Malkia Vashti chanzo cha kiburi kwa wanawake duniani

eden kimario umekisoma vizuri kitabu cha "wimbo ulio bora" cha Mfalme suleimani!?.. Ukakijua kiliundwaje na kwanini!?🙂
Hiki ninavyokielewa ni kitabu kinachozungumzia urafiki, upendo, mapenzi, kati ya mume na mke
Inasemekana Solomon ndie alieandika
Lakini ukija kwenye dini wanadai kinazungumzia upendo uliopo kati ya Mungu na watu wake
 
Kitabu hiki cha wimbo ulio bora mimi sijawahi kukichukulia kama kitabu cha Mungu ila kitabu kinachokufundisha namna ya kumsifia mkeo kwa mwanaume na mwanamke namna ya kumsifia mumewe
Halafu ukizingatia katika israel zama hizo za mfalme Solomon jambo la kuzungumzia mapenzi halikuwa na aibu hata kidogo
 
Esta ndio moja ya vitabu pekee Mungu hajaongelewa ndani yake!. Na Esta kuwaokoa kutoka kuuliwa wayahudi wote kwa kuweka decree wajilinde ndio ikatokea sikukuu ya kiyahudi wanaiadhimisha hadi leo.
Movie ya 300 rising ndio imemuongelea zaidi huyu Xerxes.
cc: Da'Vinci
Unataka kusema Easter inatokana na Esta?
Mimi najua Easter kwa lugha nzuri ni Siku kuu ya Passover ambayo chanzo chake ni ile harakati za kuokolewa Wayahudi mikononi mwa Farao.

Ilitokana na amri ya Mungu kuagiza kila nyumba ya mwana Israel ipakwe damu mlangoni kisha usiku Mungu alituma malaika wake kuangamiza kila mzaliwa wa kwanza wa wamisri ikiwa kama adhabu ya ukaidi wa Farao kutowaachia waisrael.

Ile damu mlangoni ilikuwa ishara ya kutambulisha nyumba ya waisrael wasijekuguswa na pigo hilo la Mungu.
 
We kufa tu ni haki yako mkuu kikatiba, Kijamii na kidini!.. Unadhani nitakubishia basi!?..
Ila tambua kwa ubishi wako, kuna elimu kibao utazikosa!. Leo unaamini Adam na Eva ndio watu wa kwanza, nikiuliza
  • Uovu Kaini alijifunzia wapi utanijibu?..
  • kwanini Kaini aliomba ulinzi wa Mungu wa mataifa wakimuona wasije wakamuua?.
  • Je hao wa Mataifa walitoka wapi ikiwa walizaliwa yeye na Abeli tu wakubwa!?.
  • Kwanini shetani alimtumia nyoka toka viumbe vyote utanijibu!?.
  • Kwanini Mungu aliweka mti ikiwa anajua Adam angekuja kaidi utanijibu!?.
Biblia ndani yake ina story za kusadikika, ushawahi sikia au ona Punda kaongea!?, Mungu alipopigwa na Yakobo nguvu zake aliacha wapi!?..
Kufa tu sitakuzuia mkuu!.
Mkuu inaonekana unafahamu mengi sana, sisi wengine hatujui hayo maana maarifa yetu tumeyaelekeza kwenye eneo jingine kabisa.... tusaidie kutujuza majibu ya hayo maswali uliyoyaainisha hapo.
 
Unataka kusema Easter inatokana na Esta?
Mimi najua Easter kwa lugha nzuri ni Siku kuu ya Passover ambayo chanzo chake ni ile harakati za kuokolewa Wayahudi mikononi mwa Farao.

Ilitokana na amri ya Mungu kuagiza kila nyumba ya mwana Israel ipakwe damu mlangoni kisha usiku Mungu alituma malaika wake kuangamiza kila mzaliwa wa kwanza wa wamisri ikiwa kama adhabu ya ukaidi wa Farao kutowaachia waisrael.

Ile damu mlangoni ilikuwa ishara ya kutambulisha nyumba ya waisrael wasijekuguswa na pigo hilo la Mungu.
Kabisa na kristo pia alikufa siku ya pasaka ya wayahudi ili kuunganisha hapo kuwa ni kitu kilekile
 
Unataka kusema Easter inatokana na Esta?
Mimi najua Easter kwa lugha nzuri ni Siku kuu ya Passover ambayo chanzo chake ni ile harakati za kuokolewa Wayahudi mikononi mwa Farao.

Ilitokana na amri ya Mungu kuagiza kila nyumba ya mwana Israel ipakwe damu mlangoni kisha usiku Mungu alituma malaika wake kuangamiza kila mzaliwa wa kwanza wa wamisri ikiwa kama adhabu ya ukaidi wa Farao kutowaachia waisrael.

Ile damu mlangoni ilikuwa ishara ya kutambulisha nyumba ya waisrael wasijekuguswa na pigo hilo la Mungu.
Umenielewa vibaya!.
Esther/Esta linamaanisha “Nyota/Star” na jina lake la kiyahudi aliitwa "Hadassah".
Sherehe wanayoiadhimisha wayahudi inaitwa " Purim" wanaiadhimisha kila tarehe 14 ya mwezi wao.
Story ilikua hivi baada ya Haman kuchaguliwa kuwa waziri mkuu, akataka watu wote wamsujudie, lakini Mordeci ambaye alikuwa kabila ya benjamin (myahudi) aligoma msujudia binadamu mwenzie (Haman). Taarifa zilipomfikia Haman akachukia sana, akataka kumuua Mordecai ila kwa hasira akataka awapoteze na familia nzima.
Atafanikiwaje?, akamwambia Mfalme niruhusu niwaue na kila hela ya kuua myahudi itaingia kwako. Mfalme akakubali na sheria ikapita kila myahudi tarehe 14 popote alipo anatakiwa auliwe toka watoto-wazee.
Ikabidi Esta alete mgomo wa kula ili aweze onana na mfalme (kumbuka hapo Esta kaolewa lakini kwa siku 30 hajaitwa kulala na mfalme wala kuonana nae). Habari zilipomfikia Mfalme kua Malkia wake hali akamuita ndio Esta kwenda eleza kisa.
Kwa vile kwa tamaduni zao sheria ikiwekwa hata mfalme hawezi ivunja ikabidi mfalme atoe pete yake (saini) akampa Esta aende jua atawasaidiaje watu wake (wayahudi). Na Esta asingeweza kuinullify sheria akaunda nyingine "kila myahudi tarehe 14 ajilinde asiuliwe".
Siku ya Mauaji kufika zikawepo sheria mbili huku waue kule jilindeni!. Wayahudi wakashinda hawakuuliwa!. Ndio kila mwaka wakawa wanaadhimisha kupona kwao.
Sherehe ya Purim.
 
Hapa nimekuelewa vizuri
 
Kitabu hiki cha wimbo ulio bora mimi sijawahi kukichukulia kama kitabu cha Mungu ila kitabu kinachokufundisha namna ya kumsifia mkeo kwa mwanaume na mwanamke namna ya kumsifia mumewe
Halafu ukizingatia katika israel zama hizo za mfalme Solomon jambo la kuzungumzia mapenzi halikuwa na aibu hata kidogo
Kwa lugha simple hiyo ni mitongozo ya mfalme kwa mahawara wake alokuwa akiwaona!.. Mostly hakuwa anatumia cheo kuwaita chumbani, anawatungia shairi wanaenda imbiwa!🙂.
 
Mkuu inaonekana unafahamu mengi sana, sisi wengine hatujui hayo maana maarifa yetu tumeyaelekeza kwenye eneo jingine kabisa.... tusaidie kutujuza majibu ya hayo maswali uliyoyaainisha hapo.
Mkuu mimi na kuanzisha Uzi ni mvivu unless niwe kwenye hype zangu, lakini napenda kuta kama hivi ndio tuujadili!.. Kuna huyu jamaa zitto junior ndio ana ujuzi mkubwa halafu yupo vizuri kuzianzishia nyuzi hizi mambo!.
 
huwa napenda sana nondo kama hizi, nimekuweka kwenye list ya watu ninaowasoma sana humu Jf
 
Kwa lugha simple hiyo ni mitongozo ya mfalme kwa mahawara wake alokuwa akiwaona!.. Mostly hakuwa anatumia cheo kuwaita chumbani, anawatungia shairi wanaenda imbiwa!🙂.
Sikubishii maana alikuwa nao zaidi ya elfu moja
 
Ata Kaini niemuuaji wa kwanza Duniani.
1 Adamu akamjua Hawa mkewe; naye akapata mimba, akamzaa Kaini, akasema, Nimepata mtoto mwanamume kwa Bwana.
2 Akaongeza akamzaa ndugu yake, Habili. Habili alikuwa mchunga kondoo, na Kaini alikuwa mkulima ardhi.
3 Ikawa hatimaye Kaini akaleta mazao ya ardhi, sadaka kwa Bwana.
4 Habili naye akaleta wazao wa kwanza wa wanyama wake na sehemu zilizonona za wanyama. Bwana akamtakabali Habili na sadaka yake;
5 bali Kaini hakumtakabali, wala sadaka yake. Kaini akaghadhibika sana, uso wake ukakunjamana.
6 Bwana akamwambia Kaini, Kwa nini una ghadhabu? Na kwa nini uso wako umekunjamana?
7 Kama ukitenda vyema, hutapata kibali? Usipotenda vyema dhambi iko, inakuotea mlangoni, nayo inakutamani wewe, walakini yapasa uishinde.
8 Kaini akamwambia Habili nduguye, [Twende uwandani]Ikawa walipokuwapo uwandani,Kaini akamwinukia Habili nduguye,akamwua.
9 Bwana akamwambia Kaini, Yuko wapi Habili ndugu yako? Akasema, Sijui, mimi ni mlinzi wa ndugu yangu?
10 Akasema, Umefanya nini? Sauti ya damu ya ndugu yako inanililia kutoka katika ardhi.
11 Basi sasa, umelaaniwa wewe katika ardhi, iliyofumbua kinywa chake ipokee damu ya ndugu yako kwa mkono wako;
12 utakapoilima ardhi haitakupa mazao yake; utakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani.
13 Kaini akamwambia Bwana, Adhabu yangu imenikulia kubwa, haichukuliki.
14 Tazama, umenifukuza leo katika uso wa ardhi, nitasitirika mbali na uso wako, nami nitakuwa mtoro na mtu asiye na kikao duniani; hata itakuwa kila anionaye ataniua.
15 Bwana akamwambia, Kwa sababu hiyo ye yote atakayemwua Kaini atalipizwa kisasi mara saba. Bwana akamtia Kaini alama, mtu amwonaye asije akampiga.
16 Kaini akatoka mbele za uso wa Bwana, akakaa katika nchi ya Nodi, mbele ya Edeni.
 
Back
Top Bottom