Hawa ndio baadhi ya Waanzilishi wa CCJ;
- Samuel Sitta (sh 500,000)
- Harrison Mwakyembe (sh 300,000)
- Anne Kilango (sh 400,000)
- James Lembeli (sh 400,000)
- Amina Katemi (sh 300,000)
- Alex Kisumo (sh 300,000)
- Baraka Seif (sh 300,000)
- Sospeter Banigwa (sh 300,000)
- Saleh Omari (sh 300,000)
- Asma Watosha (sh 300,000)
- Sarah Patrick (sh 200,000)
- Daniel Mwaijojeli (sh 200,000)
- Dk. Ngonyani (sh 300,000)
- Elisha Eliya (sh 200,000)
- Emanuel Magonja (sh 200,000)
- Hamad Ferej (sh 200,000)
- Gulam kutoka Zanzibar (sh 150,000)
- Innocent Makala (sh 200,000)
- Jacob Msambya (sh 200,000)
- Kipute (sh 200,000)
- Joseph Kashindye (sh 200,000)
- Kamala Ngombe (sh 200,000)
- Gumbo (sh 150,000)
- Ishelula (sh 150,000)
- Nape Nnauye (sh 100,000)
- Paul Makonda (sh 100,000)
- Hamadi Maduku (sh 100,000)
- Flavian Nkya (sh 100,000),
- Masudi Kangi (sh 100,000)
- Idd Kiriwe (sh 100,000)
- Kulwa Lulelema (sh 50,000)
- Ally Harun (sh 50,000)
- Daniel Malongo (sh 50,000).
Summary of Events
Nape, Kinana & Company (Team MEMBE??); "Rais Kateua Mawaziri Mizigo"
John Guninita (Team LOWASSA); "We Nape & Co. huna ubavu wa kumchagulia Rais Mawaziri"
Paul Makonda (Team ????); "Lowassa wacha kutuma watu (Kina Guninita) ili wawaseme vibaya Sekretariet na Viongozi wa Dini wakusaidie kupiga kampeni"
Richard Kiabo (Team LOWASSA); "Kwanza wewe Makonda na wenzio ndio mlioanzisha na kuchangia CCJ, na kiasi hiki ndicho mlichotoa, inafaa mshughulikiwe na Chama kwa kuendelea kushikilia kadi za CCJ"
John Malecela (Team ???); "Namuunga Mkono Paul Makonda, Nape na Kinana. Sekretariet imchukulie hatua Lowassa, na kama hajaanza mbio za Urais, hizi T-shirt za FRIENDS OF EDWARD LOWASSA za nini??"
Bakwata (Team LOWASSA??): "Makonda wacha kuwashirikisha waislamu kwenye Matatizo yenu, Pia usituchagulie marafiki"
tulia dawa ikuingieee,familia yenu ina mambo meng sna ya kujibu,vp ile hela jitu patel aliyomp mama yako iliwafunge harusi?vp ilikuwaje mzee malechela akabdilisha dini ali apate kuungwa mkono kwenye urais?vp ile milioni mia 6zilizo ibiwa wakat zinapelekwa dom ili zikamsaidie baba yako?vp ile familia ulioitelekeza nje?vp kuhusu kufanya editing kwwny picha ya rais na kuifnyia kinyago cha matusi?vp mbna nasikia ww ni bwabwa??tunaomba majib ya haya maswali???????
Mwee!
Baba Philipo aliyetelekezwa kwa mwendo wa Kasi Mpya, kisha akarejeshwa kundini kama suluhisho la uteuzi! Halafu akawapa miezi 6 magamba wajisalimishe, kisha akaishia kuwa msindikizaji na MC wa vikao vya Chama! Pole!
Mwenyekiti alishasema wanaoutaka uraisi waanze kujipitisha pitisha ... hii ndio style yenyewe ya kujipitisha
Yupo anawashughulikia walioingia CC kwa rushwa
Mkuu huyo unayemuulizia ni Analogy mambo ya Digital hayawezi. Sijui ata kama anajua kuna vitu vinaitwa mitandao ya kijamii? Maana ukimwangalia anatia huruma kwajinsi alivyokaa kama redio ya mkulima iliyoisha batter, maana amezungukwa na wajanja kila kona.
sasa hapa ni Mnyukano tu..., mbivu na mbichi zitajulikana kwa mtindo huu.
2016 NDIO MWISHO WA MALUMBANO HAYA,,,KIUKWELI SASA INACHOSHA,,,,,,
H@ki Ngowi: MWENYEKITI MWANZILISHI WA CCJ RICHARD KIABO AKANUSHA NAPE, MWAKYEMBE, SITTA NA MWAMBALASWA KUWA WAANZILISHI WA CHAMA HICHO KAMA INAVYODAIWA NA CHADEMA
Mweneyekiti mwanzilishi wa Chama Cha Jamii (CCJ)Richard Kiabo akizungumza na Waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kilumbe Ng'enda.Picha na Mdau Bashir Nkromo
------
Kutokana na uvumi na matamko mbalimbali kutoka kwa wanachama na baadhi ya wasemaji wa Chadema juu ya waanzilishi wa CCJ. Mimi niliyekuwa Mwenyekiti na mwanzilishi wa CCJ Taifa, napenda kufafanua kama ifuatavyo kuweka wazi jinsi na namna mbalimbali ilivyoabzishwa CCJ, pamoja na wale waliohusika hasa, tofauti na onavyotaka kupotoshwa.
A. KUANZIOSHWA KWA CCJ
Kirefu cha CCJ ni Chama Cha Jamii ambacho kilianzishwa na baadhi ya wananchi wa Tanzania. Chana hiki kilipata rasmi usajili wake wa muda, Machi 2, 2010.
Viongozi waanzilishi walikuwa ni:-
1. Ndugu Richard A. Kiyabo- Mwenyekiti Taifa
2. Ndugu Renatus Muabhi- Katibu Mkuu.
Kutokana na taratibu za usajili wa vyama vya siasa hapa nchini ilibidi tuanze harakati za kutafuta wanachama, tunashukuru kwamba Watanzania wengi walituunga mkono na hata kujiunga na chama chetu, na hatimaye kufikia kupata usajili wa muda, na miongoni mwa watu waliojiunga na chama chetu ni pamoja na Mh. Frederick Mpendazoe.
Mpendazoe alitaka awe Mwenyekiti wetu wa Taifa lakini hatukukubali ombi lake ambalo hakuliwakilisha kimaandishi bali kwa mdomo tu, lakini aliapishwa na chama kuwa msemaji wa CCJ.
Waheshimiwa ambao Mpendazoe anadai walikuwa waanzilishi wa CCJ, hoja hiyo ni ya utata mkubwa maana CCJ haikuwahi kuwa na waanzilishi wa aina hiyo yaani:-
1. Mh. Nape Nnauye
2. Mh. Harison Mwakyembe
3. Mh. Samwel Sitta na
4. Mh. Ezekiel Mwabalaswa
Swali la kumuuliza Mh. Mpendazoe ni je alipotangaza kutoka CCM waliompokea CCJ walikuwa hao aliowataja? na je wao walikuwa na nyadhifa zipi na kadi namba ngapi za uanachama? Je amesahau kuwa alinukuliwa na vyombo vya habari akimkaribisha Mh. Sitta kwamba ajiunge na CCJ? hilo atasemaje? Someni gazeti la Mwanachi, ISSN 0856-7573 Namba 03580 la April 6, 2010.
Napenda kuwakumbusha wanasiasa hasa wa Chadema kwamba siasa za udaku hazitawafikisha Ikulu, Watanzania ni waelewa na wala siyo mbumbumbu kama ambavyo Chadema wanajaribu kuonyesha.
Nawakumbusha kwamba Watanzania wamekua kisiasa ndiyo maana hawakuwaingiza IkuluChadema kwa kura zao. Kupigiwa makofi kwenye mikutano ya hadhara siyo kupewa kura kwenye chumba cha kupiga kura, Watanzania wanaelewa kwamba akili za kuambiwa kwenye mkutano changanya na zako kwenye chumba cha kupiga kura.
Nawashauri Mpendazoe na wenzake wa Chadema waache siasa za udaku, Watanzania wanataka kusikia sera za chama husika si udaku.
Wakiendelea na udaku wa kuwatuhumu watu kila kukicha mwisho tutaanza kuamini kwamba pengine hiyo ndiyo sera ya chama chao isiyo rasmi kimaandishi
Kama hawana la maana la kuwaambia wananchi ni bora wakanyamaza kuliko kuwahutubia wananchi uzushi tu kila kukicha.
B. CHADEMA NA HARAKATI ZA PEOPLES POWER
Chadema wameonyesha kuwa nguvu ya umma si kura tena, bali maandamano na vurugu zenye lengo la kuitoa serikali madarakani. wao wanajiita Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, ajabu wanayotenda siyo ya kidemokrasia tena bali ni kuwa sasa Chama chao ni cha maandamano na vurugu.
Je Wanaiheshimu kweli Demokrasia? Wakumbuke kwamba serikali iliyopo madarakani iliwekwa na Watanzania kwa kura zao sasa kwa nini hawawaheshimu Watanzania?
Wasidhani kwamba demokrasia ya kweli nchini ni mpaka Chadema ishinde uchaguzi. La Hasha! Demokrasia ni pamoja na kuheshimu maamuzi ya wananchi kwa njia ya kura zao.
Huu ni wakati wa kujengaa taifa letu tukishirikiana na Serikali yetu, na si wakati wa vurugu, maandamano kila kukicha, Watanzania tuwe makini na Wanasiasa wasio utakia mema utaifa wetu na amani ya nchi yetu.
Tukumbuke kwamba suala na amani ni sawa na nyanya, nyanya ikitumbuliwa kuishona tena haiwezekani. bila amani shughuli za kimaendeleo haziwezi kufanyika na hata shughuli zao wenyewe Chadema hawataweza kuzifanya.
Maisha ya wananchi kwa ujumla wake yanategemea amani katika nchi, hivyo sisi Watanzania hatuna budi kulipa kipaumbele suala la amani na maendeleo ya nchi yetu. Maneno yetu wanasiasa yawe ya kujenga na wala si ya kubomoa amani yetu, na tujifunze kuwa wakweli badala ya kuendekeza siasa za udaku.
MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
Richard A, Kiabo
Kada wa Chama Cha Mapinduzi
huyu richard kiabo wakati amerudi ccm alikana kuhusika kwa aliowataja sasa ktk waraka wake ktk uanzishwaji wa chama cha ccj, na aliwakashifu cdm na mpendanzoe kuwa ni wazushi na wanafiki. Leo anaibuka na kuwataja walewale aliokana mwanzo kuwa c waasisi wa ccj leo anasema ndio waasisi.je huyu mtu ni wa kuaminika? Uswahilini kwetu watu kama yeye tunawaita mal_y_ wa kisiasa. Kweli pesa ibilisi, yaani lowasa kanunua watu hadi wanajitoa ufahamu, hawajali kuonekana vituko ktk familia zao, jamii inayomzunguka,kwa wanasiasa wenzake na kwa watanzania kwa ujumla. Kweli siasa za uchumia tumbo zinadhalilisha sana, hivi kiabo haoni hata aibu jinsi anavyowadhalilisha watoto wake wenyewe na ukoo wake wa kiabo kwa ujumla? Historia itamhukumu, watoto na wajukuu zake wataona haya kujitambulisha kama wana nasaba na huyo mtu, jina la kiabo litajipambanua kama jina la kisaliti.
Hivi Anne Kilango na Mzee John Malecela walirudisha mabilioni ya jeetu patel? 1990 Mzee Malecela alipata mshiko toka uarabuni... Unahabari hii?- Kaka mbona hujaongelea Millioni 200 alizopewa Mbowe na Rostam na zile Millioni 100 alizopewa na Mkono, pole sana aibu siku hizi mnatakiwa kunyamaza tu!!
Le Mutuz