Mama Anna Mghwira kama umeamua kula Haramu kula Iliyonona nakushauri Uchukue Kadi ya CCM

Waterloo

JF-Expert Member
Nov 30, 2010
25,356
38,914
Habari za muda wadau,
Nichukue fursa hii tena kwa Mara nyingine kumpongeza Mh.Anna Mghwira kuteuliwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.
Lengo la kuandika waraka huu mfupi ni kumshauri tu mama yangu Anna Mghwira kuchukua kadi ya Chama cha Mapinduzi ili aweze kutekeleza vizuri ilani ya Chama hicho.
Ninaeleza haya baada ya kustaajabu mama akisema yeye bado ni Mwenyekiti wa ACT nikajiuliza maswali mengi yaliyokosa majibu hasa nikizingatia leo amekabidhiwa ilani ya CCM.
Huu ni ushauri wa bure tu nakupa mama kwa manufaa yako kwa siku zijazo kisiasa. Haya madaraka yanapita lakini usisahau Historia itakuhumu.
Kila la Heri na Karibu sana Kilimanjaro.
 
Mwacheni Mama afanye kazi kwani maendeleo ya nchi hayaangali tofauti za Political Ideology.
 
Ni mtu mwenye upeo mdogo anaweza kuongea kama wewe. Kama maendeleo ya nchi hayaangalii tofauti za political ideology waambie CCM wapishe ikulu pale chadema waingie .wote si tuna lengo la kuwaletea wananchi maendeleo?
 
Akichukua kadi ya CCM ile " rarity value" yake itapotea!
Aliyemteua anataka atume meseji kuwa yeye ni mtu " inclusive", sasa mama akiingia CCM hilo halitakuwa achieved!
 
Hivi anaweza kama mwenyekiti wa ACT kuita press na kutoa maazimio ya chama chake kupinga utendaji wa serikali?
Haya ndio maswali ambayo wengi tunajiuliza na ndio maana tunashauri achukue kadi ya CCM.
 
Akichukua kadi ya CCM ile " rarity value" yake itapotea!
Aliyemteua anataka atume meseji kuwa yeye ni mtu " inclusive", sasa mama akiingia CCM hilo halitakuwa achieved!
Sasa hapa kituko atakua ni mama siyo aliyemteua. Sijui kama unanipata vizuri chief
 
2a5f36681d9a7ccd27ef5b1923ae2e63.jpg
 
Aichukue kadi ya ccm kutoka wapi? Kwani siyo mwanachama wa ccm? Labda umshauri ARUDISHE kadi ya act... Umemsikia raisi aliposema HACHAGUI wapinzani? Ulimwelewa?
Yeah. Hii inafikirisha. Sikuwa nimemwelewa aliposema hivyo. Halafu kamkabidhi ilani ya CCM kuitekeleza. Interesting!
 
Ni mtu mwenye upeo mdogo anaweza kuongea kama wewe. Kama maendeleo ya nchi hayaangalii tofauti za political ideology waambie CCM wapishe ikulu pale chadema waingie .wote si tuna lengo la kuwaletea wananchi maendeleo?
Nini maana ya Uchaguzi wewe mwenye Upeo Mkubwa?
 
Back
Top Bottom