Mama achoshwa aondoka na wanawe usiku wa manane

Mama achoshwa aondoka na wanawe usiku wa manane

KUNGURUHAFUGIKI

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2013
Posts
346
Reaction score
74
Ilikuwa saa tisa usiku mama mwenye nyumba mmoja alikuwa amelala akasikia mlango ukigongwa baada ya kufungua akamuona mwanamke mmoja walikuwa wanafahamiana nae akiwa na mizigo yake baada ya kumuuliza kulikoni ndo akawa anamsimulia kwamba wamezua ugomvi mkubwa sana na mumewe mpaka ikafikia achukue maamuzi magumu ya kuchukua wanawe wanne na kuondoka nao usiku huo huo na kuelekea kwa mama mwenye nyumba huyo , yule mwanamke anadai hata rudi tena kwa mmewe anasema kamvumilia sana na amechoka na manyanyaso ya mumewe akirudi kazini ni matusi na kipigo sio mara ya kwanza ,nimemsikitia sana yule mwanamke ukiangalia ana mtoto mdogo mchanga . Wakuu nimeshindwa kumshauri huyu mngekuwa nyinyi mngemshauri nini huyu mwanamke.
 
Mpe pole sana huyo mmama na watoto wake najua yuko under very hard time,we cha kufanya mfariji na umpe msaada unaomweza kumpa ila usije kuthubutu kuunga mkono wazo lake la kutoka kwa mumewe au kumshauri aombe na talaka,yaani kwa kifupi acha kushauri lolote kuhusu mapenzi yao maanake mambo ya wawili mmmmmmmhhhhh magumu mkuu yanaweza yakaja yakakugeuka mpaka usiamini kama ni wewe au la!!!!!!!!!!!!
 
Mmmh hapo pana kazi,
unatoka kwa mume unaenda kwa shosti
na watoto wanne dah, utaishije?

Unapoamua kuachana na mwanaume uwe umejipanga kweli kweli
la sivyo utaumbuka tu.

La kumshauri afanye kila hali arudi kwa mumewe,
huo mzigo kwake itakuwa ngumu sana kuumudu.
 
Nadhani chamsingi nikumpatia nauli akarudi kwao ndio itakua msaada mkubwa,watoto wa4 sio mchezo maisha haya bora aende kwao wazazi wake ndio watafanya mamuzi ya kumuita huyo mume wayamalize...
 
jamani kumbe watu wanabadilikaga tabia sanaa... yani mpaka mtoto wa nne ulikua wapi? sikio la kufa halisikii dawa... pole sana
 
Huyo kwangu ni mama bora si bora mama!mama ambaye nyumba imemshinda haachi watoto nyuma.pole sana tena sana!akae china na mumewe wayaongelee matatizo Yao watayamaliza tu!
 
Huyu mwanamke na mwanamme wote wanakazi serikalini na yule mwanamke anampango wa kupanga nyumba aishe na wanawe wote wanne .
 
Wewe ndio mama mwenyenyumba?
Mrudishe kwa mumewe, wakalee wote watoto na mumewe ashtakiwe kwa kumnyanyasa.
 
Back
Top Bottom