Bikirajohola
JF-Expert Member
- Jun 11, 2022
- 356
- 634
Wafanya biashara wa mahindi wamejikuta kwenye wakati mgumu sana kwenye mpaka wa Tanzania na Kenya baada ya kuambiwa vibali vyao vimeisha lakini hata baada ya kununua vibali vipya mtandaoni bado viongozi wa wizara huku Tanzania hawapokei simu kwa siku nne sasa na kupelekea msululu wa malori mengi sana hapo mpakani.
====
HOLILI: MALORI YA MAZAO ZAIDI YA 40 YAKWAMA MPAKA WA KENYA
Wafanyabiashara wa mazao wanadaiwa kuwa katika wakati mgumu mpakani mwa Tanzania na Kenya baada ya kuambiwa vibali vya kuvusha bidhaa hiyo nchi jirani kumalizika muda wake
Inaelezwa hata baada ya kununua vibali vipya kwa njia ya mtandao hawakufanikiwa kuendelea na safari na hivyo wamewatupia lawama Mamlaka za Mpakani hapo kwa kutokuwapa ushirikiano na kupelekea adha ya msongamano wa malori
Kuhusu hilo, Waziri wa Kilimo, Hussein Bashe amesema "Wengi wao hawana kibali cha kutoa mazao nje ya nchi licha ya utaratibu kujulikana. Hatuzuii biashara lakini kuwe na utaratibu, tunafanya mpango kuwasaidia wapate vibali lakini wanatakiwa kupata kabla ya kufika mpakani"
#JamiiForums