Damaso
JF-Expert Member
- Jul 18, 2018
- 6,132
- 10,514
Ni saa mbili asubuhi jijini Dodoma. Simu ya mezani ya Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima, inaita mara mbili mfululizo. Ni taarifa kutoka kwa wananchi zinaoeleza kuhusu mzozo wa kifamilia uliosababisha taharuki katika moja ya mtaa ya jijini Dar es Salaam.
Kwa ustadi na umakini wa hali ya juu, Dkt. Gwajima anapokea taarifa hizo na mara moja kuanza kutoa mwongozo. Anatoa maelekezo pamoja na namba za simu za wahusika ambao wanapaswa kushughulikia suala hilo huku akiweka wazi kuwa atafuatilia suala hilo kwa upana wake na kutoa pole kwa familia.
“Jamii yenye nguvu huanzia katika familia imara,” hii ni nukuu ambayo inaendana na maisha ya Dkt Gwajima. Ni kauli ambayo si tu inaleta suluhu, bali pia inadhihirisha falsafa yake ya uongozi: kiongozi si mtu kwa cheo chake, bali ni mlezi na mshauri wa jamii.
Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima ni miongoni mwa viongozi wachache wa Tanzania ambao utumishi wao umekuwa ni tunu kwa wananchi ingawa yupo ndani ya chama cha X.
Kwa wengi, yeye ni alama ya matumaini, mtu anayeishi kile anachokihubiri. Akihusiana kwa karibu na changamoto zinazowakabili Watanzania wa hali ya kawaida, amekuwa mstari wa mbele kupigania haki za wanawake, watoto na makundi maalum. Hutumia muda mwingi kusikiliza, kuelewa na kushauri, akithibitisha kuwa nafasi yake si ya kisiasa pekee bali ni ya kijamii.
Katika kampeni mbalimbali za kitaifa zinazolenga kumaliza ukatili wa kijinsia na kuhakikisha kuwa watoto wanapata haki zao, Mhe. Gwajima amejikita si tu katika kutunga sera, bali pia katika kushiriki moja kwa moja kwenye vikao vya usuluhishi, mikutano ya kijamii na hata kutembelea maeneo yenye changamoto. Mtindo huu wa uongozi umewafanya wananchi kumwona kama kiongozi anayeishi ndani ya jamii na siyo juu yake.
Upekee wake unadhihirika pia katika namna anavyowatia moyo watu, wanaume na wanawake pamoja na vijana ingawa kuna wakati anatia chumvi na kunogesha maisha. Mara nyingi amekuwa akionekana kwenye mitandao ya kijamii akitoa elimu na wakati mwingine kuburudisha majukwaa kadhaa.
Ila upekee wake ambao unamuweka tofauti na viongozi wengine ni uchangamfu na usikivu haswa matatizo ya kijamii yakitokea.
Kitu kingine kinachomfanya awe tofauti Dkt. Gwajima ni uhalisia wa maisha yake binafsi unaoendana na dhima yake ya kitaifa. Watu humwona kama Mama mnyenyekevu, mwenye huruma na anayejua changamoto za kulea, kushauri na kulea kizazi kipya. Ni mfano wa namna mwanamke anaweza kuwa, Mama bora na bado akaendelea kuwa kiongozi thabiti.
Ni ukweli kwamba Tanzania imebarikiwa kuwa na viongozi wengi wenye nia njema, lakini si wote ambao huacha alama ya kudumu mioyoni mwa wananchi.
Kwa Dkt. Dorothy Gwajima, nafasi yake katika historia ya Tanzania ni ile ya kiongozi ambaye alitumia nafasi yake kuleta mshikamano, matumaini na mwelekeo bora kwa jamii. Yeye ni tunu ya utumishi wa umma – kioo kinachotuonesha kuwa uongozi bora ni ule unaochanganya hekima, ucheshi, upendo na mshikamano ndani ya jamii.
Mama Gwajima ninakupa heshima kubwa sana na upekee maua yako! Fahamu wewe ni kipenzi cha watanzania, ingawa upo chama X ila watu wanakupenda sana, kazi yako ni kubwa na nzito ila unatufanya tufurahi na kujifunza kupitia kazi yako. Wala huna deni na mimi, ISHI SANA BI MKUBWA.