Mama Mkwe Aleta Balaa, Ndoa Yavunjika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Mkwe Aleta Balaa, Ndoa Yavunjika

Discussion in 'Jokes/Utani + Udaku/Gossips' started by kilimasera, Jan 27, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Mwanamke mmoja wa nchini Italia amefungua kesi ya madai ya talaka mahakamani mwezi mmoja baada ya kuolewa kutokana na kitendo cha mumewe kumleta mama yake kwenye fungate (honeymoon) ya harusi yao.
  Kwa kawaida fungate(honeymoon) huwa ni muda wa farangha wa wanandoa kusherehekea harusi yao.

  Ndoa imevunjika nchini Italia baada ya mume kuamua kumleta mama yake kwenye honeymoon yao iliyofanyika mwishoni mwa mwezi disemba mwaka jana.

  Mwanaume huyo alimkasirisha mkewe siku mbili baada ya harusi yao wakati alipomleta mama yake kwenye uwanja wa ndege wa Fiumicino mjini Roma ili waende naye kwenye honeymoon yao nchini Ufaransa.

  Mkewe mwenye umri wa miaka 36 alipopinga mama mkwe wake kuambatana nao kwenye honeymoon yao, mwanaume huyo alipinga na kudai lazima waambatane na mama yake kwakuwa hali ya kiafya ya mama yake si nzuri.

  Mwanamke huyo kwa shingo upande alikubali kuambatana na mama mkwe wake na kutumia siku zote za honeymoon yao pamoja.

  Baada ya kurudi toka Ufaransa mwezi huu mwanamke huyo moja kwa moja aliomba talaka akidai kuwa kitendo cha mumewe kumleta mama yake kwenye honeymoon yao kimeonyesha kuwa ana hisia na ukaribu zaidi kwa mama yake.
   
 2. Babu Lao

  Babu Lao JF-Expert Member

  #2
  Jan 27, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 2,056
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 135
  Mmmmhhhh :twitch:
   
 3. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #3
  Jan 27, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Kama Babu lao angempata Mama Mkwe, kwa umri wake huo na huyo binti hapo kwenye picha basi nina imani kabisaaaaaaa, ANGELIKUWA KUKU NA YAI LAKE. teteteee.... :)
   
 4. senator

  senator JF-Expert Member

  #4
  Jan 27, 2011
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 1,927
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 133
  Huenda jamaa ni kitinda mimba bado anadeka au ndo wale walikuwa wakiitwa watoto wa mama..hawafanyi kitu bila mama!
   
 5. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #5
  Jan 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  hahaaa...................umeoa ila bado unadeka aisee hiyo hatari!
   
Loading...