Mama Kanifichia paja!!!

Kijana uzee tu huo na uchungu wa mwana basi. Ila jitahi uwepushe mgongano na mawazo potofu waliyokuwa nayo mkeo na mama
 
Kuna jamaa alitusimulia yaliyotokea nyumbani kwake

Jamaa akirudi toka mihangaikoni lazima mkewe ampakulie chakula........ikawa hivi;

Day 1:Kamkuta mke chumbani.........mama mkwe sebuleni..........si kawaida yake............alipomuuliza akasema "najisikia tu vibaya leo"
Day 2:Kama jana yake............alipouliza sababu.........jibu..."Bado najikia vibaya".......mume akaanza kuhisi jambo.....
Day 3:Same situation.......alipouliza......mke akamwambia "mama yako anasema mimi nakupunja chakula"...mi sitaki kuwagombanisha.

Wakatoka chumbani wameongozana na mkewe.......kufika dining....akakuta mama yake anampakulia chakula...........akajaza mlima huo!..........huku akisindikiza na maneno....."naona kila siku hushibi........mi najua ulaji wako mwanangu.........huyu mwenzio atajulia wapi wakati kakukuta ukubwani?"..................

Jibu la mwanaume:Asante mama ila siku hizi siwezi kula kama zamani........nimebadilika..................muulize mke wangu ndio anajua kiasi kinachonitosha!...............huku akikipunguza kile chakula.

Busara ni muhimu sana katika kusolve issue za namna hii!
 
ni kawaida tu,mwanaume asiyependwa na mamake hata mie ningemuogopa! wanawake inatupasa kuanza kuwa secure jamani, alikuwa na mamake lakini akajua anahitaji mke! hata apendweje na mama na dada zake hawawezi kuchukua nafasi ya mke.mueleze mkeo aelewe hili kaka,hongera kwa kupendwa!
 
Mkuu Kumbuka..

Mama ni mama na atabaki kuwa mama yaani mwenye uchungu na upendo wa kweli kwako...Mama ameishi kwa utamaduni mwingine na mke wako..hivyo basi ataendelea kufanya yale ambayo yeye anaona yanafaa na kwa utamaduni anaoujua yeye...Ni vigumu kumbadili anavyofikiri..labda unaweza kufanya taratibu na hapo atalegeza kamba kidogo sana.. Lakni kumbuka mawazo ya mama kwako kwa sasa hata kama wewe una umri wa miaka 100 kwa mama ni sawa na siku ile yeye aliyopata uchungu wako..yaani siku yako ya kuzaliwa..

Sasa..kwa upande wa pili...Mke ni sehemu yako.. mke ni wewe.. mke ni mwili wako lakini uliozaliwa na kukua katika mila, kabila na mazingira tofauti. Kazi uliyonayo ni kumfanya mke wako awe kama wewe..si lazima kwa 100% lakini hata kwa 60% inatosha..Ili nafsi ya mke iwe kama yako inabidi ufanye kazi za ziada.. inabidi ujifunue...ujivue gamba na kueleza na kumfundisha maisha yote na mila zote za kabila lenu.. inabidi ajue kila kitu hata kama ndugu zako ni wachawi...Inabidi amjue Mama yako na Baba yako na shangazi zako ..na wewe inabidi ufanye hivyo kwa upande wao...Kwa kuweza kuoanisha ..na kujuana tamaduni, mila, undugu, maisha, furaha za familia, matatizo, chuki za familia.. mtaweza kuoanisha mawazo na fikira zenu.. Kama mama atakuwa ameficha paja kwa ajili yako.. Mke atakuwa anajua toka mwaka juzi..hivyo atakuandikia sms..na kucheka...Mama ameficha paja na mimi nakufichia kidali ..between the legs..(Joke/movie /utani thread)..Anyway, What I meant..mke atafurahia kile mama anafanya kwani atakuwa anajua na wala si kwa kushtukiza..

Kwa hiyo mkuu kama bado ujajivua gamba anza leo kutoa shule kwa mke wako kuhusu familia, mila, utamaduni na maisha yenu hata kama ni wachawi.. nawe pia ingia darasa kujua upande kwa Mke..
 
Mkuu! Huyo Mama yako ni mchonganishi na nina shaka na upeo wake wa kupembua kibaya na kizuri. Si jambo la kawaida kwa mtu mzima kufanya hayo labda iwe ni stori ya kufikirika. Siku nyingine atakuja chumbani ahakikishe mkeo ana.ma.nu.a vizuri ama la. Huyo mama ni kimeo!!
 
ukiangalia mfaano wa ballerina utagundua kuwa hili jambo ni dogo sana lkn lisipoangaliwa kwa makini linaweza kusababisha balaa kubwa
 
Mama yako anatakiwa aiheshimu nyumba yako regardless umepunjwa mboga au la...!
 
baba anakula paja na maini, na still nilikuwa nimenona, kitoto nilikuwa chinenee, ukitoa mapaja, kuna filigisi, kipapatio, kichwa,shingo,mbavu,kikalio,utumbo. na kote huko unapata virutubisho.
Duh,besti inaelekea wewe ni mlaji na mzoefu mkubwa wa nyama ya kuku.Mi nlikua sijui kama kuku ana sehemu zote hizo.Anyway, cha msingi ni kua huyo mama yake jamaa hapo nyumbani ndo kafika au anapita tu?Pia inaelekea jamaa ye kila akiambiwa anatabasamu tu na kuchukulia 'simple' tu.Angekua siriaz yasingefika hapo
 
Hao mama mkwe visa vyao vimezidi. Khaa!Tutatafuta wachumba wenye single parent au orphan kabisa.
Mimi naona ingekuwa vizuri kama ungeanza wewe kuwa orphan halaf ndo umtafute mwenzio asiye na wazazi pia! Imekaa vizuri eeeh?
 
Sijajua umri wako na kama umefunga ndoa na huyo mansapu wako ila JUA MAMA YAKO KAJA KUKUVUNJIA NDOA. Hahitaji kufanya vitu ambavyo ni jukumu la mkwe, kujua umerudi, umeoga na umekula vyakula vyote yaani ni jukumu la mansapu kukuwekea na kuhakikisha umekula vyakula vyote cha mchana na cha usiku. We mwambie mama yako aache mambo hayo kabla hayajasambaa kwa dada zako kupeana zamu kuja kukutake care.
 
Migogoro na ugomvi wa mara kwa mara wakunyemelea mkuu, mbaya zaidi wazazi ambao twawategemea kwa ushauri na suluhisho wanahusika. Kua makini!
 
Mkuu hili tatizo usilichukulie kirahisi litakuletea matatizo baadae utakuwa huna raha na mkewako hapo kiutu uzima ukiangalia mama kunua paja toka nje ya nyumba kunakitu nikama anaanzisha nshu na kama ingekuwa mapenzi angemwambia mkewako muwekee mumeo hapo ingekuwa hakuna utata mke ndio mwenye hakikubwa ya kukuandalia chakula na si mama mama ni mgenitu japokuwa yeye ndio mzazi heshimayake nikuheshimiwa kwahali ya juu nakutimiziwa yanayo wezekana kwakilahali pia mkeo niwajibu wake kumuenzi mama.
cha msingi muulize mkeo mahusiano yake na mama kwakuwa muda mwingi mwanaume huwa nje ni sirahizi kugundua matatizo ya nyumbani mpaka linapojitokeza na ukijua umuingie mama kwahekima sana mana hawa huwa wanajua sisi ni watu wakujazwa maneno na wakezetu muulize vipi anamuonaje mkewako na anamtendea haki nakama kuna kitu hapendi lakini anashindwa kusema kwakuhofia kuwakosanisha ukipata majibu yao wewe ni mwanaume upime kiutu uzima na ujue jinsi gani ya kubalansi na usipende sana kutumia kilugha wakati mkeo haelewi hebu fkiri kama ni wewe mkeo wakija watu kwako na wakaongea kilugha chaoo utajiskiaje? hususani katika tukio kamahilo unazani mkeo kaelewa vip? mambo madomadogo huleta mgongano mama zetu maranyingi sana huwa wanachangia kuvuruga amani ndani huingilia visivyo wahusu
 
Huyo bibi inaonekana wazi hampendi mkeo na anafanya vituko vya kuwachonganisha hapo inahitajika busara,kwa hiyo stail usidanganyike kuwa unapendwa hapo ni uchonganishi mtiindo mmoja inaelekea kuna kimwana cha kijijini umeandaliwa kwa hiyo amekuja kubomoa ili akupatie hako kamwana
 
Kuna jamaa alitusimulia yaliyotokea nyumbani kwake

Jamaa akirudi toka mihangaikoni lazima mkewe ampakulie chakula........ikawa hivi;

Day 1:Kamkuta mke chumbani.........mama mkwe sebuleni..........si kawaida yake............alipomuuliza akasema "najisikia tu vibaya leo"
Day 2:Kama jana yake............alipouliza sababu.........jibu..."Bado najikia vibaya".......mume akaanza kuhisi jambo.....
Day 3:Same situation.......alipouliza......mke akamwambia "mama yako anasema mimi nakupunja chakula"...mi sitaki kuwagombanisha.

Wakatoka chumbani wameongozana na mkewe.......kufika dining....akakuta mama yake anampakulia chakula...........akajaza mlima huo!..........huku akisindikiza na maneno....."naona kila siku hushibi........mi najua ulaji wako mwanangu.........huyu mwenzio atajulia wapi wakati kakukuta ukubwani?"..................

Jibu la mwanaume:Asante mama ila siku hizi siwezi kula kama zamani........nimebadilika..................muulize mke wangu ndio anajua kiasi kinachonitosha!...............huku akikipunguza kile chakula.

Busara ni muhimu sana katika kusolve issue za namna hii!


Hapo Mother alinyong'onyea sana na sina shaka aaliapia kutokanyaga tena kwa wanae.

Ila pengine yabidi mume utumie busara ya hali ya juu sana katika kutatua migogoro inayohusu wanawake na ndio maana biblia inafundisha "wanaume waishi na wake zao kwa akili". Kutamka maneno fulani mbele ya mkeo au mama yako hasa wakiwa pamoja na mmoja anang'ng'ania yeyey yupo sawa, ni sawa na funda moja tu ambalo laweza kukuumbua. Wapo baadhi ya wanawake ukisikia waume zao wanaonyesha dharau au kutoa kauli ya kumkatisha tamaa hadharani ***** mzazi , mke huyo nae anapata jeuri ya kumtia adabu mama yako mzazi kwa kuona kuwa utamtetea tu!..Sina hakika kama nadharia hii ya "WANAWAKE WANAFANANA TABIA" ni ya ukweli au lah, manake maugomvi mengi katika ndoa chanzo chake ni "MKE, MAMA MKWE na MA WIII!!!" (Note that hao wote wanaweza kuwa nao wana ndoa zao Yaani: Mkeo kaolewa na wewe (mtoto wa Mamamkwe), Mama yako kaolewa na Baba yako (Babamkwe wa Mkeo); Dada yako (wifi wa Mkeo ) kaolewa na Shemejio (Kaka yake Mkeo kwa tafsiri za kibantu)
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom