Mama Kanifichia paja!!! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mama Kanifichia paja!!!

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by ngoshwe, Jul 15, 2011.

 1. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #1
  Jul 15, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  Mamsapu analia ana lalamika,

  Mama Mzazi ametutembelea nyumbani. Majuzi wakati alipokaribishwa chakula cha jioni mezani ma mamsapu (mai waifu wangu) , mama alimuuliza mamsapu kama kaniwekea na mimi ile mboga ambayo walikuwa wanakula na chakula (sikuwepo nyumbani wakati huo kutokana na mihangaiko yangu). Mamsapu akamtania kuwa "hajaweka" akidhani mama hayupo "serious" .

  Jana nilichelewa pia kurejea, lakini cha ajabu nilipofika nyumbani sikukuta mtu sebuleni (sitting room), nilipoingia chumbani, nikamkuta mamsapu akiwa amelala kajifunika gumbi gu,mbi, nikamfunia na kuuliza "vipi unaumwa??" akasema hapana, sikujali, nikarejea mezani kupata chakula, wakati nikijiandaa kula, mara mama akatoka chumbani kwake akiwa na bakuli mkoni, akaweka mezani na kuniita kwa jina langu na kuniambia kwa kilungha..."nimekuwekea hii.....akinionyesha kipaja cha kuku!!" Napo sikujali, nikamjibu tu "Asenti...!!" akatabasamu. Nikamuuliza kwani nyini wenyewew mshakula..akajibu ndio. Sikuwa na neno zaidi nikaendelea kula huku yeye akiwa amekaa pembeni yangu...mara nikasikia mlango wa chumbani kwetu unafunguliwa ..mamsapu akatoka na kuchukungula kidogo kisha akaingiza tena shingo ndani na kufunga mlango na kutoa mgumo "Mh...!!".

  Mama akaniaga, naenda kulala ..nikamruhusu ..lakini alipokuwa akiondoka akasema kwa kilugha tena .."jana hawakukuwekea hiyo mboga tulikula sisi nikaona leo nikununulie mwanangu..." nikajibu tu sawa asante...

  Mie na Mamsapu wangu hatutoki kabila moja hivyo hatuelewani pale mtu wa kwetu akiongea kikabila , niliporejea chumbani tena nikamkuta Ma msapu kakaa kitandani huku kashika tama na machozi yanamtiririka...nikamuuliza nini..akang'aka, "Naona mama yako leo ameamua kukufichia mboga??" haya bwana..lakini naona amenidharau sana!!!" sikuelewa, akanieleza yaliyotokea jana yake na siku hiyo, kumbe mama alimtuma mjukuu wake (mwanangu) klwenda kununua hicho kipaja cha kuku lakini hata mwenyewe hakula akaweka chiumbani kunusubiri..kabala mamsapu alimuulizaz akajibu amenitunzia mimi wamanae kwa kuwa jana walininyima nyama (kuku)...Ma msapu kakasirika sana anahisi ahaminiki na mama yangu, .Sielewi kama mapenzi haya ya mama kwa mwanae (mimi) ni mapenzi ya kujenga au kubomoa!! ..sijui wanaume wenzangu mna uzoefu gani na wazazi wenu wa kike, rafiki yangu mmoja kaniambia mama yake mzazi alikuwa halali jamaa akiwa hajarejea kwenye mihangaiko, atakaa sebuleni weee mpaka asikie mwanae ameingia ndani, amekula ndipo nae anyanyuke kwenye kochi sebuleni kwenda chumbani....Mwingine anasema eti hata hawa wake zetu nao wanawapenda zaidi kaka zao kuliko sie waume zao, na wakizeeka, watawapenda zaidi watoto wao wa kiume kuliko wakwe zao....
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  Jul 15, 2011
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Mama yako anakupenda wala hamna ubaya hapo.

  Kwa kuuliza tu...we hiyo jana yake kama hakukubakishia mboga (kuku) we ulikula nini!!? Labda mama kaona unapunjwa kwahiyo kaamua akunnepeshe mwenyewe wakati yuko around?!

  Binafsi nilizoea nyumbani kama baba yupo around (hayuko safarini) ila wakati wa mlo kakosekana tunamtengea mboga yake inawekwa pembeni kabla ya tuliopo kupakua.Hata asipoila akirudi ila atakuta amewekewa...kitu ambacho binafsi nadhani ni kizuri.
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  inawezekana ni upendo tu wa mama yako ambao ni natural kwa mzazi.

  Pia inawezekana mkeo anahs kuwa mzazio anaingilia maamuzi yake ya ndani.
  Au mama yako anahs mkeo hakutunzi vyema na hapo ndo ugomvi unapoanzia.

  Pili mamayako nahs ni mtumzima/mzee so inahtaji uvumilivu kuisha nao,sometimes wanakua kama watoto,so wachukulie kama walivyo

  zaid usi-take side, jitahd kuwa neutral kadri uwezavyo kuepusha misuguano.
   
 4. Magulumangu

  Magulumangu JF-Expert Member

  #4
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 7, 2010
  Messages: 3,040
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  hamna cha ajabu hapo mkuu...mama ni mama tu...mkuu usiombe mama yako ana uchungu sana na wewe na mkeo anao zaidi lkn sasa hapa daima lipo na litakuwepo kutoelewana mama na mkwe
   
 5. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #5
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  Hao mama mkwe visa vyao vimezidi. Khaa!
  Tutatafuta wachumba wenye single parent au orphan kabisa.
   
 6. The Boss

  The Boss JF-Expert Member

  #6
  Jul 15, 2011
  Joined: Aug 18, 2009
  Messages: 37,826
  Likes Received: 22,465
  Trophy Points: 280
  aisee
  mama zetu hawa bana...
  ushauri ni kuwa nunua kuku wengi uweke nyumbani..
   
 7. ngoshwe

  ngoshwe JF-Expert Member

  #7
  Jul 15, 2011
  Joined: Mar 31, 2009
  Messages: 4,075
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 145
  @ Hus, wengine wanadai wanawake wanapenda zaidi wale wa kwao (waliowazaa au kutoka katoka katika tumbo/damu moja) na hilo linafanya magomvi mengi katika ndoa yaonekane chanzo ni ma mama wakwe au mawifi..na hata wale wanaoolewa kwenye familia zisizo na wazazi wa upande wa kumeni, nao wakina kuwa mwiba kule wanakotokea (kwa wake za kaka zao) na wakizaa na watoto wao wa kiume kuoa, wanakuwa mwiba zaidi kwa wake za watoto wao wakiume (hapo wanafikia qualification ya umama mkwe).
   
 8. Husninyo

  Husninyo JF-Expert Member

  #8
  Jul 15, 2011
  Joined: Oct 24, 2010
  Messages: 23,814
  Likes Received: 583
  Trophy Points: 280
  unajua haya mambo huwa ni kwa pande zote mbili, mke nae anaweza kuwa mkorofi kuliko mama mkwe. Nafikiri kikubwa ni mwanamke kumsoma mkweo yupo vipi, kuna wakwe wengine walishazoea kufanyiwa vitu/huduma fulani na watoto wao. Wakwe wa namna hii huanza visa pale wanapokosa hiyo huduma/vitu. mke hapo kama anaafford ni bora kuendeleza yale aliyokuwa anafanyiwa mkwewe na mtoto wake. Hlf hizi habari za kuishi mke mume na wazazi wao nyumba moja ndio zinaleta mgogoro. Hebu wazazi wapeni space watoto zenu.
   
 9. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #9
  Jul 15, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Kuna baadhi ya wanawake wana hila ya choyo, kwandugu na hata kwa mumewe pia.
  Hivi mi nakulaje Kuku bila ya kumbakishia mume wangu? haiwezekani kabisa, kwahiyo inawezekana mama yako ameona kwamba mkeo ni mchoyo kwako. ndio maana amekufichia, watu wazima wanaona mbali. Mimi ninavyojua baba ndio anawekewa paja na maini.
   
 10. b

  bibi.com JF-Expert Member

  #10
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 8, 2011
  Messages: 1,155
  Likes Received: 36
  Trophy Points: 145
  jamani baba anapewa paja na maini loohh huo ni unyanyasaji kwa watoto wake, no wonder watoto wetu wana afya duni na baba zetu wanavitambi
   
 11. 22nd

  22nd JF-Expert Member

  #11
  Jul 15, 2011
  Joined: Aug 1, 2010
  Messages: 498
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  baba anakula paja na maini, na still nilikuwa nimenona, kitoto nilikuwa chinenee, ukitoa mapaja, kuna filigisi, kipapatio, kichwa,shingo,mbavu,kikalio,utumbo. na kote huko unapata virutubisho.
   
 12. s

  sinani Member

  #12
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 15, 2009
  Messages: 36
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  kosa ni kutouliza pale ulipopewa paja na mama yako..ulitakiwa baada ya kusema asante umuulize mbn jana nilikula mboga sikunyimwa??na pia jitahidi ufanye ufanyavyo urudishe uhusiano wa mkeo na mama yako km awali ukiacha mambo km yalivyo sasa am sure utarudi na stori nyingine soon kuwa washagombana na hawasemeshani
   
 13. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #13
  Jul 15, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Mama ni mama tu jamani...mke/mume ni complimentary tu!
   
 14. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #14
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Ni mapenzi tu ya mama kwa mwanae, huyo mkeo anatakiwa kulielewa hilo. We kuwa kawaida tu wala usiegemee upande mmoja ili kuepusha ugomvi manake mkeo anaweza akawa anajihisi vibaya, hasa kwa kuwa mnaongea kikabila chenu ambacho ye hakijui.
   
 15. First Born

  First Born JF-Expert Member

  #15
  Jul 15, 2011
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 5,315
  Likes Received: 96
  Trophy Points: 145
  Uwezekano wa kuwa mamsapu wako hawapatani na mama kiasi cha mama kuchukua jukumu la mke wako upo, mke wako atakuwa amemuudhi mama hadi kufikia hatua ya mama kukuwekea mboga, usije ukazidisha mapenzi upande mmoja, jaribu kufanya uchunguzi kujua fault ili ujue maamuzi sahihi.
   
 16. Katavi

  Katavi Platinum Member

  #16
  Jul 15, 2011
  Joined: Aug 31, 2009
  Messages: 39,469
  Likes Received: 4,128
  Trophy Points: 280
  Hakuna cha ajabu hapo...
   
 17. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #17
  Jul 15, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  mwenzenu sina baba wala mama. mama yangu namwona kwenye picha tuu. baba yangu alifariki nikiwa tayari nimemaliza form six. mwenzangu both parents wapo. kwa kweli wakiwa wanatutembelea yaani mpaka raha, hayo maandilizi tunayoyafanya! baba mkwe akija huwa anaondoka na kitambi. mama mkwe akija huwa nakuwa km ka mfalme flani hivi maana wife ataambiwa mpe matunda mkwe mara maziwa jagi hiloo mara mama mkwe anatuofa kitimoto yaani inakuwa burudani tosha. kingine nahisi mara nyingi wanawake wanakuwa hawana confidence sana na ndugu wa mume hasa ma wifi yaani kila kitu kinakuwa politicized na movement au gesture yoyote lazima ipate tafsiri utasikia alicheka sana au mbona haongei akila kitu bila kukimaliza issue haha si mchezo
   
 18. A

  Ave Ave Maria JF-Expert Member

  #18
  Jul 15, 2011
  Joined: Apr 22, 2011
  Messages: 10,757
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 0
  Ni mapenzi tu ya mama kwa mwanae, huyo mkeo anatakiwa kulielewa hilo. We kuwa kawaida tu wala usiegemee upande mmoja ili kuepusha ugomvi manake mkeo anaweza akawa anajihisi vibaya, hasa kwa kuwa mnaongea kikabila chenu ambacho ye hakijui.
   
 19. Ballerina

  Ballerina JF-Expert Member

  #19
  Jul 15, 2011
  Joined: Jun 2, 2011
  Messages: 388
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Yaani usipokuwa makini si muda mrefu familia yako itageuka kuwa ya mgogoro..........kisa.........mama Vs mke;

  1. Kina mama wengi huwa na mapenzi sana na watoto wao na mara nyingi husahau kuwa jukumu la kumlea huyo mtoto(ambaye keshakuwa mtu mzima na ameshaoa),linahamia kwa mke

  2. Pia huwa na dhana kuwa kwa kuwa mke amekutana na huyo mtoto(mume) akiwa mtu mzima tayari.............basi hawezi jua vizuri nini anahitaji..............kwa kiwango gani..........kwa kiasi gani...........na wakati gani......ILA yeye mama ndio anajua zaidi kwa kuwa kamlea.

  3. Kina mama wengi huwa hawajakubali kuachia...........ie to let him go..............wanaume wanakuwa na wake zao lakini bado mama anabaki anamiliki kwa remote control...........akihisi bado anahitaji kuongozwa............ile dhana kuwa si nimemzaa mimi?? bado imewakaa kichwani.

  on the other hand
  1. Mke hujiona kama nafasi yake inachukuliwa na mama mkwe.............ie kuendesha nyumba yake
  2. Mke huwa na wivu kwani yale mama anayoyafanya.....kama kumfichia kipaja cha kuku.............inatafsiriwa kuwa "ina maana mimi simjali au?......ningekuwa simpi chakula angekuwa hai mpaka leo? + mnaongea lugha ambayo mwenzenu haielewi................".

  Ikumbukwe kuwa kumuandalia mume chakula ni sehemu ya mke kuonyesha mapenzi kwa mume wake...........na maongezi mengine matamu huanzia hapo,wakati wanakula.....sasa nafasi ikichukuliwa na mama mkwe.....wivu huibuka......japo hauna maana mbaya

  Wanaume mtumie busara ya hali ya juu kubalance this kind of situation before problems arises........wote ni watu muhimu kwenu............
  Mama ana nafasi yake...mke ananafasi yake.....hapo mnapoishi ni kwa mkeo kimadaraka......wewe raisi yeye waziri mkuu........na mama mgeni mwalikwa......

  Hii ya kipaja ni dalili ya kwanza kuwa haridhiki na mkeo anavyokuhudumia....................zitakuja nyingine nyingi,mwishowe utaambiwa huyu mke hakufai.....................

  Wanaume mlio oa,hakikisheni mke anabaki kwenye nafasi yake...................na mama asidharauliwe kama mzazi.
   
 20. Anfaal

  Anfaal JF-Expert Member

  #20
  Jul 15, 2011
  Joined: Jan 19, 2010
  Messages: 1,157
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Ukisoma thread hii utagundua sisi ni masikini kiasi gani. Imagine matatizo yanaanzia kwenye mboga? Kule nje kuku ni kitu cha kawaida saana. Tujitahidi tujikwamue sisi na jamaa zetu kwenye tatizo hili. Maana hili linanikumbusha miaka ya nyuma familia zilivyokuwa zinasambaratika kisa mke kafungia TV kwenye kabati.
   
Loading...