Mama mkwe huyu anaweza kuharibu ndoa ya Mwanawe wa kike. Suluhisho ni nini?

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Feb 20, 2016
14,042
20,403
Kuna mtu kanipa kisanga hapa nimeona niwashirikishe ili nimshauri. Kijana anaishi Mbeya kabila Msangu kaoa mwanamke Mnyakyusa. Baada tu ya kuoa mama wa binti akahamia kwa kijana (mkwe wake] na kuacha familia yake huko Uyole.

Baada ya miezi 6 mama mkwe akaleta wajukuu zake wanne pale kwenye ndoa mpya [ndoa ya binti yake] na hawa watoto ni wanafunzi wanasoma shule ya bweni hivyo wakifunga wanafikia hapo.

Hii familia ni ya kilokole na hata mkwe ni mlokole. Kwa sasa familia hii imekuwa na watu 7, yaani Mume, mke, mama mkwe na wajukuu wa mama mkwe wanne.

Kijana wa kiume anasema hapati muda wa mapenzi na mkewe kwakuwa mke muda wote anakaa na mama yake mzazi sebuleni. Mama mkwe ndiye anaamua cha kupikwa, muda wa kusali, nyumba ikae vipi na mambo mengine kama hayo.

Mume kasusa tendo la ndoa maana kitanda kinapiga kelele na kipo karibu na sebule ambapo watoto wanakuwa wanaangalia TV.

Mke wa huyu rafiki yangu hajui kama ameolewa na mbaya zaidi ni wale watoto wameolewa kutokea nyumbani, hawajawahi kukaa gheto, yaani kahamishia familia yake yote hapo kwa mume.

Je, nimshauri awe anafanya mapenzi na mkewe hata kama mama mkwe yupo sebuleni na anasikia miguno ya utamu?

Huyu kijana ananiambia ukimuona mtu saa moja asubuhi yupo BAA anakunywa Pilisner baridi au ukiona mtu ananunua madada-poa muombee, hajapenda ila shida za kijinga kama hizi ndizo zinaleta stress.

Naombeni ushauri ili na mimi nimpe, JE, amchane laivu mama mkwe kwamba hamtaki ama amwambie mkewe kwamba nyumba ni ya wawili na siyo familia kubwa?
 
Mie nafukuza wote mbwa hao. Yani nyumba yangu iendeshwe na mama mkwe?

Ntachomwambia mke ni kuwa nimekuoa wewe sasa sielewi hawa watu unaonijazia hapa ni wa kazi gani?

Akianza oh mamaangu sijui blah blah...ntamuuliza tu kwani alikuwa akiishi wapi kabla sijakuoa?! Kama mamaako ndio kakuoa basi wacha mie nikaoe mwanamke mwingine na nikija nae hapa muhakikishe mnafungasha mapema tu.
 
Yaani uoe alafu ushauri ufate humu ,aisee ndoa za digitali
ila hilo sio tatizo,Mwambie MAMA MKWE NI KAMA MAMAAKE Tu..
Akae aongee nae,nina imani atamuelewa..
Asante kwa ushauri, mimi nachukua ushauri humu maana kuna wasomi, wanafunzi washafungua chuo ndio maana unaona huku kila mtu anamwaga pointi tupu.
 
Chakufanya asubiri ule muda wa dinner kila mtu yupo mezani, achokonoe TV isiwe inafanya kazi muda huo (kuwe kimya) then amuite mke wake chumbani amgegede kwa hasira ili wote wasikie. Kama kufikia jioni next day bado watakuwepo basi hao watakua wameshindikana.
 
Hapo Kama Mimi ndio huyo mume nitachofanya ntampa mke wangu hela ya nauli za kuwatosha, mke wangu amwambie mama yake asepe na hao wajukuu zake bila mimi kuhusika Moja kwa moja. Hiyo kazi ikimshinda ntahusika moja kwa moja na ntatimua wote.
 
Hapo achague ama anataka kufanikiwa kimaisha au akosane na wakwe.

Ila watu wa Mbeya wanapenda ujamaa sana wa kuishi extended family.

Niliandika comment nzuri ila sijui imekuwaje nikashindwa kusend.

jaji mfawidhi nahisi hii ndoa ni yako😀
 
chakufanya asubiri ule mda wa dinner kila mtu yupo mezani, achokonoe tv isiwe inafanya kazi muda huo (kuwe kimya) then amuite mke wake chumbani amgegede kwa hasira ili wote wsikie. Kama kufikia jioni next day bado watakuwepo bas hao watakua wameshindikana.
Hakyanani huu ushauri ninampa, tena anywe alkasusu mujarab kwanza
 
👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👏🏽👍🏽
Mie nafukuza wote mbwa hao. Yani nyumba yangu iendeshwe na mama mkwe?

Ntachomwambia mke ni kuwa nimekuoa wewe sasa sielewi hawa watu unaonijazia hapa ni wa kazi gani?

Akianza oh mamaangu sijui blah blah...ntamuuliza tu kwani alikuwa akiishi wapi kabla sijakuoa?! Kama mamaako ndio kakuoa basi wacha mie nikaoe mwanamke mwingine na nikija nae hapa muhakikishe mnafungasha mapema tu.
 
Hapo achague ama anataka kufanikiwa kimaisha au akosane na wakwe.

Ila watu wa Mbeya wanapenda ujamaa sana wa kuishi extended family.

Niliandika comment nzuri ila sijui imekuwaje nikashindwa kusend.

jaji mf[B]awidhi nahisi hii ndoa ni yako😀[/B]
Naomba hiyo comment tafadhali, uliyoshindwa kutuma.

Ndoa ya rafiki yangu tulisoma naye na wote tukapata ajira Mahakamani mwanzoni mwa 2000 kwa sasa yeye ni msajili mahakama kuu ila kituo sitasema.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom