BatteryLow
JF-Expert Member
- Aug 14, 2011
- 446
- 149
Mama mmoja alikuwa ameolewa na mwanamume wa Mwanza lakini wakawa wanaishi Dar alikokuwa anafanya kazi mume.
Mwaka 1992 wakakorofishana na mwanamke akaondoka kwa mumewe na watoto wadogo wawili, mmoja ana miaka mi4 na mdogo mwaka m1, na kuelekea kwao Moshi.
Miaka miwili baadae, mwanaume akaenda Moshi na kuchukua watoto wake wote wawili kwa nguvu na kuwapeleka kwao Mwanza akawaacha kwa bibi yao na yeye kurudi Dar kazini.
Yule baba baadae alikuja kufariki na wale watoto kwa vile walikulia kijijini na kwa bibi, hawakubahatika kusoma hivyo wakawa wanafanya vibarua hapa na pale.
Mwaka 2008, yule mdogo, wakati huo ana miaka 17, alimtafuta mama yake alipo mpaka akafanikiwa kufika Moshi alipokuwa mama yake.
Kafika nyumbani kwa mama na kupiga hodi:
Mtoto: Hodi;
Mama: Karibu. Mama akaenda kufungua mlango na kumkaribisha mgeni. "Karibu, karibu ndani.
Mtoto akaingia ndani, mama akamwambia karibu kiti , ninakuja.
Mama wakati huo alikuwa anapika huko chumbani, si unajua kule kijijini kuna chumba ndani ndio jiko. Mama kaendelea kupika huko ndani kama robo saa akatoka kuongea na mgeni (hapo mama alikuwa hajaonana na mtoto tangu ana mwaka mmoja na sasa ana 17).
Mama: Karibu, habari za wapi?
Mtoto: Nimetoka Mwanza nimekuja hapa Moshi kumtafuta mama yangu na nimeambiwa nikifika hapa kijijini niulizie jina la mzee ABC ndo atanionyesha kwa mama yangu.
Mama: Kwani ww unaitwa nani?
Mtoto: Naitwa XYZ! Yule mama alivyogundua ni mtoto wake alinyanyuka akashika mikono kichwani akaanza kulia.