Ushauri kwa Rais Samia, hata kabla afanye utaratibu wa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Tanzania Bara

mmaroroi

JF-Expert Member
May 8, 2008
4,631
2,248
Kwa heshima na unyenyekevu mkubwa ninao ushauri huu kwa Mh Rais wangu Samia Suluhu Hassan.

Ushauri wangu ni kuwa afanye utaratibu wa kisheria wa kuwepo kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa Tanzania Bara kama ilivyo kwa Tanzania Visiwani.

Faida yake ni kuwa itampunguzia upinzani ndani ya CCM na kuelekea 2025.

Pia itapunguza au kuondoa uhasama wa Utanganyika na Uzanzibar katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Hakika likifanyika hilo Mama Samia utakumbukwa daima na maendeleo ya Tanzania yatasonga mbele kimaendeleo kwa uhasama utapungua au kuisha.

Nalileta kwa Mama Samia mpendwa wetu kwa utekelezaji. Asante.
 
Chadema haitashirikiana na Wauaji
Chama chochote kitakachokuwa na sifa kinaingia kwenye ushirikiano huo. Kinaweza kuwa Chama kimoja cha upinzani au viwili au zaidi kutegemeana na utaratibu wa kisheria utakaowekwa. Hilo linaweza kufanyika hata kabla ya Katiba mpya. Litasaidia kujenga Umoja wa Kitaifa.
 
Serikali za Umoja wa kitaifa ni za kipuuzi na ni za manufaa kwa viongozi wa kisiasa tu kupata nafasi kutafuna keki ya taifa na watawala. Inatakiwa Serikali yenye Maono, nia thabiti na vitendo vya kuhakikisha kodi na rasilimali za nchi zinasimamiwa ipasavyo kuleta maendeleo ya wananchi pamoja na usalama wao, ikiwepo serikali ya namna hiyo wala hautoona wananchi wakijishughulisha sana na mambo ya siasa wala vyama vya siasa.
 
Jicho la pili si muhimu? Mnaweza pia kuweka utaratibu wa kuunda Serikali ndogo. Hata Bungeni panakuwepo uwiano fulani hivyo mambo ya ubadhirifu yatathibitiwa maana kama ni wa upande wako wameiba wa upande mwingine hawatavumilia.
 
Back
Top Bottom