Malkia Vashti chanzo cha kiburi kwa wanawake duniani

Malkia Vashti chanzo cha kiburi kwa wanawake duniani

Ahsanteni nyote kwa maoni yenu!
Me ninapita!
Kwangu Mimi,kusoma ni BORA kuliko KUANDIKA! Hasa Yale nisiyo na hakika ama ujuzi nayo.Ahsanteni.Nimejifunza yenye maana!
 
Mkuu hujui kuwa Hamani aliuwawa kwa kutundikwa!??

Soma vizuri kitabu cha Esta upate uhondo huo
Aliuawa lakini kwa sababu ya mordekai Baada ya mordekai kufichua siri za walinzi wa ikulu kutaka kumuua mfalme ahasuero hapa ndipo chuki kati ya haman na mordekai ilipoanza na hamani alikufa kwa sababu ya kisa hiki sio kumuoa vashti
 
Nakubaliana nawe kuhusu kifo hicho.
Ila kwa akili ya Hamani nafikiria kuwa alimchukua Vashti na kumfanya mchepuko wake , uasi ni pamoja na kusalandia ex wa mfalme.

Ninewaza tu[emoji2] [emoji2]
 
Alichofanya Vashti kwa mfalme kinastahili kwa wanaume katili wanaothubutu kuwahasi wenzao kama maksai na kuwafanya matowashi ili wahudumu mbele ya wake zao bila kudindisha
 
Nakubaliana nawe kuhusu kifo hicho.
Ila kwa akili ya Hamani nafikiria kuwa alimchukua Vashti na kumfanya mchepuko wake , uasi ni pamoja na kusalandia ex wa mfalme.

Ninewaza tu[emoji2] [emoji2]
Hakuna ushahidi juu ya hilo lakini
 
Alichofanya Vashti kwa mfalme kinastahili kwa wanaume katili wanaothubutu kuwahasi wenzao kama maksai na kuwafanya matowashi ili wahudumu mbele ya wake zao bila kudindisha
Hii umeipata wapi mkuu kama walinzi walikuwa wanahasiwa
 
Hii umeipata wapi mkuu kama walinzi walikuwa wanahasiwa
Kwenye biblia. Towashi ni mwanaume aliyehasiwa. Miongoni mwa watumwa walichaguliwa baadhi ya wanaume kuwalinda wake wa mabwanyenye. Hawa walihasiwa kuwaondolea uwezo wa kuwaingilia kimwili wake za mabwana hao. Ukizingatia ukweli kuwa mabwanyenye hawa walioa wake wengi ambao ilikuwa muhali kuwahudumia kingono kiufanisi na kwa wakati. Hawa matowashi wangeachwa na urijali wao wangepata urahisi 'kuwanajisi' wake zao ambao waliachwa muda mrefu na mshawasha
 
Baada ya Malkia Vashti kufukuzwa na kutotakiwa kurudi Ikulu, Ikapita kipindi Mfalme hasira zimepoa akaanza mtamani arudi. Ila kwa vile ilishawekwa sheria asije samehewa kabisa, ikabidi wafanyakazi waje na Tamasha la Urembo kumchagulia Mfalme mke mzuri ndio anakuja patikana Esta/Ester. Kumbuka hili 'shindano la urembo' lilikuwa ni mabikra wanaenda kulala na Mfalme usiku mmoja mpaka atakapopata 'Papuchi' tamu!.

Malkia Vashti alikuwa ni mtoto wa Mfalme Belshazzar wa Babylonia, iliyovamiwa na hawa wa pershi (Daniel 5). Mfalme Belshazzar alipouwawa, alichukuliwa mtoto wake wa kike akaozeshwa kwa huyo Mfalme.
Kisa cha kukataa ni sababu alikulia mazingira ya ustaarabu wa kifalme na Mfalme(mumewe) alitaka aje kuonyesha uzuri wake mbele ya wageni wake (aje uchi watu waone tamuu - Esta 1:10–11).

Hakikuwa kiburi!
 
Malkia Vashti aasi amri ya mfalme Ahasuero

1Mfalme Ahasuero, alipotawala ufalme wake ulikuwa mikoa 127, toka India hadi Kushi.

2 Kiti chake cha enzi kilikuwa katika mji mkuu Susa.

3Mnamo mwaka wa tatu wa utawala wake, mfalme Ahasuero aliwaandalia karamu viongozi na watumishi wake wa serikali, wakuu wa majeshi ya Persia na Media, watu maarufu na wakuu wa mikoa.

4Basi, kwa muda wa miezi sita, Ahasuero akaonesha utajiri wa ufalme wake mtukufu, na fahari ya utawala wake.

5Muda huo ulipomalizika, mfalme aliwaandalia karamu watu wote wa mji mkuu wa Susa, wakubwa kwa wadogo. Karamu hiyo iliyochukua muda wa siku saba, ilifanyika uani, katika bustani ya ikulu.

6Mahali hapo palikuwa pamepambwa kwa mapazia ya pamba ya rangi nyeupe na vitambaa vya rangi ya buluu. Mapazia hayo yalikuwa yamefungiwa pete za fedha kwa kamba za kitani safi za zambarau, na kuninginizwa kwenye nguzo za marumaru. Makochi ya dhahabu na fedha yalikuwa yamewekwa kwenye sakafu iliyotengenezwa kwa vijiwe vya rangi, marumaru, lulumizi na mawe ya thamani.

7Watu walipewa vinywaji katika vikombe mbalimbali vya dhahabu, naye mfalme alikuwa mkarimu sana wa divai ya kifalme.

8Kila mtu alikunywa akashiba; mfalme alikuwa ametoa maagizo kwa watumishi wa ikulu wamhudumie kila mtu kadiri ya mahitaji yake.

9Wakati huo huo, malkia Vashti naye aliwaandalia akina mama karamu ndani ya ikulu ya Ahasuero.

10Siku ya saba ya karamu hiyo, mfalme Ahasuero, akiwa amejaa furaha kutokana na divai aliyokuwa amekunywa, aliwaita matowashi saba waliomhudumia yeye binafsi: Mehumani, Biztha, Harbona, Bigtha, Abagtha, Zethari na Karkasi.

11Aliwaamuru hao wamlete kwake malkia Vashti, akiwa amevaa taji yake ya kimalkia. Malkia huyo alikuwa na sura ya kuvutia sana, hivyo mfalme alitaka kuwaonesha wageni wake na viongozi uzuri wake.

12Lakini matowashi hao walipomweleza malkia amri ya mfalme, Vashti alikataa kutii. Jambo hilo lilimwudhi sana mfalme, akawa anawaka hasira moyoni.

13Ilikuwa desturi ya mfalme kupata mawaidha kutoka kwa wenye hekima, hivyo aliwaita wanasheria na mahakimu ili wamshauri la kufanya.

14Washauri wake wa kawaida walikuwa Karshena, Shethari, Admatha, Tarshishi, Maresi, Marsena na Memukani – viongozi saba wa Persia na Media waliokuwa na vyeo vya juu kabisa katika utawala wake.

15Aliwauliza hivi: “Je, kulingana na sheria, afanyiwe nini malkia Vashti? Maana, nimewatuma matowashi wangu kwake, lakini yeye amekataa kuitii amri yangu, mimi mfalme Ahasuero!”

16Hapo Memukani akamwambia mfalme na viongozi wake, “Licha ya kumkosea mfalme, malkia Vashti amewakosea viongozi na kila mtu katika mikoa ya mfalme Ahasuero!

17Tendo hili la malkia Vashti litajulikana na wanawake wote, nao watawadharau waume zao, wakisema: ‘Mfalme Ahasuero aliamuru malkia Vashti aje kwake, lakini yeye akakataa.’

18Leo hii, mabibi wa Persia na Media ambao wamesikia alivyofanya malkia Vashti, watakuwa wanawaeleza viongozi wako; hivyo dharau na chuki vitajaa kila mahali.

19Basi, ukipenda, ewe mfalme, toa amri rasmi Vashti asije tena mbele yako. Amri hiyo na iandikwe katika sheria za Persia na Media, ili isiweze kubadilishwa. Kisha, cheo chake cha umalkia, apewe mwanamke mwingine anayestahili zaidi yake.

20Amri hiyo itakapotangazwa katika eneo lote la utawala wako, kila mwanamke atamheshimu mume wake, awe tajiri au maskini.”

21Wazo hilo lilimpendeza sana mfalme na viongozi wake, akatekeleza kama alivyopendekeza Memukani.

22Basi, akapeleka barua kwa kila mkoa kwa lugha na maandishi yanayoeleweka mkoani: Kwamba kila mwanamume awe bwana wa nyumba yake, na kuitangaza habari hii kwa lugha yake.View attachment 862824

Nimependa hapo ILIKUWA KAWAIDA YA MFALME KUTAKA USHAURI KABLA HAJACHUKUA MAAMUZI.

Jamani watu wajifunze kutaka ushauri kama viongozi ili kuepuka kukurupuka
 
Baada ya Malkia Vashti kufukuzwa na kutotakiwa kurudi Ikulu, Ikapita kipindi Mfalme hasira zimepoa akaanza mtamani arudi. Ila kwa vile ilishawekwa sheria asije samehewa kabisa, ikabidi wafanyakazi waje na Tamasha la Urembo kumchagulia Mfalme mke mzuri ndio anakuja patikana Esta/Ester. Kumbuka hili 'shindano la urembo' lilikuwa ni mabikra wanaenda kulala na Mfalme usiku mmoja mpaka atakapopata 'Papuchi' tamu!.

Malkia Vashti alikuwa ni mtoto wa Mfalme Belshazzar wa Babylonia, iliyovamiwa na hawa wa pershi (Daniel 5). Mfalme Belshazzar alipouwawa, alichukuliwa mtoto wake wa kike akaozeshwa kwa huyo Mfalme.
Kisa cha kukataa ni sababu alikulia mazingira ya ustaarabu wa kifalme na Mfalme(mumewe) alitaka aje kuonyesha uzuri wake mbele ya wageni wake (aje uchi watu waone tamuu - Esta 1:10–11).

Hakikuwa kiburi!

Hii ni tafsiri yako. La sivyo toa reference kwa kuainisha mistari inayozungumzia hayo
 
Back
Top Bottom