KERO Kero ya madereva malori: Wawekezaji walia hasara

KERO Kero ya madereva malori: Wawekezaji walia hasara

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua

Albeity93

New Member
Joined
Oct 12, 2015
Posts
2
Reaction score
4
Habari,

Kuna kero kubwa sana inayozidi kuongezeka kwenye sekta ya usafirishaji hapa Tanzania, hususan kwa madereva wa malori makubwa.

Kama transporter, serikali inaweka masharti makubwa kuhakikisha madereva wana leseni na vibali vinavyohitajika ili kusafirisha mizigo mbalimbali, ikiwemo kemikali. Wawekezaji nao wanawekeza mabilioni ya fedha kununua magari na kuyaweka barabarani kwa kufuata sheria zote.

Lakini changamoto kubwa ipo kwa baadhi ya madereva. Wanasababisha ucheleweshaji mkubwa wa safari, hawaendeshi magari kwa uangalifu, huacha magari njiani bila utaratibu, huiba mafuta, hupoteza au kuharibu magari na mizigo. Mwishowe, gharama zote hizi hubebwa na mwekezaji. Analazimika kutuma dereva mwingine, kukabiliana na adhabu au makato kutoka kwa mteja, na kugharamia matengenezo au hasara nyingine.

Cha kusikitisha ni kwamba mara nyingi dereva anayesababisha matatizo haya huondoka tu na kwenda kuajiriwa kwenye kampuni nyingine kana kwamba hakuna kilichotokea.

Naamini ni wakati sasa wa taasisi kama TATOA, kwa kushirikiana na wadau wengine wa sekta, kuweka mfumo madhubuti wa kuwawajibisha madereva wanaojihusisha na vitendo hivi. Bila hatua za pamoja, wawekezaji wataendelea kubeba hasara kubwa huku nidhamu kwenye sekta ikiendelea kudorora.
 
Wapeni mikataba ya kazi/ajira/Benefits zao zingine.
Kazi ni kipimo cha utu
 
Wapeni mikataba ya kazi/ajira/Benefits zao zingine.
Kazi ni kipimo cha utu
Kama hupo sekta binafsi, huwezi kujua madhira ya ajira ya sekta binafsi ambapo wafanyakazi na mikata ya ajira anaacha kazi na kuhamia kwingine bila hata kutoa notice ya dakika moja; mikataba linapokuja suala la Mwajiriwa haufanyi kazi.

Utaambia gari halijawashwa, kupiga simu haipatikani. Mkataba unasema ukiamua kuacha kazi kwa 24hrs unalipa mshahara wa mwezi lakini mwajiri hawezi ku enforce hii. Ila wewe ukimfukuza kazi anaenda CMA. Kama andiko lilivyo, anaonewa Mwajiri tu. Hana pa kukimbilia.
 
Sio madereva tu, kuajiri vijana wa sasa ni changamoto sekta zote.
 
Je mnawalipa kwa wakati?,mshahara mzuri?,posho je,bima ya afya je?
 
Back
Top Bottom