Mama bado anaupiga mwingi?

Mama bado anaupiga mwingi?

Amalrik TZ

JF-Expert Member
Joined
Aug 9, 2020
Posts
341
Reaction score
303
Neno ‘mama’ lina maana kubwa maishani mwakila mmoja wetu. Ninapotamka ama kusikia neno mama mawazo yangu yanazama kwenye fikiria za matumaini, Faraja,huruma na upendo wa dhati usikuwa na kipimo kutoka kwa mama.

Rais wa awamu ya sita alipoingia madarakani akiwa ni mwanamama mioyo ya watanzania walio wengi ilipata matumaini, matarajio mapya Pamoja nakudhani nuru mpya imeingia.

Watazania walio wengi walidhani wakati wa uonevu hasa kwa wanasiasa wa upinzani, wafanya biashara wakubwa nchini na wale wote wenye mawazo kidhani na serikali yamezikwa na Magufuli kule Chato.

Mama naye hakuanza kinyonge kabisa alianza kwa bwebwe na kwa kauli zenye kuchochea matumaini makubwa ndani ya mioyo ya watanzania. Nakumbuka tarehe 01/04/2021 akiwa ikulu Chamwino Dododma akiwaapisha baadhi ya Mawaziri wake wapya aliowateua alimwambia Waziri wa fedha DR. Mwigulu Mchemba

“Muende mkatanue wigo wa walipa kodi, lakini pia mtengeneze walipa kodi wapya wengi Zaidi. Trend unayoenda nao sasa hivi nikuua walipa kodi, mnaua wafanya biashara, mnatumia nguvu Zaidi kuliko akili na maarifa kupata kodi.

Sasa wale mnao wakamua mkaenda kuchukua vifaa vyao vya kazi, kienda mkafungia akaunti zao, mkaenda chukua pesa kwa nguvu kwenye akanti kisa sheria inakuruhusu kufanya hivyo akitoka hapo anakwenda kufunga biashara anahamia nchi ya pili mnapunguza walipa kodi”. – Rais Sahia Suluhu Hassani.

Hii ni kauli yenye matumaini makubwa na inaleta Faraja kwa kila mtanzania hata mimi nisiyekuwa mfanyabiashara.

Fikira zetu zilianza kuamini maneno matupu kama haya na kudhani maisha mapya yanakuja and things will never be the same again.

Furaha ya kupata Rais wa awamu ya sita tena mwanamama ilifunika akili zetu kuzitafakari kwa kina kauli zake kama hizi ; “Ukinizingua tutazinguana” haya nayo ni maneno ya mama aliyoyasema tena uso na mikono yake ikionyesha msisitizo mkubwa huki pia kila akisimama kuhutubia anarudia rudia kauli yake ya “Mimi na Magufuli ni kitu kimoja”.

Ni kweli Mama na Magufuli ni kitu kimoja kwani wote wamepikwa na kuiva vizuri na Chama Cha Mapinduzi. Wote wawili ni mazao bora ya CCM.

Hawa wote wamepatikana kwa kupitia Katiba tunayoitumia sasa iliyoandika enzi ya chama kimoja na kufanyanyiwa marekebisho kadha wa kadha.

Tukumbuke Katiba hii iliandikwa na wanaCCM na marekebisho hata yake ya mwaka 1995 ya kuruhusu vyama vingi yaliongozwa na wanaCCM huku wakijua namna ya kutengeneza mfumo wa wao kuongoza milele.

Ngugu yangu, hakuna mwenye nia ya kumzingua Mama(Rais). Bali wengi wanapiginia haki na utawala bora wa sheria kitu ambacho ni tishio kubwa kwa Chama Cha Mapinduzi.

Mambo ya kupigania Katiba mpya na utawala bora wa sheria yote yanayoeenda kinyume na agenda za CCM. Chama Cha Mapinduzi hakijajengwa wala hakiishi kwa misingi ya haki na usawa.

CCM imejengwa kwa kutumia dola na kila Rais lazima afundishwe namna bora ya kutumia polisi na taasisi zote kiusalama ili kuhakikisha utawala wa chama hiki.

Ndiyo maana Swala lolote lile linaloenenda kinyume na agenda za CCM mama anaona kama watu wanamzingua nayeye anatumia dola kuwachapa wale wote wanao mzingua.

Ndiyo maana alisema swala la Katiba mpya apewe muda kwanza ajenge kwanza wanchi. Na juzi kwenye mahojiana na BBC Swahili alisema wale wote wanaodai katiba mpya ni kama wanafanya siasa za chokochoko dhidi ya utawala wake.

Katiba mpya sio agenda ya CCM na kamwe haiwezi kuwa agenda yao. Kwasababu hakuna binadamu mwenye akili timamu anayependa kujiua mwenyewe.

Siku ambayo CCM itakakubali agenda ya katiba mpya ndio utakuwa mwanzo wa mwisho wa chama hiki na kusahaulika kama kilichotokea kwa chama cha KANU kilivyosahaulika nchini Kenya.

Mama akiwa kama Mwenyekiti wa chama na Amiri jeshi mkuu lazima afanye jambo la kila namna kulinda chama chake. Njia pekee ambayo mama kama mama anaweza kulinda maslahi ya chama chake ni kuwa Dikiteta.

Hali hii ndiyo inayopelekea matukio ya ajabu ajabu na uonevu mkubwa kwa wale wote wenye mawazo pinzani na CCM na serikali kupata mateso makali. Mbowe kuitwa Gaidi sio jambo la kushangaza kwani ndio option pekee walionayo mkononi kwa sasa.

Hali kama hii itaendelee sana na wengi wetu tutaumia. Ndugu zangu Katiba mpya haitapatikana kwa mapenzi mema ya Chama Cha Mapinduzi bali itapatikana kwa mapenzi na utayari wa watanzania kuipigania katiba mpya kwa nguvu, akili na mali zao.

Nakumbuka kipindi Mama anaingia madarakani niliandika Makala fupi sana na kupost humuhumu Jamii Forumu na kusema “CCM ni ileile’’ unaweza kuisoma ukiingia kwenye profile yangu na hakuna mabadiliko yanayoweza kutoka bila ya mabadiliko ya katiba mpya.

Tatizo sio Magufuli au Mama. Tatizo ni Katiba iliyopo sasa inayoruhusu CCM kujenga mfumo kandamizi kwa washindani wake wa kisiasa. Dawa pekee ya tatizo hili ni Katiba mpya na uwezo wa kupatikana kwa Katiba mpya mpo mikononi mwa watanzania.

“Praise team” mnaosema mama anaupiga mwingi, vipi kashafunga magoli mangapi?

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Hatukati kabisa katika hilo na tunaheshimu kitu cha urais haijalishi yupo Mwanamke au Mwanaume.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app

Tunatakiwa kumuongelea Samia Suluhu Hassan kama Rais rais ambaye ni mama/mwanamke, sio tumuongelee kama mama peke yake

Kila mwanaume/Mwanamke anaweza kuwa baba/mama kwa uzazi au malezi lakini sio kila mwanamke/mwanaume anaweza kuwa rais. Na hilo tulielewe na kuliheshimu
 
Mwambieni kuna sheria ya offside katika mpira, asipokuwa makini ataondoka bila kufunga hata goli moja... ili afunge lazima awe line moja na mabeki wa timu pinzani ili awatoke - sasa yeye anakaa mbele kabisa kwa kipa wa timu pinzani eti wamwagizie mpira wa juu kwa juu ili atupie.. hilo haliwezekani.
 
Kumbe Mbowe alikuwa "atouchable" pamoja na kufanya uovu wake wote huo!

Alikuwa anajificha kwenye kivuli eti cha kudai demokrasia kumbe alikuwa mafia wa kupanga mikakati miovu! duh!

Bora amekamatwa na kufikishwa ktk vyombo vya sheria maana endapo angeachiwa angeumiza wengi sana, lakini pia kama kuna mtandao wake wote alio utengeneza ktk harakati za kigaidi unapaswa umalizwe wote kuwe na siasa safi na sio kutisha na kuuwa.

Tanzania lazima iendelee kuwa na amani na utulivu.
 
kumbe Mbowe alikuwa "atouchable" pamoja na kufanya uovu wake wote huo!
,alikuwa anajificha kwenye kivuli eti cha kudai demokrasia kumbe alikuwa mafia wa kupanga mikakati miovu! duh!...
Chombo pekee cha kuamua kama kina Mbowe ni Gaidi au laa ni Mahakama wala sio Rais. Rais hana mamlka ya kuhukumu mtu isipokuwa Mahakama pekee

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
IMG-20210811-WA0125.jpg
 
kumbe Mbowe alikuwa "atouchable" pamoja na kufanya uovu wake wote huo!!!
,alikuwa anajificha kwenye kivuli eti cha kudai demokrasia kumbe alikuwa mafia wa kupanga mikakati miovu! duh...
Lazima tuwe na Katiba ambayo haitoi mianya kwa mtu kuwa "untouchable". Japo katiba hii inamapungufu lakini kina Mbowe sio untouchable mtu pekee ambaye ni untouchable ni Rais aliyeko madarakani.

Sent from my SM-A107F using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom