Mama mkwe anaumwa

Mama mkwe anaumwa

Satuuuu

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2015
Posts
1,849
Reaction score
1,994
*MAMA MKWE* [emoji101]

_Ilikuwa wakati wa mchana ambapo mume alirejea nyumbani akiwa na habari mbaya._

*MUME:* _Mpenzi, nimepigiwa simu: Mama hajisikii vizuri. Tunaweza kwenda kumnunulia baadhi ya mahitaji kwa ajili ya kumtembelea?_

`Tafadhali andika orodha ya mahitaji kisha tuondoke.```

*MKE:* _Orodha ya vitu hivyo sio muhimu, tutanunua tu kabichi 2 na lita 2 za mafuta ya kupikia._

*MUME:* _Vitatosha kweli?_

*MKE:* _Ndiyo mpenzi, hakuna haja ya kupoteza pesa, vitatosha._

```Walielekea mjini na kununua kabichi 2 na lita 2 za mafuta ya kupikia. Wakati wakinunua mume alimuuliza mkewe tena kama vitu hivyo vingetosha.```

_Mke alisisitiza zaidi kuwa hawatakiwi kutumia pesa nyingi kwenye ziara ya kushtukiza._

```Walianza safari kuelekea kijijini, na walipofika kwenye eneo la njia panda yenye barabara zinazoelekea vijiji mbalimbali, mume alikata kona kuelekea kwao na mke.```

*MKE:* _(Kwa mshituko) tunaelekea wapi mpenzi? Nilidhani tunaenda kumtembelea mama yako._

*MUME:* _Ndiyo, ndiko tunakuelekea. Ni mama yako (mama yetu) ndiye anayeumwa._

*MKE:* _(kwa mshituko na kilio), lakini mahitaji haya hayatoshi. Turudi tuongeze vitu vingine._

*MUME:* _Hapana! Nilikuuliza tena na tena kama mahitaji hayo yanatosha, ukaniambia “NDIYO”. Hakuna kurudi….._

```FUNZO:```

```Wafanyie wenzako kile unachotaka ufanyiwe!!```

*UBAGUZI NI HATARI ( MPENDE MWENZAKO KAMA NAFSI YAKO) huu no mfano mojawapo tu. Mwanamke kama huyu hawezi kubagua watoto wake na wa wenzake( ndugu) katika kulea???
 
Ilikuwa zamani hiyo

Siku hizi najificha then natuma Mpesa mwenyewe

kila mmoja awe anajali wa kwake

kwani ni mama yangu yule?


Ndoa zenyewe za siku hizi ...


Bora ujali tu mama yako kwanza!!

sorry!!
Sasa mkuu mpaka ujifiche shida zote za nini ?
 
Sasa mkuu mpaka ujifiche shida zote za nini ?


Hapo nilikuwa nawapa mbinu hao wanaosumbuka na hayo makitu

ngoja nifike kwa ndoa. labda vitu ni tofauti na navyodhani

Ila mama ako ni mama ako hata kama mama mkwe huitwa mama pia
 
Ilikuwa zamani hiyo

Siku hizi najificha then natuma Mpesa mwenyewe

kila mmoja awe anajali wa kwake

kwani ni mama yangu yule?


Ndoa zenyewe za siku hizi ...


Bora ujali tu mama yako kwanza!!

sorry!!
ndio maana hatukupi like kama mambo yenyewe ndio haya
 
Halafu ulete na hiyo simu

mwenyewe anaitaka

usisahau kulog out jf

jana kaona hadi PM zako

sijui hukulog out
mwambie namalizia kifurush changu soon kinaisha ntarudisha... ahaa nlisahau aisee uzur hazina madhara zilikua za kukumbushana kusali tu.
 
ndio maana hatukupi like kama mambo yenyewe ndio haya

Yaani huwa nazitamani za mshana jr hivi zina raha?

Mie nazeekea jf sasa na sinazo hata za kutosha

Ntakuwa bibi bila hata like 500?

Hebu nipeni jamani, tena za kutosha,

Nipeni za kutosha na mimi ntawapa nanilii, ile naniliu nini ile?

Ile nyeusi inaitwaje?

Inaitwa like!!

Nipe nikupe!
 
Yaani huwa nazitamani za mshana jr hivi zina raha?

Mie nazeekea jf sasa na sinazo hata za kutosha

Ntakuwa bibi bila hata like 500?

Hebu nipeni jamani, tena za kutosha,

Nipeni za kutosha na mimi ntawapa nanilii, ile naniliu nini ile?

Ile nyeusi inaitwaje?

Inaitwa like!!

Nipe nikupe!
ha ha ha ha ha kumbe na wewe umeliona enhee,,
 
Ilikuwa zamani hiyo

Siku hizi najificha then natuma Mpesa mwenyewe

kila mmoja awe anajali wa kwake

kwani ni mama yangu yule?


Ndoa zenyewe za siku hizi ...


Bora ujali tu mama yako kwanza!!

sorry!!
Mkuu hela yako tena ya halwli bado ikutese?

Bora hata kila mtu aangalie upande wake kama mashaka ni mengi japo nayo matatizo
 
mwambie namalizia kifurush changu soon kinaisha ntarudisha... ahaa nlisahau aisee uzur hazina madhara zilikua za kukumbushana kusali tu.


Kaondoka amekasirika

naona anaenda kuchukua ile sufuria yako mpya aitie misumari

bora uje haraka!!
 
Ilikuwa zamani hiyo

Siku hizi najificha then natuma Mpesa mwenyewe

kila mmoja awe anajali wa kwake

kwani ni mama yangu yule?


Ndoa zenyewe za siku hizi ...


Bora ujali tu mama yako kwanza!!

sorry!!
una shida mpaka ujifiche...hauko huru hapo
 
Ndo hapo inapotakiwa kupata mwenza mwenye hofu ya Mungu.
 
Back
Top Bottom