Mama Kilango apiga Kambi Moshi mjini; kumng'oa Ndesamburo?

We patachimbika hapo pamoja na kuisaidia Chadema na Moshi kiujumla! Huyo Mengi atabwagwa maana watu wa Moshi Mjini hawanunuliki kwa hela wamepinda! Muende muone msimamo wao haswa wa Moshi Mjini na hivi ndivyo kila mahali Tanzania kunatakiwa kuwa hivi Tarimerisation iwe kila mahali achukue time zake huyo Mengi, haka kazee kanafiki!
 
Mkulima, Ndesa hazungumziwi kwa sababu ni mbuge kutoka Chadema, bali ni kwa style yake ya kuwatumikia watu wake kwa hali na mali ikiwa ni pamoja na kujitolea kwake kwa watu wa Moshi.
Huyu hata angekuwa ni Mbunge kutoka CCM, nahakika hata watu wa Chadema wangemuunga mkono.
Wana JF hatuhitaji kupelekwa mirembe, apelekwe yuleyule aliyependekezwa na Tingatinga.

We patachimbika hapo pamoja na kuisaidia Chadema na Moshi kiujumla! Huyo Mengi atabwagwa maana watu wa Moshi Mjini hawanunuliki kwa hela wamepinda! Muende muone msimamo wao haswa wa Moshi Mjini na hivi ndivyo kila mahali Tanzania kunatakiwa kuwa hivi Tarimerisation iwe kila mahali achukue time zake huyo Mengi, haka kazee kanafiki!
 
Duuuuuuuh,

Kazi kweli kweli Me nadhani kabla ya mtu kuanzisha mashambulizi iwe ni ccm,chadema,cuf, etc ni budi wwajumbe wa chama hicho wakae na wajadiliane ili wajue ni jinsi gani ya kwenda kushambulia, usije ukapata aibu baadae, Maaan akuna majibo mengine ni wananchi wanamtaka mgombea fulani na atapita kwa ridhaaa yao, ivi watakaka kuniambia Slaa nandesamburo ni kwamba wana chadema tu ndio inao wapigia kura??? hilo me kwangu haliingii akilini na uhakika wana CCM, CUF na wengine wanawapigia kura hao jamaaa Slaa na ndesamburo, sasa ni bora kutizama nyuma nini mapungufu yenu kwa wapiga kura wenu waki mwaenda kombo wananchi wenu wanataka nini na nani wanamtaka? msiwalazimishia wagombea wasio kubalika jamani.

Sasa hii ya kilango kwenda Moshi kwa mashambulizi hayo kweli ameroba step hapo akajipange twahitaji siasa zenye mwelekeo na sio porojo jamani yeye kama yeye hakuna tatizo ila hao waliomshauri kwenda pale wanatelekeza na kuupoteza umaarufu wake. CCM mjipange upya na msafisheni makosa yenu, jengeni imani kwa wananchi wenu kwanza na ndipo mwingie vitani
 
Nani kamtuma huyu Mama au ametumwa na hisia zake? Kama katumwa na CCM, basi naona ccm imemchoka na inataka ajimalize mwenyewe.
Namshauri arudi jimboni mwake. Aachane na majimbo ya watu, ataumbuka bure, na sidhani kama anaweza kukaa moshi kwa muda huo wote aliosema, ataoroka tu kwanza usiku.
 
Ina maana Mpare anaweza kuwa tayari kumuuza hata mumewe ili ashinde kesi?

Mama Simba, changamkia tenda hiyo, Mgogo John itabidi auzwe, Mpare ashinde kesi ..... hahaaaa Shemeji zangu Wapare.

Utani wa ngumi huu sasa!!
 
Nani kamtuma huyu Mama au ametumwa na hisia zake? Kama katumwa na CCM, basi naona ccm imemchoka na inataka ajimalize mwenyewe.
Namshauri arudi jimboni mwake. Aachane na majimbo ya watu, ataumbuka bure, na sidhani kama anaweza kukaa moshi kwa muda huo wote aliosema, ataoroka tu kwanza usiku.

Nahisi CCM ndio waliomtuma ili ajimalize taratiiiibu na awaache mafisadi bungeni wakipeta, au....hii nafikiri ni kiwewe baada ya kuumbuliwa na Sophia msema hovyo, mwisho naona kama vile kakosea mlango kaingia choo cha kiume vile!
 
Mwe,Mwe,Mwe...Mama kawachokoza wachagga na Chadema yao,angepiga kambi Monduli angesifiwa kuwa ni kamanda wa makamanda lakini kwa sababu ni moshi kwa Chadema mama atatukanwa leo..mwe..mpaka Tanzania Daima gazeti la Chadema limemwandika mama.Tuliambiwa anataka kuja Kyela vilevile tunamkaribisha,nondo za mama SS zitammaliza.Kama ndoa iliendeshwa na pesa za kifisadi kwahiyo hiyo ni ndoa ya kifisadi..mweeeeeeeeeeee.
Mkuu IMBOGAMBOFU, Hapo chini mama alisema hivi...
nimeongea na Ndesamburo ananiambia wanaompa ubunge ni wanaCCM wenyewe hili halikubaliki.
Read btn the lines
 
Hapa shangazi yangu Anne kaniangusha kwa kweli,Labda niambiwe kwamba hapo mwakani Mzee Ndesa hana mpango wa kugombea, lakini kwa jinsi ninavyolifahamu jimbo la Moshi kumuondoa Ndesa ni ngumu zaidi ya kuuhamisha Mlima Kilimanjaro, asikiaye na afahamu.
 
We patachimbika hapo pamoja na kuisaidia Chadema na Moshi kiujumla! Huyo Mengi atabwagwa maana watu wa Moshi Mjini hawanunuliki kwa hela wamepinda! Muende muone msimamo wao haswa wa Moshi Mjini na hivi ndivyo kila mahali Tanzania kunatakiwa kuwa hivi Tarimerisation iwe kila mahali achukue time zake huyo Mengi, haka kazee kanafiki!

Hii nimeipenda
Tarime iko juu kisiasa hawanunuliki wala hawana bei.
 
CHADEMA wakiguswa JF huwa pananoga! This is like chickens coming home to roost.

Huyu mama leo atatukanwa matusi yale yale ambayo mama Simba alipoyatamka, wengi tu hapa JF walikubaliana huyo mama akapimwe Mirembe.

Sijui na sisi wana JF tukapimwe Mirembe pia?

Mkulima
Ha ha ha!Imekugusa eee kuwa mvumilivu mamabo ndio yalivyo.Ukiona hivyo uje CHADEMA chama cha wajanja wanojua kutetea chama chao kwa udi na uvumba.Kama sisiem wamejaa vilaza je hata kutumia kompyuta hawajui ,watajibu saa ngapi hoja?
 
MOSHI MJINI:

..Moshi Mjini wana Hospitali ya Rufaa KCMC.

..Moshi Mjini wana Chuo Kikuu cha Utabibu, Chuo Kikuu cha Ushirika,na Chuo cha Ufundi.

..Moshi Mjini wana barabara za lami toka Uhuru.

..Moshi Mjini wanapata maji ya bomba.

SAME MASHARIKI:

..sina uhakika kama Same Mashariki kuna hospitali yenye hadhi ya hospitali ya wilaya.

..hawana barabara ya lami. Kikwete aliwaahidi lakini mpaka leo hakuna kilichofanyika.

..Same Mashariki ni jimbo la mwisho kimaendeleo ktk mkoa wa Kilimanjaro.

..majuzi mvua zilileta maafa ambako wananchi 25 walipoteza maisha.

..hali ya maisha haijarudi kuwa ya kawaida kwa waathirika wa maafa ya mvua Same Mashariki.

KATIKA MAZINGIRA KAMA HAYA KWANINI ANNA KILANGO ANAKWENDA KUPIGA KAMBI MOSHI MJINI?

WANANCHI WA SAME MASHARIKI HATA HAWAJAANUA MATANGA YA VIFO VYA WALE WAHANGA 25, HALAFU MBUNGE WAO TAYARI 'KIGUU NA NJIA' KWENDA KUPIGA KAMPENI ZA SIASA?
 
MOSHI MJINI:

..Moshi Mjini wana Hospitali ya Rufaa KCMC.

..Moshi Mjini wana Chuo Kikuu cha Utabibu, Chuo Kikuu cha Ushirika,na Chuo cha Ufundi.

..Moshi Mjini wana barabara za lami toka Uhuru.

..Moshi Mjini wanapata maji ya bomba.

SAME MASHARIKI:

..sina uhakika kama Same Mashariki kuna hospitali yenye hadhi ya hospitali ya wilaya.

QUOTE]

Ipo bana! Inaitwa Bombo Hospital..
 
AmaniGK,

..Hospitali ya Bombo si iko Tanga?

..hata hivyo Same Mashariki ni choka mbaya kulinganisha na majimbo mengine ya Kilimanjaro.

..pia waliahidiwa barabara na JK lakini hakuna kilichofanyika.

..sasa hivi kuna maafa yametokea Same Mashariki ambapo wananchi 25 wamefariki. it is not even a month since that happened.

..sioni busara ya Mbunge wa Same Mashariki kwenda kufanya kampeni dhidi ya Mbunge wa Moshi Mjini.

..ningemuelewa Mama Kilango kama angekuwa Moshi Mjini kutafuta misaada kwa ajili ya wananchi wake waliothirika na maafa ya mvua.
 
Mkuu Joka Kuu hayo majina yanafanana tu ila kwenye jimbo la mama Kilango ipo nyingine yenye jina kama hilo ambayo inamilikiwa na Walutheri.
Hata hivyo niko pamoja nawe, Mama Kilango hana budi kuangalia hilo jimbo lake na kuachana na hayo mawazo ya kuweka kambi huko Moshi.Hilo jimbo la Moshi watu wameshafunguka macho,hawadanganyiki tena na Vipande vya kanga na madebe ya pilau, wao wanataka vitendo na maadam Mzee Ndesa ameshawaonesha kuwa anaweza kuwafanyia hayo ambayo CCM imeshindwa kwenye majimbo mengine,basi wala CCM wasihangaike watapoteza nguvu na hela zao bure tu!
 
Utabiri wangu unatimia nilisha wakana hawa wanao jiita wapambanaji siku nyingi . Wapambanaji wanawaza sawa na Mwenuyekiti wao wanadhani CCM kwanza then Tanzania na Watanzania . Ni aibu hii . Nakupengeza FMES kwa comments zako najua uko karibu na Mama utampa ukweli kama ulivuyo andika .Mama anaiwafanyia watanzanai ufisadi wa hali ya juu na anaongoza sanaa sasa .
 
huyu mama anatakiwa awe strategic, ajue nini anachokitaka, soon she will starts loosing direction, nimekaa moshi kidogo, watu wanampenda ndesa, sasa yeye amevimba kichwa kwa kusifiwa anaenda kufanya kazi isiyo na ija kwa taifa ( in long run) maana hatomaye ni watu wa moshi watakaohamua ni nani wanamtaka, i can say kilango is getting out of her self
 
Huyu mama hadi kufikia hapo means kapoteza mwelekeo kabisaaaaaaaaaaa kama huamini endelea kumsikia kaamua hata kumuacha Mzee Malecela mwenyewe eti anapiga kambi ili kundi lake la wajanja liichukue Moshi .
 
Lunyungu,

Huyu mama hata mimi naona ni mbabaishaji kweli kwa sasa ila amenifanya nianze kuamini maneno ya Simba kuwa hakuna asiye fisadi CCM!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom