Mama aolewa na mwanaye baada ya kumpa ujauzito

Mama aolewa na mwanaye baada ya kumpa ujauzito

CTX

JF-Expert Member
Joined
Jan 3, 2015
Posts
1,273
Reaction score
987
zim-marry.jpg

Betty Mbereko na mwanaye, Farai Mbereko.

BETTY MBEREKO (40) mwanamke anayeishi Mwenezi huko Masvingo, Zimbabwe, ameolewa na mwanaye wa kumzaa aitwaye Farai Mbereko mwenye umri wa miaka 23.



Katika hali hiyo ambayo ilitokea mwanzoni mwa mwezi huu wa Oktoba, mama huyo anategemea kupata mwanaye ambaye pia ni mjukuu wake. Mwanamke huyo amekuwa mjane kwa miaka 12 iliyopita ambapo amekuwa akiishi na mwanaye huyo.



Alithibitisha hivi karibuni kuwa ana ujauzito wa miezi sita na hivyo akaona afadhali “aolewe” na mwanaye kwani hakutaka kuolewa na mmoja wa wadogo wa marehemu mumewe, aliosema wanamtamani.



Betty aliishangaza mahakama ya kijijini kwake aliposema alianza kuzini na mwanaye miaka mitatu iliyopita. Alisema baada ya kutumia fedha nyingi kumsomesha Farai baada ya kifo cha mumewe, aliona ana haki ya kufaidi fedha ya mwanaye na si mwanamke mwingine.



“Tazama, nilihangaika kumsomesha mwanangu na hakuna aliyenisaidia. Sasa mwanangu anafanya kazi na watu wanasema nimefanya kosa. Acha nifaidi mazao ya jasho langu,” aliiambia mahakama hiyo.

Farai alisema yuko tayari kumwoa mama yake na atalipa mahari kwa babu na bibi zake, ambayo baba yake hakuimalizia.



“Nafahamu baba alikufa kabla ya kumalizia mahari; niko tayari kuilipa Ni yema kutangaza kinachotokea kwani watu lazima wafahamu kwamba ni mimi nilimpa ujauzito, bila hivyo watasema ni mzinifu,” alisema Farai.

Lakini kiongozi wa kijiji hicho, Nathan Muputirwa, anasema: “Hatuwezi kuruhusu hili litokee kijijini kwetu, kwani hii ni dalili mbaya. Hapo zamani watu hawa walistahili kuuawa lakini leo hii hatuwezi kwa sababu tunaogopa polisi.”

Aliwaonya wawili hao wavunje ndoa yao au waondoke kwenye kijiji hicho ambapo walichagua uamuzi wa pili, na tangu hapo wameondoka kijijini hapo.
 
Sijui nini huwa kinabadili mawazo na usemi wa wazee.

Mb... Yako inasimama vipi kwa mama yako? Kivipi? Japo ni story ya mud mrefu lakini kiini cha haya yote ni mama.

Mpaka uoneshe paja, ndipo utakapo oneshwa mb...
 
Aman iwe nanyi wapendwa katika bwana

Tukio hili limetokea huko zimbambwe ambapo mama mmoja kwa jina la betty miaka 45 amefunga ndoa na mwanae farao 25 baada ya kumpa mimba

Mama huyo amedai ameanza kufanya mapenz na mwanae miaka mitatu iliyopita


Mama amedai kamuhangaikia sana huyo mwanae na kamsomesha kwa shida sana hivyo kwa sasa anafaid matunda yake


Mama huyo amedai hatak mwanae aowe mwanamke mwingine kwa sababu yeye ndo kamzaa hivyo ni lazima ale alichokihangaikia na kukizaa kwa uchungu wake


Kijana huyo miaka 25 amedai yuko mbion kwenda kwao na mama yake yaan kwa bibi na babu yake kutoa mahar ili amuoe mama yake huyo

Mwanamke huyo kwa sasa ana mimba ya miez sita hivyo kakalibia kujifungua mwanae ambae pia ni mjukuu wake

zim-marry.jpeg


LONDON BABY
 
Back
Top Bottom