Candid Scope
JF-Expert Member
- Nov 8, 2010
- 11,897
- 6,933
Matukio mengi yanayotokea siku hizi yanatia kichefuchefu zaidi ya kinyaa. Katika mizunguko yangu ya hivi karibuni katika shughuli zangu, nilifikia guest moja ya kawaida iliyokidhi kiwango ninachotaka, kwa vile napenda sehemu tulivu, isiyo na makelele wala walevi. Wahudumu wenye heshima zao na wanaowajali na kuwapa taadhima stahiki wateja.
Nilihitaji kupata soda, hivyo nikatoka chumbani na kumwomba mama mhudumu wa guest ile akaninunulie. Wakati namwagiza, ghafla niliona anashtuka alipoona kijana mmoja ambaye alipanga chumba karibu yangu akiingina na msichana mmoja aliyevalia nadhifu. Nikaona anaonyesha dalili ya kama kuchanganyikiwa, na yule msichana alipoingia alishtuka ghafla kabla hajaingia chumbani, akataka kurudi lakini kijana yule akamshika mkono na kumvutia ndani ya chumba.
Nilimwuliza mama mhudumu kwa nini anashtuka, akanijibu kuwa haamini anachoona maana yule msichana ni mke wa mtoto wake. Akataka kumfuata chumbani, akaenda kugonga mlango na hawakufungua, nikamshauri aachane nao kwani ni watu wazima hao. Hata hivyo mama wa watu hakuwa na amani ila tu akabaki kufuata ushauri wangu. Hawakukaa muda mrefu chumbani labda 30 minutes wakatoka.
Siku iliyofuata binamu yangu kaja kunichukua nikale lunch si mbali sana kutoka pale na ni mwendo wa dakika kumi hivi. Wakati akina mama wanaandaa msosi ndani, tukawa tumekaa nje tukipiga stori na kama block moja toka pale kulikuwa na nyumba nyingine ya wageni. Kufumba na kufumbua nikamwona kijana yule niliyemwona akina na msichana guest niliyofikia na kufumwa na mama mkwe wake akawa ameongozana na msichana yule wakaingia guest.
Amini hapa ninachoandika si hadithi za abunuwasi, ni kitu cha kushuhudia, movie hii ilinishangaza, na nilipomsimulia binamu yangu pale wakati tunaongea, akanitonya kwamba kijana yule wanamjua ni mtembeaji sana na wasichana wengi na anabadilisha kama kanga. Inaaminika ana biashara nzuri ya unga maana anaonekana ni mtanashati na mwenye mvuto sana. Zaidi aliyoniambia usalama wa kiafya wa kijana yule ilinishtua zaidi, maana pesa imekuwa urimbo kwa akina dada zetu, wake zetu, ndugu zetu, na yawapatayo si ajabu watatuambukiza tulio wapenzi wao, washikaji wao, waume zao, nk.
Kuna tatizo la self control, na kuruhusu silika na kuitii kila mwamko unapojitokeza dhahiri unakuwa mtumwa wa nature badala ya kuiitiisha nature.