Mama Maria: Kuilipa Dowans tatizo kubwa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Maria: Kuilipa Dowans tatizo kubwa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BAK, Jan 31, 2011.

 1. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #1
  Jan 31, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,550
  Likes Received: 81,990
  Trophy Points: 280
  Mama Maria: Kuilipa Dowans tatizo kubwa  * Ataka CCM, wanachama watafakari kabla ya kulipa

  Na Daud Magesa, Butiama

  Majira

  MJANE wa Hayati Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere ameibuka na kusema kulipa mabilioni ya fedha kwa kampuni ya
  Dowans ni sawa na kuwaingiza wananchi kwenye matatizo makubwa.

  Mama Nyerere amekitaka Chama Cha Mapinduzi (CCM) na wanachama wake wakae watafakari kwanza kabla ya kulipa fedha hizo, zinazokadiriwa kufikia sh. bilioni 94, kwa kuwa suala hilo litafanya CCM ama isiaminike, au wananchi waichukie.

  Aliitaka serikali kuwawajibisha wote wanaohusika na Dowans ili kurejesha maadili ya uongozi kama ilivyokuwa wakati wa mwalimu, badala ya kukurupuka kulipa sh. bilioni 94 bila kuangalia athari watakazopata wananchi.

  Mama Maria Nyerere alitoa kauli hiyo nyumbani kwake Mwitongo, Butiama, juzi, wakati akizungumza na Kamanda wa Umoja wa Vijana (UVCCM) Mkoa wa Mbeya, Bw. Mwakajumilo Isaac ambaye pia ni Mhasibu Mwandamizi wa Benki Kuu ya Tanzania (BoT), Tawi la Mbeya, waliomtembelea baada ya kuanguka hivi karibuni na kuumia wakati akielekea kanisani.

  Alisema kwamba jahazi hili (Tanzania) linaelekea kuzama kutokana na vurugu na mapigano ya wenyewe kwa wenyewe, na hivyo kuwataka Watanzania watambue kuwa, 'sote tutaangamia kutokana na athari za machafuko hayo'.

  Alisema kuwa baadhi ya viongozi na Watanzania wamepoteza maadili na hivyo kutoa kauli zinazoweza kuiingiza nchi kwenye machafuko kwa maslahi ysao binafsi, na kwa manufaa yao kisiasa.

  Baadhi ya kauli hizo, alisema ni zinazohusiana na mifarakano ya kidini, na nyingine kuhusu na suala la dowans , ambayo alikuwa anaifuatulia kwenye televisheni.

  Kuhusu mabadiliko ya katiba, Mama Nyerere alisema amekuwa akifuatilia mijadala mbalimbali kwenye runinga na kuona ulivyopamba moto, na hata kijijini kwake, Mwitongo, nako mjadala unaendelea.

  Alisema kwamba Watanzania waendelee kuwa watulivu na mijadala hiyo iendeshwe kwa kushirikisha wadau na viongozi kutoka makundi yote kwa haki na usawa, huku wakizingatia umoja, amani na utulivu wa taifa ili kuenzi mazuri yaliyoachwa na waasisi wa taifa hili kwa manufaa ya wote.

  Mjane huyo wa Baba wa Taifa alieleza kuwa viongozi mbalimbali, wananchi na wadau wote wawe watulivu huku wakiliombea taifa wakati mchakato wa katiba mpya ukisubiriwa
  kuanza.

  Akigeukia sera ya Kilimo Kwanza, aliwaeleza makada hao wa UV-CCM kwamba watu hawapendi tena kilimo, hasa vijana wenye nguvu ,wamekuwa wakikimbilia mijini kufanya biashara na kusababisha maeneo mengi ya vijijini kukabiliwa na tishio la njaa huku mabepari nao wakipigania kuondoa historia nzuri ya taifa.

  “Vijana wangu, hakuna mtu ambaye angependa kuwa maskini, lakini pia huwezi kuwa tajiri kwa njia za mkato, hasa kwa hawa watumishi wa umma, jambo kubwa ni viongozi kuzingatia na kufuata maadili kama ilivyokuwa kwenye uongozi wa serikali ya awamu ya kwanza ya hayati Mwl Julius Nyerere kwa kuthubutu kuwaondoa wasiofaa na kuwataja hadharani,” alisema na kuongeza:

  “Serikali inapaswa iwaondoe wanaoiharibia, hata kama wanafahamiana. Pia ikihakikisha kauli za watu na wanasiasa zisizofaa kwa Watanzania, zenye lengo la kuhatarisha amani hazipewi nafasi na hatua kali zichukuliwe kwa wale wanaotoa kauli za uchochezi ili kuliangamiza jahazi la taifa letu lenye historia ya pekee na mfano kwa mataifa mengine”.

  Alitoa wito kwa viongozi wa serikali kuhakikisha misingi yote ya taifa iliyoasisiwa na viongozi waliotanguliwa wanaendelea kuilinda wakiweka mazingira mazuri kwa kuboresha huduma mbalimbali za kijamii hususani vijijini ambako utoaji wa huduma hauridhishi na hauna tija.

  Alisema uduni wa huduma hizo husababisha jamii kulalamikika kutokana na wananchi wengi wa kipato cha chini kukosa huduma za afya, maji, elimu, barabara, bei nzuri ya mazao na upatikanaji rahisi wa nishati ya umeme.

  Aliwaasa Watanzania kuacha kukubali kutumiwa na watu ambao malengo yao ni kujinufaisha kisiasa na kupata umaarufu ,huku wakiliacha taifa likiangamia kutokana na kutaka kuwagawa kwa kuzungumzia ukabila, udini na rangi vitu ambavyo wakati nchi ikipata uhuru Mwl. Nyerere na waasisi wengine walivipinga kwa nguvu zote, na hadi leo tu wamoja.
   
 2. G

  Gad ONEYA JF-Expert Member

  #2
  Jan 31, 2011
  Joined: Oct 26, 2010
  Messages: 2,641
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nadhani huyu mama yupo kwenye hallucination ya ccm iliyoundwa na mumewe Kambarage Nyerere, bahati mbaya things are not same as they used to be in those times. CCm ya sasa ni mpya, ccmpreneurs whose main objective is personal interest driven!
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Jan 31, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  Hawa jamaa hawamsikilizi hata huyu mama jamani!???
   
 4. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #4
  Jan 31, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,129
  Trophy Points: 280
  Hivi huyu mama anamiradi kama walivyo ma first lady waliomtangulia?......akina salma kikwete hadi kuifanya ikulu mradi wa familia, anna mkapa na mama siti mwinyi ni kufuru tupu kujichotea mihela ya taifa bila kujali na bila kuficha,./.......nauliza tena huyu mama maria nyerere amewahi kumiliki kitega uchumi gani?....au walikuwa washamba yeye pamoja na nyerere wake?
   
 5. Jile79

  Jile79 JF-Expert Member

  #5
  Jan 31, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 11,364
  Likes Received: 3,129
  Trophy Points: 280
  Kikwete anasubiri hata walioko makaburini pia waseme ndipo atachukua hatua za kujiuzulu?.................mbona walio hai na ambao wana elimu km yake wanayaona mambo ni wazi yanakwenda kombo tena kwa kiasi cha kutisha
   
 6. Ng'wanangwa

  Ng'wanangwa JF-Expert Member

  #6
  Jan 31, 2011
  Joined: Aug 28, 2010
  Messages: 10,180
  Likes Received: 895
  Trophy Points: 280

  Mwananchi wa Kwanza:
  Kwa nini serikali inashindwa kunibana nilipie ujenzi wa shule, leo nalazimishwa kulipa Dowans? Mbona Kikwere hawataji wamiliki wa Dowans? Amekaa kimya?

  Mwananchi wa Pili: Kwa nini serikali inaruhusu wageni kumiliki raslimali zetu na kutuacha sisi wananchi na njaa?

  Majibu kutoka kwa Stephene Wasira :

  anasema si busara kumhusisha Rais wake (Kikwete) na Dowans

  Akaendelea kusema (sijui nini nini....) Mara habari ikayeyuka na ITV wakatupeleka kwenye majibu ya kipimajoto.
   
 7. Juaangavu

  Juaangavu JF-Expert Member

  #7
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 3, 2009
  Messages: 915
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 35
  Haki uinua taifa, sina hakika kama hivi sasa tunakopelekwa na viongozi wetu ni mahali salama. Sina hakika kama viongozi wenyewe wanaelewa hali waliyonayo wapiga kura wao.

  Ukishindwa kumhusisha mwenyekiti wa baraza la mawaziri na maamuzi yaliyotolewa na vikao anavyovisimamia yeye kama m/kiti, kimantiki utakuwa hauna busara. Hivyo kutomhusisha mh JK na dowans, kwa maoni yangu naona busara itakuwa haijachukua mkondo wake labda kama tutaamua kuendekeza utaratibu wa Ndiyo mzee, bila kutafakari.
   
 8. Mpita Njia

  Mpita Njia JF-Expert Member

  #8
  Jan 31, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 7,012
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 145
  Kwani nani anamhusisha Kikwete na Dowans? Alipoamua kuingia humo si aliamua mwenyewe, kuna mtu alimlazimisha? Yeye mwenyewe ndo alichagua kujiingiza Dowans kwa hiari yake, hivyo awe tayari kukabili yote yatokanayo ya Dowans
   
 9. Smartboy

  Smartboy JF-Expert Member

  #9
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 12, 2010
  Messages: 1,110
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Futa kauli yako ya ushamba, huyu mama hana kitu anacho miliki zaidi ya nyumba anazokaa dar na butiama na nimewahi kumsikia akijieleza kwamba ikihitaji mahitaji muhimu anapewa na serikali huyu mama ni mwadilifu hata watoto wake ni watu wa kawaida tu.
   
 10. o

  olng'ojine Senior Member

  #10
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 119
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  majibu yenyewe ya Tyson ni ya ki-tyson tyson..porojo tupu.
   
 11. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #11
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,317
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  huyu wasira anajibu kwa style ya kumnyenyekea aliyempa uwaziri na kuwassahau wapiga kura wake wa bunda!
  hashangai kuona wananchi wa kawaida kama hao kumuuliza maswali hayo yanayofanana na kwa ujasiri mkubwa?
   
 12. kitungi

  kitungi Senior Member

  #12
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 3, 2010
  Messages: 134
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 35
 13. Japhari Shabani (RIP)

  Japhari Shabani (RIP) R I P

  #13
  Jan 31, 2011
  Joined: Jan 16, 2007
  Messages: 721
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Tumekua tukishuhudia na kwa kipindi kirefu mjandala kuhusu malipo ya kampuni ya kitapeli DOWaNS na misimamo ya watu mbalimbali wanasiasa,vyama vya kisiasa,viongozi wa serikali,wanaharakati wlalala hoi n.k.Wapo waliolipigia na kupigia kelele wizi huu wa mchana!wWapo wanaounga mkono wizi huu n.k.Kitu cha kushangaza ni ukimya na kigugumizi cha |JK kwa swala hili nyeti! Nini msimamo wake kuhusu swala hili?!Ukimya wake unatufanya tuamini ya kua DOWANS ni JK na JK Ndiyo dowans.Angalau athibitishe hili a akanushe ili atupe nafasi ya kujadili na kutafuta wa tatizo hili kwani kwa kuzingatia msimamo wake katika swala hili zima utatupa mwanya na wapi pa wa kuelekeza vilio vyetu.KWAKE- KAMA SI YEYE DOWANS-AU KWINGINE KAMA- YEYE NDIO DOWANS.MUNGU IBARIKI TANZANIA
   
 14. VoiceOfReason

  VoiceOfReason JF-Expert Member

  #14
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 4, 2010
  Messages: 5,234
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 0
 15. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #15
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,157
  Trophy Points: 280
  mkwere dowans ina muhusu na yeye ni mmoja wa wawamiliki wa kampuni hiyo.wanampango wa kutuibia pesa zetu na kutufanya sisi kua watumwa wao.
   
 16. m

  mzambia JF-Expert Member

  #16
  Jan 31, 2011
  Joined: Dec 31, 2010
  Messages: 885
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Jamani acheni kumsingizia baba mdogo ye hausiki ila wanaohusika ni rafiki zake wakubwa sana tena wa damu
   
 17. Arafat

  Arafat JF-Expert Member

  #17
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 17, 2009
  Messages: 2,582
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 0
  We advocate vipi?? Unataka Kikwete atoe matamko mara ngapi!! tayari ametoa matamko yeye kama Rais na pia kama M/kiti wa CCM au ufuatilii matukio.
   
 18. kweleakwelea

  kweleakwelea JF-Expert Member

  #18
  Jan 31, 2011
  Joined: Nov 29, 2010
  Messages: 2,421
  Likes Received: 435
  Trophy Points: 180
  kha sio mchezo.makali ya maisha yamefika hadi bara.
   
 19. newmzalendo

  newmzalendo JF-Expert Member

  #19
  Feb 1, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 1,359
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Dowans italipwa bilioni94,umeme wa mgao utaendelea mpaka july 2011,matumizi ya msingi yatapunguzwa serikalini e.g dawa za maleria ,vitabu mashuleni ,huduma kwa wazee,walemavu kukosa pesa kabisa
  Mashangingi i.e landcruisers V8 yatazidi kununuliwa,Safari za nje kutafuta wafadhili-wanunuzi wa rasilimali ,AKA wawekezaji kuongezeka
  Kiwango cha elimu kitazidi kushuka kwa kuwa mishahara ya walimu haitopanda na walimu kundelea kusoma ili kubadili career ,tayari walimu wengi wakishapata degree zao hawarudi kufundisha ktk shule walizotoka,hivyo tutakuwa na walimu wa short courses ,temporary without anycomitment to teaching as a career
  Bei ya mafuta itazidi kupanda,Gas yetu itauzwa soko la nje -kuibiwa juu kwa juu.
  Mh.J.K kazi yake itazidi kuwa ngumu,kwani mpaka sasa hajaweza kuteua wakuu wa mikoa,wilaya,wakurugenzi.
  Katiba haitojadiliwa Tena,itaundwa tume na hiyo tume itasimamiwa na watu wale wale.....
  Ahadi za CCM zitakuwa ngumu kutekeleza kwani watumishi wengi wa umma hawana moyo wala imani na viongozi walioteuliwa.

  Tutalikumbuka Azimio La Arusha,hasa kuhusu maadili ya uongozi,viongozi na familia zao.
  2015 CCM Kushika hatamu tena Raisi akiwa na Asilia ya Somalia-Iran
   
 20. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #20
  Feb 1, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,231
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Kuna sehemu sijaelewa utabiri wako vizuri....
   
Loading...