoni, yaani mahaba km yote wakati wowote. Aishi maisha yake na afanye wajibu wake.
 
Kuna mtu kanipa kisanga hapa nimeona niwashirikishe ili nimshauri.

Kijana anaishi Mbeya kabila Msangu kaoa mwanamke Mnyakyusa.

Baada tu ya kuoa mama wa binti akahamia kwa kijana (mkwe wake] na kuacha familia yake huko Uyole.

Baada ya miezi 6 mama mkwe akaleta wajukuu zake wanne pale kwenye ndoa mpya [ndoa ya binti yake] na hawa watoto ni wanafunzi wanasoma shule ya bweni hivyo wakifunga wanafikia hapo.

Hii familia ni ya kilokole na hata mkwe ni mlokole. Kwa sasa familia hii imekuwa na watu 7, yaani Mume, mke, mama mkwe na wajukuu wa mama mkwe wanne.

Kijana wa kiume anasema hapati muda wa mapenzi na mkewe kwakuwa mke muda wote anakaa na mama yake mzazi sebuleni. Mama mkwe ndiye anaamua cha kupikwa, muda wa kusali, nyumba ikae vipi na mambo mengine kama hayo.

Mume kasusa tendo la ndoa maana kitanda kinapiga kelele na kipo karibu na sebule ambapo watoto wanakuwa wanaangalia TV.

Mke wa huyu rafiki yangu hajui kama ameolewa na mbaya zaidi ni wale watoto wameolewa kutokea nyumbani, hawajawahi kukaa gheto, yaani kahamishia familia yake yote hapo kwa mume.

Je, nimshauri awe anafanya mapenzi na mkewe hata kama mama mkwe yupo sebuleni na anasikia miguno ya utamu?

Huyu kijana ananiambia ukimuona mtu saa moja asubuhi yupo BAA anakunywa Pilisner baridi au ukiona mtu ananunua madada-poa muombee, hajapenda ila shida za kijinga kama hizi ndizo zinaleta stress.

Naombeni ushauri ili na mimi nimpe, JE, amchane laivu mama mkwe kwamba hamtaki ama amwambie mkewe kwamba nyumba ni ya wawili na siyo familia kubwa?
Aende akawaone viongozi wa kanisa anakosali mama mkwe. Watamuita waongee naye .
 
Ila kuna familia zenye changamoto jamani
Mama mkwe huumwi wala huna shida yoyote unaacha mji wako unahamia kwa mtoto wako pamoja na wajukuu???
Mbaya zaidi unageuka mama mwenye nyumba heheee!!!!

Tunapenda wazazi wetu ila ifike mahali tuwaeleze ukweli unaouma watusaidie kuondokana na hizi aibu.....familia zinahitaji privacy na uhuru, mambo ya kuwa mtumwa ndani ya nyumba yako mwenyewe hapana kwa kweli!!!!

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa si inabidi ukite mdundo kwanguvu lengo mama mkwe ajue hakupaswa kukaa hapo?

Pole mdau hizi ndiyo familia zetu za kiafrika ukioa au kuolewa na mtu toka familia maskini. Au ukikutana na mkwe mzurulaji au mpenda vizuri kuliko uwezo wake.

Sema kwenye kula unakubalije upangiwe wakati wewe ndiyo mwenye nyumba?

Kuhusu kujaza ndugu hilo mueleze ukweli tu mkeo.
Kususa ni kwasababu chumba cha wanandoa kipo pua na mdomo na sebule, waki-kitana miguno inaikika sebuleni.
 
Watu ambao hawana misimamo wanaendeshwa sana

Mimi huwa sivumilii ujinga yaani sinaga simile na upuuzi

Nawawaisha fasts tu yaani timua timua wote wapotele mbali

Mke nae akizingua natimua

Kila mtu na kila kitu kikae mahali pake sahihi
 
Waendelee na tendo. Mama mkwe anajua kinachomuweka mwanae hapo. Hata nyumba nzima wakisikia kinachoendelea pengine ndio watajiuliza kwa nini wapo hapo?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom