Malumbano CCM: Kiyabo amjibu Makonda

Malumbano CCM: Kiyabo amjibu Makonda

[/CENTER]
Mbele ya waandishi wa habari, Kiabo aliwataja waasisi hao wa CCJ na fedha walizochangia kwenye mabano kuwa ni pamoja na Dk. Harrison Mwakyembe (sh 300,000),
Samuel Sitta (sh 500,000),
Anne Kilango (sh 400,000),
Nape Nnauye (sh 100,000),
Paul Makonda (sh 100,000) na
James Lembel (sh 400,000) ambao kwa sasa ni miongoni mwa wanachama wa CCM wanaotajwa kuwa na makundi ya urais.


Wengine ni
Amina Katemi (sh 300,000),
Alex Kisumo (sh 300,000),
Baraka Seif (sh 300,000),
Sospeter Banigwa (sh 300,000),
Saleh Omari (sh 300,000),
Sarah Patrick (sh 200,000),
Daniel Mwaijojeli (sh 200,000),
Dk. Ngonyani (sh 300,000),
Elisha Eliya (sh 200,000),
Emanuel Magonja (sh 200,000) na
Asma Watosha (sh 300,000).

Pia wamo,
Kulwa Lulelema (sh 50,000),
Hamadi Maduku (sh 100,000),
Flavian Nkya (sh 100,000),
Gulam kutoka Zanzibar (sh 150,000),
Hamad Ferej (sh 200,000),
Ally Harun (sh 50,000),
Masudi Kangi (sh 100,000),
Gumbo (sh 150,000),
Idd Kiriwe (sh 100,000),
Innocent Makala (sh 200,000),
Jacob Msambya (sh 200,000),
Ishelula (sh 150,000),
Kipute (sh 200,000),
Joseph Kashindye (sh 200,000)
Kamala Ng’ombe (sh 200,000) na
Daniel Malongo (sh 50,000).


NAPE ANA KADI MBILI?

Cc, Ritz, Nape,
 
Sasa huu sio mpasuko ndani ya chama bali ni kupasuana tu. Kazi kweli kweli...
 
mbombo jinogile.....kama nao wanaweza wajaribu kuwatoa mamluki hao ndani ya chama,they need to learn more from chadema to take sameone out who want to destroy institution!!
 
Hivi watu wanadhani kuanzisha chama cha siasa ni lelemama e?

Yaani Nape alidhani ataanzisha chama cha siasa kwa laki moja? Au Sitta alidhani laki 5 zinaanzisha chama kikawa chama?

Wasinichekeshe...
Kuna jamaa mwingine naye yuko uchochoroni kwa sasa wanamdanganya anaweza kuanzisha chama kupingana na chama makini. Sasa awaulize wenzie walishindwa nini?
 
Mzee Philipu Mangula uko wapi mbona kimya? Hebu wakemee hawa wanaojifanya miamba ya kupasho wanakuharibia sifa ya chama chako. Maana katika viongozi wewe ndiye mkongwe.
Mwee!

Baba Philipo aliyetelekezwa kwa mwendo wa Kasi Mpya, kisha akarejeshwa kundini kama suluhisho la uteuzi! Halafu akawapa miezi 6 magamba wajisalimishe, kisha akaishia kuwa msindikizaji na MC wa vikao vya Chama! Pole!
 
Hawa mimi nawajuwa vyema, nchi ilisimama miaka miwili kwa ulaghai wa Sitta na Mwakyembe, finally Obama amekuja kuibariki Richmond na sasa tunawalipa Wamarekani.

Harusi ya Malecela na Anne Kilango Jeetu Patel aliwapa milioni 200 hawa wanafki wazazi wa Le Mutuz, na kinachomuuma huyu hopeless oldman ni Anne Kilango kupigwa chini na Sofia Simba UWT sasa anadhani watanzania ni mazuzu wa kulishwa chuki zao binafsi, tunajitambuwa vizuri sana.

Hii familia ya Malecela ni political losers family.

- Kaka mbona hujaongelea Millioni 200 alizopewa Mbowe na Rostam na zile Millioni 100 alizopewa na Mkono, pole sana aibu siku hizi mnatakiwa kunyamaza tu!!

Le Mutuz
 
Kuna jamaa mwingine naye yuko uchochoroni kwa sasa wanamdanganya anaweza kuanzisha chama kupingana na chama makini. Sasa awaulize wenzie walishindwa nini?

- Chama makini kinachopokea Rushwa za rostam na Mkono ndio unaita chama makini?

Le Mutuz
 
- Kaka mbona hujaongelea Millioni 200 alizopewa Mbowe na Rostam na zile Millioni 100 alizopewa na Mkono, pole sana aibu siku hizi mnatakiwa kunyamaza tu!!

Le Mutuz

Na zile Milion 200,000 alizopewa Baba yako na Jeet Patel za Mchango wa Harusi unasemaje?
 
Lakini hat yy ni msaliti coz alikuwa ccj kama akina sita so hakuna cha ajabu
 
2016 NDIO MWISHO WA MALUMBANO HAYA,,,KIUKWELI SASA INACHOSHA,,,,,,

H@ki Ngowi: MWENYEKITI MWANZILISHI WA CCJ RICHARD KIABO AKANUSHA NAPE, MWAKYEMBE, SITTA NA MWAMBALASWA KUWA WAANZILISHI WA CHAMA HICHO KAMA INAVYODAIWA NA CHADEMA


Mweneyekiti mwanzilishi wa Chama Cha Jamii (CCJ)Richard Kiabo akizungumza na Waandishi wa habari mjini Dar es Salaam, leo. Kulia ni Katibu wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Kilumbe Ng'enda.Picha na Mdau Bashir Nkromo
------

Kutokana na uvumi na matamko mbalimbali kutoka kwa wanachama na baadhi ya wasemaji wa Chadema juu ya waanzilishi wa CCJ. Mimi niliyekuwa Mwenyekiti na mwanzilishi wa CCJ Taifa, napenda kufafanua kama ifuatavyo kuweka wazi jinsi na namna mbalimbali ilivyoabzishwa CCJ, pamoja na wale waliohusika hasa, tofauti na onavyotaka kupotoshwa.



A. KUANZIOSHWA KWA CCJ
Kirefu cha CCJ ni Chama Cha Jamii ambacho kilianzishwa na baadhi ya wananchi wa Tanzania. Chana hiki kilipata rasmi usajili wake wa muda, Machi 2, 2010.



Viongozi waanzilishi walikuwa ni:-
1. Ndugu Richard A. Kiyabo- Mwenyekiti Taifa
2. Ndugu Renatus Muabhi- Katibu Mkuu.



Kutokana na taratibu za usajili wa vyama vya siasa hapa nchini ilibidi tuanze harakati za kutafuta wanachama, tunashukuru kwamba Watanzania wengi walituunga mkono na hata kujiunga na chama chetu, na hatimaye kufikia kupata usajili wa muda, na miongoni mwa watu waliojiunga na chama chetu ni pamoja na Mh. Frederick Mpendazoe.
Mpendazoe alitaka awe Mwenyekiti wetu wa Taifa lakini hatukukubali ombi lake ambalo hakuliwakilisha kimaandishi bali kwa mdomo tu, lakini aliapishwa na chama kuwa msemaji wa CCJ.


Waheshimiwa ambao Mpendazoe anadai walikuwa waanzilishi wa CCJ, hoja hiyo ni ya utata mkubwa maana CCJ haikuwahi kuwa na waanzilishi wa aina hiyo yaani:-
1. Mh. Nape Nnauye
2. Mh. Harison Mwakyembe
3. Mh. Samwel Sitta na
4. Mh. Ezekiel Mwabalaswa


Swali la kumuuliza Mh. Mpendazoe ni je alipotangaza kutoka CCM waliompokea CCJ walikuwa hao aliowataja? na je wao walikuwa na nyadhifa zipi na kadi namba ngapi za uanachama? Je amesahau kuwa alinukuliwa na vyombo vya habari akimkaribisha Mh. Sitta kwamba ajiunge na CCJ? hilo atasemaje? Someni gazeti la Mwanachi, ISSN 0856-7573 Namba 03580 la April 6, 2010.


Napenda kuwakumbusha wanasiasa hasa wa Chadema kwamba siasa za udaku hazitawafikisha Ikulu, Watanzania ni waelewa na wala siyo mbumbumbu kama ambavyo Chadema wanajaribu kuonyesha.


Nawakumbusha kwamba Watanzania wamekua kisiasa ndiyo maana hawakuwaingiza IkuluChadema kwa kura zao. Kupigiwa makofi kwenye mikutano ya hadhara siyo kupewa kura kwenye chumba cha kupiga kura, Watanzania wanaelewa kwamba akili za kuambiwa kwenye mkutano changanya na zako kwenye chumba cha kupiga kura.
Nawashauri Mpendazoe na wenzake wa Chadema waache siasa za udaku, Watanzania wanataka kusikia sera za chama husika si udaku.


Wakiendelea na udaku wa kuwatuhumu watu kila kukicha mwisho tutaanza kuamini kwamba pengine hiyo ndiyo sera ya chama chao isiyo rasmi kimaandishi
Kama hawana la maana la kuwaambia wananchi ni bora wakanyamaza kuliko kuwahutubia wananchi uzushi tu kila kukicha.


B. CHADEMA NA HARAKATI ZA PEOPLES POWER
Chadema wameonyesha kuwa nguvu ya umma si kura tena, bali maandamano na vurugu zenye lengo la kuitoa serikali madarakani. wao wanajiita Chama Cha Demokrasia na Maendeleo, ajabu wanayotenda siyo ya kidemokrasia tena bali ni kuwa sasa Chama chao ni cha maandamano na vurugu.


Je Wanaiheshimu kweli Demokrasia? Wakumbuke kwamba serikali iliyopo madarakani iliwekwa na Watanzania kwa kura zao sasa kwa nini hawawaheshimu Watanzania?
Wasidhani kwamba demokrasia ya kweli nchini ni mpaka Chadema ishinde uchaguzi. La Hasha! Demokrasia ni pamoja na kuheshimu maamuzi ya wananchi kwa njia ya kura zao.
Huu ni wakati wa kujengaa taifa letu tukishirikiana na Serikali yetu, na si wakati wa vurugu, maandamano kila kukicha, Watanzania tuwe makini na Wanasiasa wasio utakia mema utaifa wetu na amani ya nchi yetu.


Tukumbuke kwamba suala na amani ni sawa na nyanya, nyanya ikitumbuliwa kuishona tena haiwezekani. bila amani shughuli za kimaendeleo haziwezi kufanyika na hata shughuli zao wenyewe Chadema hawataweza kuzifanya.



Maisha ya wananchi kwa ujumla wake yanategemea amani katika nchi, hivyo sisi Watanzania hatuna budi kulipa kipaumbele suala la amani na maendeleo ya nchi yetu. Maneno yetu wanasiasa yawe ya kujenga na wala si ya kubomoa amani yetu, na tujifunze kuwa wakweli badala ya kuendekeza siasa za udaku.

MUNGU IBARIKI AFRIKA, MUNGU IBARIKI TANZANIA
Richard A, Kiabo
Kada wa Chama Cha Mapinduzi
 
- The mburulazzz kama kweli Lowassa anafanyiwa kampeni za urais na watu kama huyu basi ndio maana hatakuwa, what is this? Hili tu ndio tatizo kubwa la Kambi ya Lowassa ni kuamini kwamba wanaweza kutumia ubabe na pesa kuapta urais what is CCJ? Kwani kuanzisha CCJ kama ni kweli ilikuwa a Crime against the State? au ilikuwa a Crime aganist CCM?

- I mean nyie watu wa Lowassa kama kweli mnataka Urais mnatakiwa kuachana na wajinga wajinga kama huyu mtu, so haya ndio majibu ya Ile hotuba ya Makonda? Kweli yale maneno ya Makonda unaweza kuyajibu na foolishness kama hizi?

Le Mutuz

tulia dawa ikuingieee,familia yenu ina mambo meng sna ya kujibu,vp ile hela jitu patel aliyomp mama yako iliwafunge harusi?vp ilikuwaje mzee malechela akabdilisha dini ali apate kuungwa mkono kwenye urais?vp ile milioni mia 6zilizo ibiwa wakat zinapelekwa dom ili zikamsaidie baba yako?vp ile familia ulioitelekeza nje?vp kuhusu kufanya editing kwwny picha ya rais na kuifnyia kinyago cha matusi?vp mbna nasikia ww ni bwabwa??tunaomba majib ya haya maswali???????
 
- Kaka mbona hujaongelea Millioni 200 alizopewa Mbowe na Rostam na zile Millioni 100 alizopewa na Mkono, pole sana aibu siku hizi mnatakiwa kunyamaza tu!!

Le Mutuz

w .j malekela,, ha ha haaaaaa ,,!! Hivi na wewe ni msomi??
 
tulia dawa ikuingieee,familia yenu ina mambo meng sna ya kujibu,vp ile hela jitu patel aliyomp mama yako iliwafunge harusi?vp ilikuwaje mzee malechela akabdilisha dini ali apate kuungwa mkono kwenye urais?vp ile milioni mia 6zilizo ibiwa wakat zinapelekwa dom ili zikamsaidie baba yako?vp ile familia ulioitelekeza nje?vp kuhusu kufanya editing kwwny picha ya rais na kuifnyia kinyago cha matusi?vp mbna nasikia ww ni bwabwa??tunaomba majib ya haya maswali???????

Duu! Ndo yamekuwa hayo? JF chiboko! Watu mna data nyie!!!!
 
- Kaka mbona hujaongelea Millioni 200 alizopewa Mbowe na Rostam na zile Millioni 100 alizopewa na Mkono, pole sana aibu siku hizi mnatakiwa kunyamaza tu!!

Le Mutuz

Kwahiyo unakubali baba yako alihongwa million 200 na Jeetu Patel? Labda tuanzie hapo kwanza swali huwa alijibiwi kwa swali bali wananchi wanahitaji majibu ya swali langu kwanza.
 
SIKU moja baada ya Umoja wa Vijana wa CCM
(UVCCM) kutoa tamko la kumtaka aliyekuwa
Waziri Mkuu, Edward Lowassa, kuacha
kukigawa chama kwa madai kuwa hana sifa
kuwa rais, mambo mazito yamezidi kuibuka
huku ikitolewa orodha ya wanachama wa CCM
wakiwemo mawaziri, wabunge na makada
maarufu wanaodaiwa kukisaliti chama hicho.
Hatua hiyo imeenda sambamba na kumtaka
Katibu wa Umoja wa Vijana Uhamasishaji na
Chipukizi, Paul Makonda, kuacha
kuwanyooshea vidole wenzao, wakati ndani ya
chama hicho kuna wasaliti wakubwa na
wasiokuwa na usafi wowote wa kuwasema
wenzao.
Hayo yamewekwa hadharani Dar es Salaam
jana na aliyekuwa Mwenyekiti na mwanzilishi
wa CCJ Taifa, Richard Kiyabo, wakati
akizungumza na waandishi wa habari kwenye
ukumbi wa mikutano Idara ya Habari
(MAELEZO).
Kiyabo aliitaka CCM kusafisha wanachama
wasio waaminifu ambao ni mamluki wakiwemo
mawaziri, wabunge machachari na makada
maarufu kutokana na kushiriki kwao kuanzisha
Chama Cha Kijamii (CCJ) huku bado
hawajarejesha kadi za chama hicho.
Kiyabo alisambaza kwa waandishi wa habari
orodha ya wanachama wa CCM 37 anaodai
walishiriki kutoa michango ya fedha kwa ajili ya
kufanikisha maandamano ya amani ya CCJ
yaliyolenga kupinga uonevu wa msajili wa
vyama vya siasa nchini.
Alisema tayari ameshamwandikia barua
Makamu Mwenyekiti wa CCM (Bara) Philip
Mangula kukiomba chama kichukue hatua za
kinidhamu na kimaadili kwa wanachama ambao
si waaminifu na tayari walikwishapoteza sifa za
kuwa wanachama, kutokana na kushirikiana
nao kuanzisha CCJ, huku wakiwa wanachama
wa CCM.
"Kitendo cha kuwa wanachama wa vyama viwili
kwa wakati mmoja ni kosa kubwa na ni usaliti
ndani ya chama, kosa hili halipishani na kosa
la uhaini ndani ya chama, lakini kwa masikitiko
yangu makubwa watu hawa hadi sasa
hawajaitwa na vikao vya chama wala hakuna
hatua yoyote iliyochukuliwa au kujadiliwa kwa
makosa ya kukisaliti chama na kuamua kuwa
mamluki ndani ya chama," alisema Kiyabo.
Alisema mwanzoni mwa mwaka 2010
walipokubaliana kuanzisha CCJ malengo makuu
ilikuwa chama hicho kushiriki uchaguzi mkuu
na kusimamisha mgombea wa kiti cha urais na
wabunge, pamoja na madiwani kama
wangekidhi matakwa ya kisheria.
"Nashangaa ndani ya CCM bado kuna
wanachama na viongozi waandamizi wana kadi
mbili za CCJ na CCM na wanashindwa
kuzirudisha na hata kukana, ikiwemo
kuwaomba radhi wanachama kwa kitendo cha
usaliti," alisema na kuongeza kuwa
anawashangaa baadhi ya wanachama ambao si
waaminifu ndani ya chama.
Mbele ya waandishi wa habari, Kiabo aliwataja
waasisi hao wa CCJ na fedha walizochangia
kwenye mabano kuwa ni pamoja na Dk.
Harrison Mwakyembe (sh 300,000), Samuel
Sitta (sh 500,000), Anne Kilango (sh 400,000),
Nape Nnauye (sh 100,000), Paul Makonda (sh
100,000) na James Lembel (sh 400,000) ambao
kwa sasa ni miongoni mwa wanachama wa
CCM wanaotajwa kuwa na makundi ya urais.
Wengine ni Amina Katemi (sh 300,000), Alex
Kisumo (sh 300,000), Baraka Seif (sh 300,000),
Sospeter Banigwa (sh 300,000), Saleh Omari (sh
300,000), Sarah Patrick (sh 200,000), Daniel
Mwaijojeli (sh 200,000), Dk. Ngonyani (sh
300,000), Elisha Eliya (sh 200,000), Emanuel
Magonja (sh 200,000) na Asma Watosha (sh
300,000).
Pia wamo, Kulwa Lulelema (sh 50,000), Hamadi
Maduku (sh 100,000), Flavian Nkya (sh
100,000), Gulam kutoka Zanzibar (sh 150,000),
Hamad Ferej (sh 200,000), Ally Harun (sh
50,000), Masudi Kangi (sh 100,000), Gumbo (sh
150,000), Idd Kiriwe (sh 100,000), Innocent
Makala (sh 200,000), Jacob Msambya (sh
200,000), Ishelula (sh 150,000), Kipute (sh
200,000), Joseph Kashindye (sh 200,000)
Kamala Ng’ombe (sh 200,000) na Daniel
Malongo (sh 50,000).
Alisema ni vyema wakati huu kuelekea uchaguzi
CCM ianze kujisafisha ili wale mamluki
waumbuke na wasipewe nafasi ya kugombea
wakati ukifika
Makonda alipoulizwa kuhusiana na madai hayo
alijibu kuwa anaelewa kuwa mchezo huo
unachezwa na vibaraka kwani suala hilo halina
uzito ndani ya chama.
Alidai kuwa suala la kuondoa watu
wanaotumiwa na Lowassa kukihujumu chama
hicho halijibiwi. Alisema ni muhimu kuelewa
kuwa wapambe wote wa Lowassa watatoka na
watakapomalizika atashughulikiwa yeye
kichama kwani ndiye tatizo.
“Wapambe wote watoke na watakapoisha
tutashughulika na bosi wao anayewatuma...
ninajua hawajajipanga ndiyo maana
wamekurupuka na kuja na hoja rahisi," alisema.
Alisema wanamtaka Lowassa akanushe
kuwatumia hao watu. Kwa Nape, alisema
yalishajadiliwa na mjadala kufungwa ndani ya
chama, hivyo madai hayo si mapya hawezi
kuyazungumzia.
 
Back
Top Bottom