Mama hamtaki mchumba wangu

Mama hamtaki mchumba wangu

Nimeshawahi kuwaza kitu kama hiko.. maybe hiyo ndio sababu kubwa lakini anakwepa kuniambia.

Sent from my SM-J110F using JamiiForums mobile app
UNAHITAJI KUTUMIA BUSARA KUBWA SANA HAPO MOSI MCHUMBA/MKEO ANATAKIWA AJUE NAFASI YAKO KTK FAMILIA YAKO NA AIKUBALI 100%(ila ningumu kwa wabeijing)na KUISHIRIKI KWA MOYO WAKE WOTE MAANA SI WAWILI TENA BALI NI WAMOJA.NA MTENGENEZE MBINU MBADALA YA KUONGEZA NGUZO MBALALA ILI NANYI MUWEZE TENGENEZA MJI WENU BAADAE
O
 
Ila binti akishakataliwa na mama mkwe ni sheeedah!!! Mama akishaonesha chuki ata akikukubalia mwanzoni ujue Vita ataendelea mkiwa kwene ndoa mi nayaona kwa Dada angu adi mama mkwe anamuendea kwa waganga afu makabila ndo kama hayo mama mkwe mchaga.....mwalii mkurya
 
Mwenzio yameshanikuta hayo,tena sio mama pekee hadi dada na wadogo zangu wa kike ila msimamo wangu ndo ulinisaidia.kuna msemo unasema ISHI UTAKAVYO SIO WATAKVYO.Yani leo ndo wifi kipenzi cha wote kwani kuweka tinted na kuvaa head phone ilisaidia sana.
 
Habari za asubuhi ndugu zangu, natumai mmeamka salama.

Lengo la kuleta hii mada ni kuomba ushauri kwa ajili ya jambo linalo nisumbua kwa muda mrefu.

Mimi ni kijana mwenye miaka 25, nimemaliza chuo miaka miwili iliyopita na namshukuru Mungu maisha yanaenda vizuri. Ndugu zangu nimekuwa kwenye mahusiano kwa miaka miwili na mchumba wangu. Tumesaidiana mengi na ameonesha mapenzi ya kweli kwangu kwani amejitoa kwa mengi nami nampenda sana kutoka moyoni.

Tatizo ni kwamba toka nilipomtambulisha kwa mama, mama ameonesha chuki waziwazi kwake. Nilijaribu kukaa na mama na kuongea nae lakini sasa hana sababu maalumu ya kumkataa.

Niliwahi kumuuliza pole pole lakini akasema kuwa hajisikii amani moyoni mwake kuhusu mchumba wangu. Nikamuuliza kwanini hajisikii amani? Akakosa jibu akanipotezea.

Sasa mchumba wangu ameumia mno kiasi kwamba anataka tuvunje mahusiano baada ya kujua mama hampendi. Kwakweli nimejaribu kila njia katika kusuluhisha hili jambo lakini naona naelemewa.

Ndugu wa mwanamke wananielewa sana na imetokea kwao wamenikubali sana, haswa mama yake na baba yaani wakiniona wanafurahi. Lakini mama yangu mimi hamtaki na hana sababu maalumu ya kumkataa.

Nifanyaje wadau? Naombeni ushauri wenu.
HAWA AKINA MAMA HUWAGA NA SIRI KUBWA , MTUMIE SHANGAZI, AU BIBI YAKO AKUULIZIE USIJEKUTA HUYO MCHUMBAAKO NI DADA YAKO.
 
Mwenzio yameshanikuta hayo,tena sio mama pekee hadi dada na wadogo zangu wa kike ila msimamo wangu ndo ulinisaidia.kuna msemo unasema ISHI UTAKAVYO SIO WATAKVYO.Yani leo ndo wifi kipenzi cha wote kwani kuweka tinted na kuvaa head phone ilisaidia sana.
Thanks brother eddy... mi ni mtu naamin katika misimamo sana.. i hope kipind hiki ndio misimamo inahitajika sana.
 
Kumbe wewe ni mchaga, bure kabisa, muoane tu wenyewe kwa wenyewe, maana huyo dada mkurya mtamuambukiza ubinafsi na ukabila wenu, huyo mama aendelee kukataa tu, pia huyo binti ashikilie msimamo wake ili muachane tu.
 
Kumbe wewe ni mchaga, bure kabisa, muoane tu wenyewe kwa wenyewe, maana huyo dada mkurya mtamuambukiza ubinafsi na ukabila wenu, huyo mama aendelee kukataa tu, pia huyo binti ashikilie msimamo wake ili muachane tu.
Among the greatest thinkers of jamii gorums...ahahaaaaa....unajenga au unabomoa?
 
Hisia za kimapenzi kuna wakati huzidi nguvu ya hekima. Chunguza kwa umakini ili utambue kwa nini Mama anakataa, kisha sababu zake zitafakari kwa umakini kwa kuegemea kwenye hekima na kujitahidi kushinda nguvu za hisia.

Kuna wakati ushauri wa kutoendelea na mipango ya ndoa huwa una faida kwa nyie wote wawili japo mkiwa kwenye nguvu za hisia za kimapenzi hamtaweza kulitambua hilo. Jitahidi mpaka ufahamu sababu za Mama kukataa ili uweze kuzipima sababu zake kama ni za msingi au hapana.

Lakini utambue pia kuwa Mama yako kumkataa mchumba wako , naye mchumba wako kulitambua hilo, tayari ni doa hata kwa mipango ya mbeleni. Mkiendelea na mipango yenu, maisha yakaenda vizuri itakuwa ni heri lakini mambo yakienda vibaya, mtayakumbuka yote haya tena na tena.
 
Kua na msimamo. Wamama weng wanawivu na wengi wanaoharibu ndoa Za watu ni mawifi na ma mkwe, ww simamia msimamo wako kua huyo ndio chaguo lako pia ukae na mchumba wako na umwambie pamoja na kua mama yako hamtak ila atakapokua mke wako kamili asimlipize ma mkwe ampende kwa dhat pamoja na mawifi zako wao wenyewe wataongeza, jaman wamamamkwe wivu nn muwe mnawaacha watoto wenu waishi na machaguo ya moyo wao, jaribu kufikir upande mwingine angekua mwanao wa kike kakataliwa kuolewa na kabila fulan ww kama mama ungejisikiaje? Mkuki ni mtamu kwa nguruwe kwa binadamu ni mchungu tu, ni hayo tuu
 
mwanamke aliambiwa ataachana na wazaz wake atafatana na wazaz wake , hata wewe mwnamme itakuwa hivyo hivyo, la muhimu hapa ni we kuelewa kuwa ampende hasimpende wewe lazima uoe unapo taka, haiwezekani mamako akuchagulie mchumba, we unamtomasa mamako nini? mpe vyake huyo mama ni mama mke ni mke, kwa umri wako mama ko huwezi mvulia chupi akaonoa nyoya lako ila mchumba wako unamvulia na kumjambia kama kawa kama dawa, ila mamaako hata kumjambia uwz.
 
Kuanza kabisa mimi ningependa kukuondoa wasiwasi, mabinti wa kikurya wakiolewa huwa hawahusiki kwa namna moja au nyingine na nyumbani kwao, kwa hiyo kuhusu binti kuwa na msimamo eti atakufanya usahau kwenu sio kweli, Kwani binti wa kikurya akisha olewa anakua ni kwa upande wa mwanaume tu, hata kama awe na msimamo vipi, pili kama umeridhika nae serious kuwa na msimamo wa kiume, sababu sio kila kitu lazima ufuate wanachosema wazazi, wao sio malaika wanaweza wakakosea pia.
 
Ila binti akishakataliwa na mama mkwe ni sheeedah!!! Mama akishaonesha chuki ata akikukubalia mwanzoni ujue Vita ataendelea mkiwa kwene ndoa mi nayaona kwa Dada angu adi mama mkwe anamuendea kwa waganga afu makabila ndo kama hayo mama mkwe mchaga.....mwalii mkurya
Wachaga bn mbona binti zao wakiolewa na kabila zingine huwa hawapingi, kumbe huwa wanamaslahi yao binafsi eeeeh???
 
Katika ndoa kuna kuachana je kwa mama nae? Fikiria sana mama yako amekutoa wapi mpaka umefika hapo na mchumba wako amekukuta wapi na mnakwenda wapi
 
ukikubali matakwa ya mama yako utamchukia hadi unakufa. mke wako mpya akizingua kidogo hasira utakuwa unapeleka kwa mama. utajisemea, nilikuwa na demu mzuuri kisa mama nimepata garasa. kama hana sababu ya msingi kuwa mwanaume fata unayoona yanafaa.
 
Lazima mama ana sababu za kumkataa;
Zaidi ya hapo atakuwa mke wako pekee yako;
jishauri, chukua hatua.
hawezi kumkataa bila sababu. anachotakiwa ni kusema ipimwe uzito. kukataa b kusema sababu ni dharau kubwa kwa kijana wake.
 
Back
Top Bottom